Tafuta

Vatican News
Maaskofu wa Antille wakati wa Mkutano wao na Papa Francisko Maaskofu wa Antille wakati wa Mkutano wao na Papa Francisko   (Vatican Media)

Carribbien:Maaskofu wa Antille:siyo wakati wa kutafunga bandeji ni kutafuba njia bunifu!

Mara baada ya Mkutano wa maaskofu wa Antille wameandika taarifa yao kwamba wanao utambuzi wa kina hasa wa athari za kushangaza za majanga ambayo watu wao wamekuwa wakikumbana nazo katika eneo hilo la Antille.Siyo wakati wa kutafuta bandeji na kufunga vidonda bali kuungana ili kufanikisha wakati ujao.Siyo wakati wa kutembea kila mmoja na kuomba wafadhili kwa maana wafadhili wakuu wamekumbwa na janga la covid-19.Jibu la changamoto zinahitaji watu wote.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baraza la Maaskofu wa Antille wameaandika ujumbe wao walioupatia jina “Ujumbe wa Matumaini”, uliotolewa hivi karibuni mara baada ya Mkutano wao mkuu wa 64 uliofanyika kwa njia ya mtandao katika jukwaa la Zoom kutokana na dharura ya janga la virusi vya corona. Ni katika muktadha wa dharura hiyo ya Afya ambapo mkutano huu umechukua fursa ya ufunguzi wa ujumbe ambao unawaalika waamini wote kutafakari juu ya changamoto ambazo watu wa Kisiwa cha Caribbien wamelazimika kukabiliana nazo. Kupoteza nafasi za kazi, hasa baada ya kuanguka kwa sekta ya utalii, sheria za karantini za kukaa katika makazi ili kuzuia na usambaaji zaidi wa virusi vya corona na kufungwa kwa makanisa ambapo katika hofu ya kuungana pamoja kati ya waamini labda ingeweza kuchangia hatari zaidi ya maambukizi.

Miaka mingi visiwa hivi vimekuwa na changamoto ya dhoruba kali

Maaskofu wa Antille wanaandika wakiwa na utambuzi wa kina hasa wa athari za kushangaza za majanga ambayo watu wao wamekuwa wakikumbana nazo katika eneo hilo la Antille. Walio wengi wao kwa hisia na utupu wa kiroho, wameonesha umaskini wao, udhaifu wao na kuathirika kwao. Kwa miaka mingi wamekumbwa na kukuabiliana na majanga mengi. Vipindi vya dhoruba ni mwanzo wa mzunguko wa wasiwasi, majanga na ujasiri pia. Katika kujibu changamoto hizi inahitaji watu wote wa visiwa vya Carribien ili kuwa na tathimini halisi ya nini kilichotokea na kusaidiana na kila mmoja aweze kushiriki katika ujenzi mbunifu wa miundo na uhusiano wa kijamii.

Ni lazima kutunza kwa uhakika imani, matumaini na upendo hata katika kipindi hiki cha janga katika kanda yao na katika ulimwengu mzima ili usiharibiwe na zaidi kuweza kutoa fursa ya kipindi cha neema huku wakifikiria na kubuni njia mpya za kushiriki na kuishi katika Kanisa la leo hii wanabainisha maaskofu. Hata hivyo pia wanasema kuwa watu hao wako  tayari na ni mfano wa mashuhuda, kati ya wanandoa, familia na jumuiya katika mtindo huo mpya wa kuwa Kanisa. Maaskofu katika ujumbe wao wanatoa wito wa nguvu kwa viongozi wote wa kisiasa mahalia, ili waweze kweli kushirikiana wakiwa wameungana bila kuangukia katika vishawishi vya kwenda mbele kila mmoja na njia yake  huku akiomba msaada kutoka nje, kwa sababu wanasisitiza, hata wafadhili wakuu wamekumbwa sana na janga la virusi vya corona au covid-19.

Siyo kipindi cha kutafuta bandeji ya kufunga vidonda bali umoja wa kubuni njia

Maaskofu wa Antille aidha wanaandika kwamba "siyo wakati wa kutafuta bandeji ya kufunga vidonda vyetu tu", badala yake maaskofu wanasema "umefika wakati sasa wa kutafuta kwa kina ndani ya dhamiri zetu ili kufanikisha umoja huo ambao unawawezesha kushinda changamoto kubwa kwa pamoja, na hii ni kweli hasa katika muktadha wa usalama wa vyakula".  Maaskofu wanasisitiza kuwa tunapaswa na lazima kujitegemea katika sekta hiyo" , wakisisitiza na kuonesha msaada wao kwa juhudi hizo ambazo wamelenga kuzifanya katika kusahihisha ukosefu wa haki kulingana na mifumo wa ulimwengu.

Vipawa mbele vinne vya kichungaji:kanisa la nyumbani,ajira watoto/vijana na mazingira

Baraza la Maaskofu wa Antille (Aec) limetoa taarifa kuhusu vipawa mbele vinne vya kichungaji ambavyo vimethibitishwa wakati wa mkutano wao kuwa ni Kanisa la nyumbani, ajira (hasa wale waliopoteza kazi kwa sababu ya janga), watoto na vijana wakubwa, na ulinzi wa mazingira. "Leo hii kwa hakika ni kuendeleza kile ambacho kimeandikwa kwenye Wosia wa Querida Amazonia wa Papa Francisko baada ya Sinodi ya kuhusu Amazonia" wanaandika maaskofu. "Uchaguzi wa dhati kwa ajili ya maskini na waliosahaulika unatusukuma kuwakomboa na majanga yao na kulinda haki zao kwa kutoa pendekezo kwao ili kuwa na urafiki na Bwana na kuwahamasisha  zaidi huku wakipatiwa hadhi yao" (Querida Amazzona 63). Wakati huo huo katika fursa ya mwaka wa Tano tangu kutangazwa kwa Wosia wa Papa Francisko wa 'Laudato si' kuhusu Utunzaji bora wa Mazingira nyumba yetu ya pamoja, Maaskofu wa Antille wamethibitisha kuwa “tunaoutambui kuwa Mungu atahukumu kulingana na uongozi wa kimaadili na kiroho kwa mujibu wa utunzaji wa walio wadhaifu na walioathirika, kwa maana ya uwajibikaji mbele ya kazi ya uumbaji na kwa ajili ya umoja wetu madhubuti wakati wa shida”.

Kwa maombezi ya Bikira Maria Kanisa liwe tangazo la matumaini

Kwa kuhitimisha, taarifa yao, maaskofu wanapongeza ulimwengu wa mitandao ya kijamii ambayo wakati wa janga, imekuwa zana na ufunguo msingi wa kusambaza ujumbe wa matumaini. Mitandao ya kijamii kiukweli imesaidia familia, jumuiya, makampuni na marafiki kubakia na uhusiano japokuwa usio wa moja kwa moja lakini katika kujenga jumuiya wakati huu wa dharura ya kiafya wanabainisha. Ni matumaini ya maaskofu kwamba mazingira ya kidijitali yataendelea kutumika katika ujenzi wa ushirikiano wa pamoja na wa muungano, huku yakibaki na lengo moja tu a kutafuta namna ya kuunganisha wale ambao wanabaki nje. "Sasa ni kipindi cha majaribu, lakini hakitakiwi kukata tamaa. Mungu ni wakati wetu endelevu na "tumkabidhi Bikira Maria ili kwa njia ya maombezi yake Kanisa liweze kuwa tangazo la matumaini daima".

04 June 2020, 14:23