Hatua zilizochukuliwa katika kudhibiti wa usambaaji wa virusi nchini Uholanzi ni lazima kuvaa barakoa katika njia zote za usafiri. Hatua zilizochukuliwa katika kudhibiti wa usambaaji wa virusi nchini Uholanzi ni lazima kuvaa barakoa katika njia zote za usafiri. 

UHOLANZI#coronaviru:Barua ya maaskofu katika fursa ya Pentekoste 2020

Katika miezi ya mwisho haikuwa rahisi,kwani ilikabiliwa na vifo,upweke,umbali na kupoteza kazi kwa wengi.Ni maelezo yaliyomo kwenye barua ya Maaskofu katoliki nchini Uholanzi kwa waamini wakati wa fursa ya sikukuu ya Pentekoste tarehe 31 Mei 2020.Aidha wanajibu waliolalamikia Kanisa kuwa hatua zilizochukuliwa zilikuwa za lazima kwa ajili ya kulinda afya ya kila mmoja na kuokoa maisha ya walio wengi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika barua iliyotumwa kwa waamini kwenye fursa ya Siku kuu ya Pentekoste, Maaskofu wa Uholanzi wanazungumzia kuhusu kipindi kigumu walichokumbana nacho wakati wa sehemu ya kwanza ya janga la virusi vya corona au covid-19. Na zaidi wanaelezea juu ya kile kipindi ambacho hakitasahulika kwa upande Kanisa, kwa sababu ya kufungwa kwa maparokia, ambapo walitakiwa kuandaa kwa upya namna ya utendaji wa shughuli za kichungaji ili zipate kuendelea bila kuacha. Kwa maana hiyo wanasema “miezi ya mwisho haikuwa rahisi kwa maana ilikabiliwa na vifo, upweke, umbali na kupoteza kazi.”

Makanisa yalifungwa na kubaki na kuadhimisha misa kwa njia ya mtandao

Katika barua hiyo aidha wanabainisha ni jinsi gani makanisa yao yalikuwa matupu bila kuadhimisha misa  na waamini, huku maadhimisho yakiwafanyika kwa njia ya mitandao bila mawasiliano ya ukaribu wa waamini. Yote hayo haijawahi kutokea! Kutokana na kurudia kwa upya sasa kuandhimisha Ibada za Misa  wanasema inawezekana kabisa kuwa na utambuzi ya kwamba  Bwana yupo pamoja daima na hakuacha yoyote kamwe. Maaskofu pia wamewashukuru wale wote ambao kwa sasa wanaendelea kuhakikisha usalama katika maparokia ili kuhakikisha  kuwa sheria na kaununi zote zilizowekwa na vyombo vya serikali zinafuatwa. “tuombe ili Roho Mtakatifu atuangazie na kutujaza mioyo yetu” inasomeka barua hiyo. 

Hatua zilizochukuliwa na Kanisa ni kwa ajili ya kulinda afya ya kila mtu

Kwa kuwageukia wale wote ambao wamejaribiwa na hasira na kukata tamaa wakati wa kipindi cha kwanza cha kuwekwa karantini, Maaskofu wanaandika“ Imesikika malalamishi kuwa Kanisa lilitakiwa kusikia sauti yake na kutenda kwa kiasi kikubwa hasa cha kujitegemea. Tunajibu kuwa hatua zilizochukuliwa zilikuwa za lazima kwa ajili ya kulinda afya ya kila mmoja na kuokoa maisha ya walio wengi”.

Licha ya ufunguzi wa shughuli,maambukizi bado yapo

Hata hivyo katika nchi hiyo bado inaendelea kuorodhesha kesi mpya kwa mujibu wa mamlaka ya Afya. Baadhi ya watu wamefariki kwa siku za hivi karibuni kama walivyothibitisha Wizara ya Afya na sasisho la waathirika wamefikia 5,951 na wakati  maambukizi mapya yaliyothibitishwa ni 131, kwa kufikisha jumla ya watu  46.257 walioambukizwa na virusi vya corona.

01 June 2020, 12:43