Tafuta

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni  Mchungaji Martin Junge ametuma barua yake kwa Kardinali Kurt Koch,Rais wa Braza la Kipapa la uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni Mchungaji Martin Junge ametuma barua yake kwa Kardinali Kurt Koch,Rais wa Braza la Kipapa la uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo 

Shirikisho la Kilutheri la pongeza Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo!

Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni limetuma barua kwa Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo (PCPCU) wakikumbuka juu ya uhusiano wa kidini ambao umekuwapo kwa muda mrefu katika fursa ya Baraza la kipapa kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Sekretarieti ya uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo ilianzishwa kunako tarehe 5 Juni 1960 na Papa Yohane XXIII ili kuwezesha ushiriki wa viongozi wa uangalizi  wasio Wakatoliki katika Mtaguso II wa Vatican. Mkutano huo muhimu wa maaskofu Katoliki kutoka ulimwenguni kote ulifunguliwa miaka miwili baadaye kunako Oktoba 1962 na kumaliza kikao chake cha mwisho kunako Desemba 1965. Sekretarieti ya uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo ilibadilishwa jina lake kunako mwaka 1988 na  kuwa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kristo. Kwa njia hiyo katika kuadhimisha miaka 60 ya Baraza hilo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kilutheri duniani (LWF), Mchungaji  Dk. Martin Junge ametuma barua yake  kwa Rais wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Kikristo  (PCPCU), Kardinali Kurt Koch, kufuatia na fursa ya kutimiza  miaka 60 tangu kuanzishwa Baraza hili la  kiekuemene Vatican.

Katika barua ya kuwapongeza, Kiongozi wa kilutheri amesema kuwa miaka 60 iliyopita katika ofisi hiyo imejikita kwenye katika  mchakato wa kuendeleza nyayo za uekumene. Hata kabla ya Mtaguso wa II wa Vatican, Mchungaji Junge  amebainisha kuwa  Sekretarieti ya Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo chini ya maono ya uongozi wa Kardinali Bea walianza kufanya kazi katika mwelekeo wa Mtaguso na kusaidia kuandaa hati kadhaa pamoja na maelezo kuhusu uekumene “Unitatis Redintegratio.”  Aidha katika barua yake kwa Kardinali, Mchungaji Junge ameandika kwamba Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Kikristo (PCPCU) na Shirikisho la Kilutheri Ulimwengunini (LWF) wamekuwa na uhusiano wa muda mrefu na wenye kuzaa matunda, kwani tangu mwaka  1965 wamekuwa na Tume ya kwanza ya pande zote mbili ya Kilutheri na Katoliki kuhusu Umoja.

Kiongozi wa Kilutheri anakumbuka nyaraka kadhaa muhimu zilizotolewa na Tume, ikiwemo ya 1980 isemayo “Wote ndani ya Kristo” na ile ya 1999 juu ya “Mafundisho ya Haki”  ambayo inasema, “inaongoza kazi yetu ya kiekumene hadi leo.”Kwa pamoja, ushiriki wetu unaoendelea wa kihistoria unahitaji kuwajibika kwa wito wa Mungu na shauku  ya watu wetu kwa umoja”. Amesisitiza kiongozi huyo.  Aidha Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni  anakumbusha historia ambayo haitasahaulika kuhusu  maadhimisho ya Miaka 500 tangu ya mageuzi ya Kanisa lao wakiwa na Papa Francisko,iliyofanyika huko Sweden kunako Oktoba 2016. Anatoa shukrani kubwa za kina  kwa  Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo (PCPCU) kwa kazi yake na ushuhuda, kwani amesema, linahakikisha kwamba kazi ya uekumene unabaki moyoni mwa Kanisa Katoliki. Vile vile amesisitiza kuwa; pamoja na mchakato wa kuendeleza uekumene unahitaji kuwajibika kutimiza wito wa Mungu na shauku ya  watu wote  ajili ya umoja.

