Tafuta

Vatican News
Maaskofu wa Congo Brazzaville wanashukuru jitihada za serikali mbele ya kukabiliana na janga la virusi lakini  wanaomba waendelee katika mwelekeo huo kwa waathirika zaidi. Maaskofu wa Congo Brazzaville wanashukuru jitihada za serikali mbele ya kukabiliana na janga la virusi lakini wanaomba waendelee katika mwelekeo huo kwa waathirika zaidi.  (AFP or licensors)

Brazzaville#coronavirus:Janga la virusi lipelekee uongofu wa kila mmoja!

Katika Ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa Congo Brazzaville mara baada ya mkutano wamebainisha kuwa matukio ambayo yameleta wakati mgumu sana hasa yale ya karantini kwa sababu ya kuzuia mambukizi zaidi, pia suala hata la kufunga maeneo ya ibada,waamini kubaki hai katika matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi na kudumisha upendo wa Mungu ambao ndiyo mkubwa zaidi ya yote na kwamba virusi vya corona havitakuwa na neno la mwisho

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Madhara ya janga hili yaliyojitokeza litakumbukwa daima katika akili zetu na historia, na athari kubwa kwa pande zote na katika maeneo tofauti na ambalo lipelekee uongofu wa kila mmoja. Kwa maneno ya Papa Francis  katika sala ya tarehe 27 Machi katika Uwanja wa  Mtakatifu Petro, ndiyo wanaanza nayo maaskofu wa Congo katika ujumbe uliochapishwa baada ya mkutano wao mwishoni mwa Mei uliofanyika huko Brazzaville. Katika ujumbe wao wamesisitiza kuwa matukio ambayo yameleta wakati mgumu sana hasa yale ya karantini kwa sababu ya kuzuia mambukizi zaidi, pia suala hata la kufunga maeneo ya ibada, waamini kubaki hai katika matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi na kudumisha upendo wa Mungu ambao ndiyo mkubwa zaidi ya yote na kwamba virusi vya corona havitakuwa na neno la mwisho

Baraza la Maaskofu wanatambua aidha jitihada za serikali mbele ya kukabiliana na janga na hatua zilizochukuliwa kwa maana hiyo wanaomba waendelee katika mwelekeo huo na kuwa msaada kwa watu hasa walio katika mazingira magumu zaidi. Vile vile maaskofu wanapongeza sana mashirika na vyama ambavyo hadi sasa vinaendelea kwa jitihada zake kutoa msaada. Katika ujumbe wao pia wanaomba kufunguliwa kwa majengo ya ibada  na zaidi wanabinisha kwamba ni katika kurahisisha uhamasishaji juu ya covid-19 na kuwaalika kwa nguvu zote jumuiya nzima ya Congo kuheshimu hatua zilizochukuliwa na mamlaka katika kusimamisha maambukizi zaidi ya virusi.

Maaskofu katika ujumbe wao wanashuru  Majukwaa yote ya kupambana na virusi vya corona ya Baraza la Maaskofu na  kuyashauri yaendeleea kuonesha, licha ya vizingiti vya vifaa na zana, ule uso wa Kanisa mahalia katika jamii. Mtazamo wao pia umewaelekea hata Tume ya kusaidia mshikamano wa kitaifa dhidi ya virusi vya corona wakiwemo wawakilishi wa madhehebu mbali mbali ya dini ili waanzishe mambo mengine mapya ya dhati kama yaliyofanyika  ya kidini tarehe 14 Mei katika Jumba Kuu la Mkutano. Hatimaye wanatoa baraka yao kutoka kwa Mungu kwa ajili ya Congo na watu wake wote kwa namna ya pekee kwa vokosi vya ulinzi na usalama kitafia, walimu, wahudumu wa afya na viongozi wote wa nchi ili muktadha wa ustawi wa wote uweze kuangazia utu. Na wanahitimisha kwa kuwahakikishia sala zao kwa wagonjwa kwa namna ya pekee waliokumbwa na virusi, na kuwakabidhi katika huruma ya Mungu roho za marehemu waliofariki katika kipindi hiki cha janga.

16 June 2020, 15:26