Tafuta

Vatican News
2020.05.23 Padre Filipe Sungo, Gambera wa Chuo Kikuu Katoliki Msumbiji  (UCM) 2020.05.23 Padre Filipe Sungo, Gambera wa Chuo Kikuu Katoliki Msumbiji (UCM) 

Msumbiji:Maaskofu watoa wito wa amani mkoani Cabo Delgado!

Maskofu nchini Msumbiji wametoa ujumbe kwa nchi yao kuhusu amani hasa kufuatia watu wa Mungu wa Mkoa wa Cabo Delgado ambao kwa miaka mitatu wamekuwa waathiriwa wa kushambuliwa na wanamgambo wa kiislam kutoka nchi jirani au waasi wa ndani,Wanawataka nchi nzima kukomesha udhalimu mwingi na vitendo vya unyanyasaji wa kweli ambavyo vinaendelea katika mkoa huo.

Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kukomesha udhalimu mwingi na vitendo vya unyanyasaji wa kweli ambavyo vinaendelea katika mkoa wa Cabo Delgado. Ni maombi ya sauti kuu ya Baraza la Maaskofu nchini Msumbiji (CEM) mara baada ya Mkutano wao wa mwaka uliofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni huko Matola, katika Seminari ya Mtakatifu Agostino. Mwisho wa kazi yao, maskofu wametoa ujumbe kwa waamini wa Cabo Delgado ambao kwa miaka mitatu wamekuwa waathiriwa wa kushambuliwa na wanamgambo wa Kiislam kutoka nchi jirani au waasi wa ndani. Ni maelfu ya waliokufa na zaidi ya watu 200,000 waliohama makazi yao, hadi sasa.

Maaskofu katika barua yao wamekumbuka ujumbe wa Urbi et Orbi uliotangazwa na Papa Francisko mnamo Jumapili ya Pasaka tarehe 12 Aprili, na  kwa kuzingatia kile kinachotokea, maaskofu wanaomba usikivu na mshikamano kutoka pande za watu wote, hasa katika mwanga wa shida kubwa za kibinadamu ambazo wanapitia. “Tunahitaji majibu ya dharura kwa ajili ya  janga hili  Ujumbe wao unasomeka na kwamba ni lazima waingilie kati  sababu za mizozo pia kupitia uhamasishaji wa mipango ya maendeleo na utoaji wa huduma muhimu, kama zile zinazohusiana na afya na elimu. Wakati huo huo, Baraza la Maaskofu Cem wanatoa shukrani zao kwa familia nyingi na raia wa kawaida ambao wamefungua nyumba zao kuwakaribisha waathiriwa wanaokimbia vurugu na kwamba hiyo wanaonyesha moyo mkuu wa Msumbiji, na ambao unaonyeshwa kupitia mshikamano na ukaribu”, wanasema maaskofu. Aidha wanaongeza “ Bwana hubadilisha mioyo ya wale wanaosababisha uovu” na huku wakihimiza kila mtu kuheshima kwa jina la Mungu na hadhi ya mtu.

Je ni nini namna ya kuishi imani, katika muktadha huu? Baraza la Maaskofu wa Msumbiji (Cem) katika hati yao wanazingatia familia  kuwa ni Kanisa la nyumbani ambalo katika kipindi hiki limetumia wakati mwingi wa sala nyumbani. Kuanzisha kwa upya na kuinua vyombo vya habari kama chombo cha kuinjilisha pia ni muhimu, pamoja na kujitoa kila mtu kuwa Kanisa linalotoka nje na ambalo ni huruma, msamaria, karibu na mateso na watu walioathirika na janga hili, wamesisitiza . Kutokana na hilo ndipo Maaskofu wa Msumbiji wanatoa wito wa kuacha kuwanyanyasa wagonjwa wa Covid-19, badala yake ni kuwaonyesha mshikamano na huruma. Uangalifu zaidi unahitajika kwa watu maskini, ambao hali zao zimezidi kuwa mbaya na shida ya kiafya. Kwa upande huo, Baraza la Maaskofu  (Cem) anasisitiza kujitoa kwao katika sekta ya kijamii, inayotendeka kupitia Caritas, pamoja na lengo la kutaka kuanzisha kikundi kinachofanya kazi ambacho kiko katika mawasiliano ya kudumu na Wizara ya Afya ili kuanzisha njia na nyakati za kuanza tena kwa liturujia  za umma.

Maaskofu wa Msumbiji aidha wametoa wito wa uwajibikaji wa raia, busara na tahadhari kwa wote na kwamba shida huchochea kukomaa na kwa sababu hiyo, janga linaweza kuwa fursa ya kugundua tena uwepo wa Mungu katika maskini na kuwa na dhamiri ya mshikamano kama chombo cha maendeleo ya jamii. “Matumaini ya Kikristo yanayotokana na imani, na ndiyo msindikizaji mwezetu hivyo  ni muhimu kubaki kidete na hai”, wanaandika maaskofu Msumbiji. Hatimaye Mkutano wa maaskofu pia walitafakari juu ya umuhimu wa kuimarisha malezi katika seminari na wakaandaa njia ya maandalizi ya Mkutano wa nne wa Kichungaji wa Kitaifa, uliopangwa kufanyika kunako 2023. Ni mpango wenye mizizi katika urithi ulioacha na ziara ya Papa Francisko nchini Msumbiji kunako Septemba 2019.

19 June 2020, 10:49