Tafuta

Vatican News
Wauguzi nchini Kenya na wanaendelendea na harakati za mapambano ya virusi vya corona Wauguzi nchini Kenya na wanaendelendea na harakati za mapambano ya virusi vya corona 

KENYA#coronavirus:Ask.Mkuu Muheria:Msitumie hisani kwa madhumuni

Askofu Mkuu Mheria wa Nyeri na Rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Uchungaji wa Walei nchini Kenya ametoa onyo kwa wanasiasa,wasitumie matendo ya hisani kwa madhumuni yao binafsi,badala yake hisani hizo ni kwa faida ya pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Matendo ya hisani na mshikamano hasa katika kipindi hiki cha janga la corona hayatakiwi kutumika kwa malengo na faida binafsi, badala yake ni kwa ajili ya ustawi wa wote. Ndilo tamko  na ushauri uliotolewa kwa viongozi wa kisiasa, kutoka kwa Askofu Mkuu Anthony Muheria, wa Jimbo Kuu Katoliki la Nyeri na Ris wa Tume ya Uchungaji na Utume wa Walei ya Baraza la Maaskofu Nchini Kenya.

Kila mtu ahisi kuwa familia moja ya mshikamano

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwenye blog ya Amecea, Askofu Mkuu anabainisha kuwa mshikamano ni msingi kwa ajili ya wema wa wote hasa ndugu kaka na dada walio katika matatizo na kwa maana hiyo hisani hizo hazipaswi kuchukuliwa kama kifaa cha kupatia umaarufu na faida za kibinafsi”. Janga la Covid-19, anasisitiza tena Askofu Mkuu Muheria, “linaleta wasiwasi mkubwa kwa watu wetu. Kwa hili, ninawaalika kila mtu katika umoja, ili kuhisi kama familia moja katika mshikamano”.  Kwa namna ya pekee  Askofu Mkuu anawaomba  viongozi wa kisiasa “kuwa mfano bora  kwa kudumisha uhusiano mzuri na wapinzani wao, kwa lengo la heshima hiyo ambayo inaunganisha na inatoa matumaini”.

Siasa zinapaswa kutendwa kwa furaha na amani

Askofu Mkuu wa Nyeri amethibitisha kwamba “Kiukweli, siasa zinapaswa kufanywa kwa furaha na amani, siyo kwa chuki. Mungu anawategemea ninyi, na kuongeza kuwa “Hakikisha kwamba Bwana yuko katika vitendo vyenu, ili muweze kutenda kwa uwajibikaji na busara na muwe watu wa  upendo na umoja”, amehitimisha Askofu Mkuu Muheria. Itakumbukwa kwamba, wa mujibu wa takwimu zilizosasishwa hadi Mei 31, zimethibitishwa kesi  za Covid-19 nchini Kenya 1,848, na watu 464 wamepona wakati huo huo  watu  63 wamekufa.

01 June 2020, 10:20