Tafuta

Vatican News
Maaskofu nchini Argentina katika harakati za kupinga sheria ya utoaji mimba Maaskofu nchini Argentina katika harakati za kupinga sheria ya utoaji mimba  (©unlimit3d - stock.adobe.com)

Argentina:Tamko la Maaskofu kuhusu utoaji mimba:maisha ni hadhi daima!

Maaskofu wa Jimbo Kuu la Buenos Aires nchini Argentina wameandika ujumbe wao mara baada ya mpango wa bunge kutaka kuhalalisha utoaji wa mimba na kwa maana hiyo wanasema kila maisha yana hadhi yake.Inawahumiza na kuwatia uchungu sana.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kila maisha daima yana hadhi yake. Amesema hayo Askofu Mkuu wa Buenos Aires, Kardinali Mario Aurelio Poli, na maaskofu mwengini wa Majimbo katika barua iliyotolewa kufuatia idhini ya Bunge la Sheria la jimbo la Buenos Aires, kuhusu ajenda ambayo inataka rasimu ya sheria ya serikali kuhalalisha kutoa mimba kwa hiari ya ujauzito. Chaguo ambalo, kulingana na maaskofu, linapingana na dhamana ya kikatiba kwa ajili kulinda maisha. Na kwa maana hiyo wanathibitisha kwamba hawapingi haki za wanawake, lakini katika kupendelea maisha kwa njia inayojidhihirisha na katika hali zote.

“Inatuumiza na kututia uchungu, kwamba katikati ya maambukizi mabaya, ya kifo ambayo wafanyakazi wengi wa afya na wafanyakazi katika huduma muhimu wanathubutu na kuhatarisha maisha yao ili kuokoa wale kaka na dada zao, wabunge wanachukulia kuwa inafaa kuendeleza sheria, ambayo kiukweli hailingani na ‘kuheshimu maisha’, kama tunavyopenda kusikiliza na kuimba.”

Ujumbe huo wa maaskofu unaendelea: “Haki ya kutoa mimba iliyotangazwa, hasa kwa wasichana walio katika mazingira magumu zaidi na  ambao, kulingana na hoja zilizowekwa, wasingekuwa na chaguo isipokuwa kwenda kutoa mimba kinyume cha sheria, wanapingana na utashi wa  wasichana wengine wengi ambao wamejiweka katika kuchezea maisha”.

“Tunaelewa kuwa afya iko hatarini, maaskofu bado wanaandika, lakini pia tunaelewa kuwa afya haiwezi kupatikana kwa kumbagua mwanadamu mwingine. Ndiyo maana,wanawake ambao wanaishi katika mitaa mibovu zaidi, utoaji mimba ni uzoefu kama mchezo wa kuigiza, wa kibinafsi na wa kijamuiya. Hapa linafuata wazo la maana sana: siyo ubinadamu wa kupendelea dhaifu dhidi ya mwingine aliye  dhaifu  zaidi”.

20 July 2020, 13:21