Vatican News
Msimamizi wa kitume wa Kanisa Kuu la Manila anaomba waamini wazingatie sheria katika Kanisa na wakati huo serikali kuzingatia huduma ya kidini ni kwa ajili ya watu wote. Msimamizi wa kitume wa Kanisa Kuu la Manila anaomba waamini wazingatie sheria katika Kanisa na wakati huo serikali kuzingatia huduma ya kidini ni kwa ajili ya watu wote.  (ANSA)

UFILIPPINI#coronavirus.Kanisa la Manila:shughuli za kidini ni huduma msingi!

Twende mbele ni jina la Barua ya Kichungaji iliyoandikwa na Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Kuu la Manila nchini Uffippilini akitoa wito kwa serikali kuzingatia shughuli za kidini kama huduma msingi kwa ajili ya watu wao.Na kwa waamini wafuate ushauri uliotolewa na jimbo kwa mujibu wa sasisho la wizara ya Afya nchini.Makuhani wasikilize waamini na kushirikishana mawazo yao kwa ajili ya kusaidia wanaohitaji zaidi.

Sr.Angela Rwezaula – Vatican

Huduma ya kidini ni msingi kwa ajili ya watu wetu, ndiyo wito uliotolewa kwa serikali uliomo katika Barua ya Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Kuu katoliki la Manila Ufippini, Askofu Broderick Pabillo. Barua ya Kichungaji iliyopewa jina “Twende mbele” wa hakika Askofu anabainisha juu ya kanuni zinazotumika wakati huu wa janga la virusi vya corona na hasa kwa serikali  baada ya kuweka vizingiti  vya maadhimisho ya kidini kwa uwepo wa watu kumi tu, bila kuzingatia ukubwa tofauti na uwezo wa maeneo ya  kufanyia ibada katika Makanisa hayo.

Wakati huo huo, Askofu katika barua yake amewashauri waamini bado aendelee kuheshimu miongozo iliyoanzishwa na Jimbo Kuu na iliyosasishwa na Idara ya Afya ya nchi hiyo kwani anasema  ni muhimu, kwa sababu “kila mmoja wetu lazima azingatie siyo afya ya mtu binafsi lakini pia hata ya wengine”. Kwa njia nyingine msimamizi huyo  anahamasiaha kanuni za janga na hasa la kukaa nyumbani kwa wazee au wagonjwa; kuwasaidia wanaohitaji zaidi hasa katika mantiki ya msaada wa Kanisa la umoja kwa ajili ya kushirikiana ili kwa pamoja inawezekana kutembea pamoja katika hali hiyo.

Na kwa upande wa Makuhani, Msimamizi wa kitume jimbo Kuu Manila  anabainisha juu ya umuhimu wa kusikiliza mawazo ya waamini wenyewe wakati wa kipindi hiki na ili kuleta pamoja ushiriki hai wa maisha ya Kanisa. Askofu Pabillo amewaachia kila parokia na vyama vya kitume kupanga shughuli zao binafsi katika kipindi hiki  kwa kutoa mwaliko wa kuacha nafasi katika “shughuli za  uchungaji wa afya hasa kwa wazee na wagonjwa ambao hawawezi kwenda Kanisani. Mungu ni yupo hai hata katika kipindi hiki kipya kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye anazidi kuvuvia na kwa maana hiyo ni vema kung’amua na kumfuata, amehitimisha Askofu Pabillo. 

03 June 2020, 15:34