Papa Francisko na Askofu Mkuu  Alfred Xuereb, Balozi wa Kitume wa Korea na Mongolia Papa Francisko na Askofu Mkuu Alfred Xuereb, Balozi wa Kitume wa Korea na Mongolia 

Papa Francisko amebariki waamini na kuwatia moyo katika ujenzi wa amani ya Korea!

Katika mkutano wa Papa Francisko na Balozi wa Kitume,Askofu Mkuu Xuereb wa Korea amewabariki watu wa Korea wakati katika furusa y kumbu kumbu ya ya miaka 70 tangu kuibuka kwa vita vya wao kwa wao ambavyo vimeleta majanga makuu katika nchi hizo mbili.Kardinali wa Jimbo Kuu la Seoul amewashauri sehemu zote mbili za nchi kuomba msamaha kuanzia kwa viongozi wa kisiasa ili waweze kuwa na amani ya kudumu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amebariki watu wote wa Korea Kaskazini na kusini na kwa namna ya pekee kwa kuwatia moyo wale wote ambao wanaendelea na mchakato wa ujenzi wa amani na kuhamasisha mapatano. Amesema hayo katika mkutano wake kwenye  nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican asubuhi tarehe 25 Juni 2020 na Balozi wa Kitume wa Korea na Mongolia, Askofu Mkuu Alfred Xuereb. “Nimemaliza kukutana na Baba Mtakatitu ambaye amekumbuka kuwa leo hii ni miaka 70 tangu kuibuka kwa vita vya korea ambapo leo hii, maaskofu wa Korea wanaadhimisha misa maalum kwa ajili ya kuomba mapatano”.

Kila mwaka ifikapo tarehe 25 Juni, maaskofu wa Korea walikuwa  na utamaduni wakuunganika pamoja katika Jimbo kuu la Seoul ili kuadhimisha misa  kwa ajili ya kuomba upatanisho. Mwaka huu kutokana na janga la virusi vya corona maaskofu hao wamefanya maadhimisho ya misa kila mmoja katika jimbo lake. Huko (Seoul), kwa mujibu wa Shirika la habari za Kanisa, linabainisha kuwa Kardinali Andrew Yeom Soo-jung, Askofu Mkuu wa Jimbo katoliki hilo ameadhimisha Ibada Takatifu ya Misa asubuhi saa 4.00 kamili, tarehe 25 Juni 2020 katika Kanisa Kuu la Myeongdong.

Katika mahubiri yake, Kardinali Soo- Jun amesema kuwa “kufikia amani ya kweli ambayo watu wote wanatamani ni jambo gumu sana, lakini linawezekana”. Katika misa ambayo imeshiriki na waamini 230 tu kulingana na sheria za usalama dhidi ya maambukizi ya covid -19, amehimiza kuhamasisha amani. Kardinali Yeom Soo-jung ameashauri sehemu zote mbili za nchi ya Korea kuwa na msamaha na kwamba “ikiwa  msamaha utatawala katika  siasa, ni wazi kwamba  haki itageuka kuwa ya kibinadamu na amani ya kudumu zaidi”. Kutokana na hili  Kardinali amesali kwa ajili ya viongozi wote wa kisiasa  ili “waweze kwenda mbali na upeo wa matakwa binafsi, chama na taifa” na waongeze bidii kwa ajili ya amani na kutazama ustawi wa pamoja wa Korea zote mbili kaskazini na Kusini.

Katika ujumbe wa hivi karibuni kwa matazamio ya kumbu kumbu ya miaka 70 tangu mfumko wa vita vya wenyewewe kwa wenyewe,  Rais wa Tume ya Maaskofu katoliki wa kwa ajili ya mapatano ya watu nchini Korea ya Kusin (Cbck), Askofu Lee Ki-heon, alirudia kuhamasisha kuhusu amani ili kuweza kusitisha kabisa vita, moja ya janga la umwagaji damu na mgogoro wa wa kihistoria baada ya vita mbili vya kidunia na  hata kufikia ufutaji wa wa silaha za  nyuklia katika peninsula hiyo.

Makubaliano ya Panmunjom 2018 yalikuwa yameleta shauku kubwa na kuongeza matumaini kwa ajili ya mwanzo mpya.  Lakini Mkutano huo mkuu hakuleta matunda. Kwa mujibu wa Askofu Lee Ki-heon anasema, ukosefu wa matunda hayo unaweza kuwa umesababishwa kwa wale ambao wanajinufaisha mbele ya nchi yao. Katika ujumbe wake  pia alikuwa amebainisha matatizo ya nchi ambayo ni moja katika dunia iliyogawanyika sehemu mbili mahali ambapo vita havijaisha na kuendelea kuona wazalendo wake wanaishi katika vikwazo vya nguvu kwa mantiki ya kidemokrasia.

26 June 2020, 13:25