Tafuta

Vatican News

MAREKANI:Ask.mkuu Gomes apokea simu kutoka kwa Papa!

Askofu Mkuu Jose Horario Gomez wa Jimbo Kuu Katoliki la Los Angeles na Rais wa Baraza la Maaskofu Marekani,tarehe 3 Juni 2020,amepokea simu kutoka kwa Papa Francisko ya kuwatia moyo na sala kwa wote kutokana na kile tukio lililotolea na kile kinachoendelea hadi sasa nchini humo kufuatia na kifo cha George Floyd ambacho kimezua hisia kali za maandamano ya chuki na ghasia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Askofu Mkuu José H. Gomez wa jimbo Kuu Katoliki Los Angeles na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Marekani, (USCCB) amepokea simu kutoka kwa Papa Francisko Jumatano tarehe 3 Juni 2020 mahali ambapo Papa Francisko ameelezea hisia zake za maombi  huku akiungana na Kanisa na watu wote wa Marekani katika kipindi hiki cha mivutano na ghasia. Askofu Mkuu  Gomez ameshirikisha habari hizi kwa maaskofu wote wa Marekani kwa matumaini kwamba wanaweza kupata faraja na nguvu katika kutiwa moyo na Papa.  Aidha Papa Francisko ametoa shukrani zake kwa maaskofu kutokana na sauti moja ya kichungaji katika majibu ya Kanisa kufuatia na maandamano nchini, tangu kutokea kifo cha George Floyd  na amependa kuwahakikishia maaskofu kuendelea na sala zake na ukaribu katika siku na wiki zijazo. Ameonesha kuendelea kuomba sala yake maalum kwa Askofu Mkuu Bernard A.Hebda na Kanisa mahalia la Mtakatifu Paulo na Minneapolis.

Kwa upande wa Askofu Mkuu Gomez, na kwa niaba ya  Baraza zima la Maaskofu Marekani (Usccb) ametoa shukrani kwa Papa Francisko kwa maneno yake mazito ya kuwaimarisha na kuwatia moyo ambayo aliyatoa wakati wa kumaliza Katekesi yake siku ya Jumatano asubuhi tarehe 3 Juni 2020,na kwa kwa upande wake amemwakikishia sala kwa Papa  Hata hivyo katika maneno ya Papa alisema "haiwezekani kuvumilia ubaguzi wa aina yoyote na wala kufumbia macho kwa kisingizio cha kulinda utakatifu wa maisha. Lakini zaidi na watu wanapaswa kutambua kwamba, ghasia na vurugu za hivi karibuni, zimepelekea watu wengi kujeruhiwa pamoja na uharibifu mkubwa wa mali."

Kwa mujibu wa kile ambacho kinaendelea nchini Marekani, "haiwezekani kutumia mbinu za kisiasa katika kukiuka misingi ya kidini na badala yake ni lazima kutetea haki za kila mtu hata wale ambao hawawezi kukubaliana. Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa ni mtetezi mkuu wa haki na hadhi ya kila mtu". Hili ni tamko na onyo kutoka kwa Askofu Mkuu Wilton D. Gregory wa Jimbo kuu Katoliki la Washington DC, mara baada ya tendo la Rais kuonekana katika madhabahu ya Yohane Paulo II katika hali ambayo siyo ya kawaida.

Hata hivyo baada ya picha za kushtukiza mbele ya Kanisa la Kiaskofu, vyombo vya habari vimeonyesha ziara ya Rais Trump katika Madhabahu ya Kitaifa ya Yohane Paulo II, na mbele ya Kanisa la Kiaskofu karibu na Ikulu, mkononi mwa Rais ukiwa umeinua Biblia. Tendo hilo limeibua mitazamo na maoni tofauti kutoka kwa wachambuzi kadhaa. Wakati huo huo vurugu kali katika mijini, hadi kufikia kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji likiendelea.

Askofu Mkuu Wilton D. Gregory  wa Washington katika hili amesema “Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa ni mtetezi mkuu wa haki na hadhi na heshima  ya kila mtu. Urithi wake ni ushuhuda hai wa ukweli huu. Kiukweli hasingekubaliana na matumizi ya utumiaji wa mabomu ya kutoa machozi na vizuizi vingine vinavyolenga kuwanyamazisha, kuwatawanya au kuwatisha watu hawa kwa sababu tu wamepata fursa ya kupiga picha mbele ya mahali pa sala na amani”.

04 June 2020, 10:16