Katika janga la virusi, wazee wamekuwa ni waathirika sana katika taasisi na nyumba za kutunzia wazee kuliko wanaokaa katika jumuiya zao. Katika janga la virusi, wazee wamekuwa ni waathirika sana katika taasisi na nyumba za kutunzia wazee kuliko wanaokaa katika jumuiya zao. 

Siku ya kupinga manyanyaso kwa wazee:Kuna haja ya mfumo wa haki ya utunzaji na msaada kwa wazee!

Bila wazee hakuna wakati endelevu.Hakuna huduma ya afya ya upendeleo.Ndiyo kauli mbiu ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika wito wa kimataifa na ambapo wamerudia kuutoa wakati wanaadhimisha “Siku ya Kupinga manyanyaso kwa wazee”,iliyofanyika tarehe 15 Juni katika mataifa yote mahali ambamo wanatenda utume wao.Kuna haja ya mfumo unaotoa kipaumbele cha haki ya utunzaji na msaada kwa wazee.

Katika Siku ya kupinga manyanyaso kwa wazee ulimwenguni, ambayo imeadhimishwa tarehe 15 Juni na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Nchi zote mahali ambamo jumuiya ilipo katika utume wake, Jumuiya imehimiza kwa mara nyingine tena kuendeleza na ukusanyaji wa saini ya wito wake kimataifa unaoongozwa na kauli mbiu “Bila wazee hakuna maisha endelevu. Kurudisha ubinadamu kwa upya katika jamii zetu dhidi ya huduma ya afya ya upendeleo".

Muktadha huo ambao  kama watia  saini wake wa kwanza Andrea Riccardi, mwanahistoria na Mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio; Romano Prodi, Waziri Mkuu Mstaafu na wa Tume ya Umoja wa Ulaya; Jeffrey D. Sachs, Mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mtandao wa Suluhisho la Maendeleo Endelevu; Aleksandra Dulkiewicz, Meya wa jiji la Danzika, Poland; Simonetta Agnello Hornby, Mwandishi wa vitabu nchini Uingereza; Vile vile Manuel Castells, Profesa wa Masuala ya kijamii katika Chuo Kikuu cha California Berkeley, kutoka Uhispania; Irina Bokova, Mkurugenzi Mtaafu wa UNESCO, na mjumbe wa Kamati Kuu ya Udugu wa Kibinadamu, wa Bulgaria; Mark Eyskens, Waziri Mstaafu wa Ubalgiji; Hans Gert Pöttering, Spika Mtaafu wa Bunge la Ulaya wa Ujerumani; na majina mengine muhimu, ya Ulaya  na ulimwenguni wameongeka wengine. 

Hii ni kwamba katika siku chache zilizopita wameona utekelezwaji wa makumi ya maelfu ya raia pamoja watu wengine wanaojulikana katika  sekta tofauti, ikiwa ni pamoja na mbunifu Renzo Piano, katibu wa CISL, Anna Maria Furlan, aliyenusurika kifo cha kimbari dhidi ya Wayahudi (Shoah)Sami Modiano, mwandishi Paolo Rumiz, mtangazaji wa runinga Flavio Insinna na mtunzi na mwimbaji Claudio Baglioni.

Wito huu unazaliwa kutokana na hali halisi iliyoonekana ya idadi kubwa ya waathirika wa Covid-19  ambao miongoni mwao ni wazee, kwa namna ya pekee walioko katika taasisi za kutunzwa wazee, na nyumba za wazee  na kwa njia hiyo Jumuiya hiyo  inapendekeza mabadiliko ya  kina na ya kiakili ambayo yapelekee kuanzisha mambo mapya ya kijamii na kiafya.

Ripoti ya Shirika la Afya ulimwenguni WHO kunako mwaka 2018 ilikuwa limekwisha onyesha kwamba kiukweli “katika taasisi, viwango vya unyanyasaji ni vikubwa zaidi kulinganisha na mazingira ya kijumuiya” na ni pamoja na ukatili  kadhaa ikiwemo vizuizi vya mwili, kunyimwa hadhi, utekelezaji wa kazi za kila siku, utoaji duni kwa makusudi katika utunzaji, uzembe na unyanyasaji wa mfadhaiko”.  Hali halisi ilizidi kuwa mbaya hasa wakati wa janga la Covid-19 lililosababisha  kama inavyojulikana kwamba  kiwango kikubwa cha watu waathirika ndani ya taasisi, karibu ni mara mbili ya idadi ya wazee wanaoishi nyumbani, kulingana na takwimu zilizotolewa  na Taasisi ya Juu ya afya.

Kwa sababu hiyo, katika Siku ya kupinga manyanyaso ya wazee ulimwenguni  ambayo imeadhimishwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio pamoja na wito kimataifa, pia Jumuiya hiyo imewasilisha hata kwa serikali za mikoa na wilayani lile hitaji kubwa la kufika kwa haraka iwezekanavyo ule mfumo ambao unatoa kipaumbele cha haki ya utunzaji na msaada kwa wazee.

16 June 2020, 11:39