Mchungaji Junge anamshukuru Kardinali Kurt Koch kwa uongozi wake wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo ambapo amenukuu maneno ya Rais wa Shirikisho la Kulutheri Ulimwenguni ( LWF), Askofu Mkuu Panti Filibus Musa kwa Papa Francisko wakati wa fursa ya kukutana kwao kwa mara ya kwanza  Vatican: “Tumeanza safari yetu isiyoweza kubadilika kutoka katika mgongano hadi muungano,  kwa maana hiyo tusitamani kuruhusu usimame tena”. Katika maadhimisho haya ya miaka 60, barua inathibitisha kuwa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni linafurahi naye pamoja na Kanisa lote kumshukuru Mungu kwa ushuhuda wa wito wa Injili: Ut unum sint” , yaani “ ili wawe na  umoja”.

Ni miaka 60 iliyopita kwa utashi wa Papa Yohane XXIII alipoanzisha kwa uthabiti mwelekeo mpya katika maisha ya dhati ya Kanisa Katoliki katika uhusiano wa Makanisa mengine na Umoja wa Wakristo. Kuanzishwa Sekretarieti kwa ajili ya Umoja wa Wakristo ambapo kwa sasa inajulikana kama Baraza la Kipapa la  Uhamasishaji wa Wakristo ilikuwa ni sehemu fungamani ya usasishaji ambao ukatoliki ulikuwa unahisi mahitaji makubwa kwa kipindi kirefu. Sekretarieti hiyo ilikuwa chini ya uongozi wa rais wa kwanza Kardinali Augustin Bea, ambaye alipewa majukumu ya kila siku ya mtaguso, kati ya mambo mengine ilikuwa ile ya hali ya kuishi migawanyiko ya kizamani na mashindano katika ulimwengu wa kikristo na msimamo wa umoja ambao ulipendelewa na Bwana mwenyewe “Ut unum sint” “ Ili wawe na umoja (Giovanni, 17, 21), ”.

Kazi hiyo ilijiwakilisha kama changamoto ya kweli na ngumu.  Na ili wakatoliki waweze kuwa na msukumo wa kiekumene ambao tayari ulikuwa ujengwa kati ya waprotestanti na waorthodox, kulikuwa na ulazima  msingi wa matarajio ya Kanisa  na kama ilivyo asili yake na juu ya thamani za jumuiya nyingine za kikristo. Mara nyingi tunasahau kwa urahisi ya kwamba sehemu kubwa ya maaskofu waliounganika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro tarehe 11 Oktoba 1962 ili kuanza Mtaguso, kwa sababu ya mafunzo yao, ulikuwa unamwilishwa na kuamini kuwa nje ya Kanisa katoliki wapo ambao wanapinga. Zawadi  ya miujiza, mikuu ya kizamani ya Mungu kwa Kanisa ni kwamba katika miaka minne tu ya Mtaguso , maaskofu hao hao walifika na maono ya Kanisa la kupyaishwa kwa kina na ambao katika muda huo na baadaye ingeweza kuonekana mambo mapya hata ya kuleta wasi wasi, lakini kiukweli ilikuwa ndiyo mchakato mpya  katika uthabiti wa kukimbilia umoja wa Kanisa.

Katika upyaisho wa maono ya kikanisa, mababa wa mtaguso walifikia kutambua kuwa Makanisa mengine na Muungano wa kikristo katika fumbo la wokovu siyo tu wenye maana kubwa na thamani (Unitatis redintegratio, 3), na zaidi Roho wa Kristo hajakataa kutumia kama vyombo vya wokovu (ibidem). Matokeo yake ni  jukumu la kuunda umoja wa wafuasi wa Kristo ulijionesha  kuwa na hitaji kubwa sana. Mwendelezo mwema  Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa  Ukristo ilianza kuwa na maendeleo haya wakati na baada ya Mtaguso kuandika vizuri hati  na ndiyo inakumbusha na kusherehekea kwenye kumbukumbu hii ya miaka 60. Kwa miaka mingi, uhusiano wa kidugu na Wakristo wengine na mazungumzo ya kitaalimungu yenye lengo la kushinda mgawanyiko umeongezeka na kuwa na mafaniko mengi hadi kufikia kubadilisha kwa kina muhili wa ulimwengu wa Kikristo wenyewe. Katika mchakato huo bado Roho Mtakatifu anaendelea kufungua kwa harakati za kidini ambazo zinaonekana kwetu na zaidi zinaelekeza wakati ujao. Kwa maana hiyo mchakato huo unajikita hata katika changamoto ya mshikamano wa kidini na  wazo halisi la mazungumzo.

15 June 2020, 10:41