Janga la Covid-19 licha ya madhara makubwa kimwili, kijamii na kiuchumi lakini pia athari za kisaikolojia. Janga la Covid-19 licha ya madhara makubwa kimwili, kijamii na kiuchumi lakini pia athari za kisaikolojia. 

AFRIKA#Coronavirus:Amecea yazindua mpango wa misaada kisaikolojia na kiroho kwa watu waathiriwa wa janga!

Usaambaji wa virusi vya Corona na sheria kali za kuzuia maambukizi zilizochukuliwa na Serikali zinaendelea kuleta matokeo hasi juu ya maisha ya watu na wataalam.Kutokana na hilo Amecea imezindua mpango wa kuweza kusaidia kisaikolojia na kioroho kwa watu waathirika.Mpango iliozinduliwa mwanzoni mwa Julai na utaanza kutumika mwanzoni kwa Agosti ijayo.

Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican

Program ya msaada wa kijamii, kisaikolojia na kiroho wa watu wote ambao wameguswa sana na matokeo haya ya kisaikolojia kutokana na janga la virusi au covid-19, na ambao ni wahudumu wa kichungaji, mapadre, watawa wa kike na kiume, wafanyakazi katika taasisi katoliki, wahudumu wa kiafya, lakini pia hata raia wa kawada ambao wanahudumu katika majengo ya kidini. Mpango huu ambao umeundwa katika Kitengo cha kichungaji cha Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (Amecea) kitawahusu Nchi zote wanachama wa wa Amecea katika nchi ya Ethiopia, Eritrea, Sudan, na Sudan Kusini, Uganda, Kenya, Tanzania, Malawi na Zambia.

Kwa mujibu wa mahojiano na Mratibu wa Mpango huo Padre Emmanuel Chimomboha yaliyotolewa katika blog ya Amecea amebainisha kuwa “Usaambaji wa virusi vya Corona na sheria kali za kuzuia maambukizi zilizochukuliwa na Serikali zinaendelea kuleta matokeo hasi juu ya maisha ya watu na wataalam”. Aidha “Watu wengi wamepoteza kazi zao na kuleta mvutano mkubwa wa kihisia, baadhi wameogopa sana na kutishwa na wengine wamekumbwa kiuchumi”.

Lengo kuu la program hii pia ni kuwafanya waelewe ni jinsi gani watu wanakabiliana na mgogoro huo. “Tunajua kuwa serikali na mashirika mengine yanaendelea kuwasaidia watu wengi kwa ngazi ya zana na kifedha, lakini sisi tunataka kuchangia kwa namna tofauti hasa ya kuwa na mpango wa kiroho” amebainisha Padre Chimomboha. Mpango huo umezinduliwa mwanzoni mwa Julai, lakini huduma yake itaanza kufanya kazi kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi Agosti.  Kuhusiana na mana ya utoaji wa msaaada huu wa kisaikolojia utatolewa katika aina mbili: Kwanza ushauri wa mtu binafsi, na kupitia redioni.

Katika huduma ya ushauri wa mtu binafsi, kila Baraza la Maaskofu wataweka mtaalam anayestahili. Mashauriano yatafanyika karibu katika mtandano au kwa njia ya simu, lakini siyo kuonana moja kwa moja, ili kupunguza hatari ya kuambukiza, kama inavyopendekezwa na mamlaka, Padre Chimomboha anabainisha.

Kwa kutumia ushauri kwa njia ya redio ya pamoja kila Baraza la Maaskofu watabaini mtangazaji katika uwezekano wa masafa mazuri kwenye eneo hilo na mshauri ambaye atafaa kipindi kwa karibu saa moja kila siku na ambaye ataweza kuzungumza pia na wasikilizaji katika kutoa maoni yao. Katika tukio ambalo mtu hawezi kuongea juu ya shida fulani kwenye redio na anahitaji umakini wa mtu binafsi, atawasiliana na mshauri binafsi ambao watakuwa wamewekwa kwa ajili hiyo.

Lengo ni kufikia angalau 60% ya idadi ya watu katika kila nchi. Ni lengo kubwa sana ambalo Padre Chimomboha anakiri kwa sababu watu wengi hawawezi kumudu njia tunazotaka kutumia. Changamoto nyingine amesema inawakilishwa na kuunganishwa kwa sababu katika nchi nyingine mawasiliano yana shinda au haitoshi, lakini nusu ya jambo moja ni bora kuliko kukosa kabisa anasema Padre. Amecea pia itaratibu hata maoni ya mpango huu na kushirikishana uzoefu wa wanasaikoloji ambao watafanya mara mbili kwa wiki ili kubaini masuala ambayo yanahitaji umakini maalum na kwa upande wake kutoa ushauri na maelekezo.

20 July 2020, 13:34