Yesu anajionesha kwa kutuvutia na anatukaribia katika uelewa wa ahadi ya Ufalme wa Mungu.Anawatuma wafuasi wake kwenda ulimwenguni kote kutangaza Injili yake kwa kila kiumbe. Yesu anajionesha kwa kutuvutia na anatukaribia katika uelewa wa ahadi ya Ufalme wa Mungu.Anawatuma wafuasi wake kwenda ulimwenguni kote kutangaza Injili yake kwa kila kiumbe. 

AUSTRALIA-PMS:Tangazo la furaha ya Injili ni utume wa Kanisa katika ulimwengu!

Ujumbe wa Papa Francisko ni ujumbe wa kutia moyo sana kwa sababu unaalika kupokea na kukaribisha kwa furaha ya Injili.Tangazo la wokovu na zawadi ya imani vinaleta zawadi ya Roho Mtakatifu ambayo inajumuisha undani wa zawadi ya imani na ambayo ni tunda la kuvutia.Ni tafakari ya Padre Brian Lucas,Mkurugenzi wa Utume wa Kitaifa wa Shirika la Kipapa la matendo ya Kimisionari(PMS)nchini Australia,kuhusu ujumbe wa Papa Francisko wa tarehe 21 Mei 2020 kwa shirika hili.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Padre Brian Lucas, Mkurugenzi wa Utume wa Kitaifa wa Matendo ya Kipapa ya Kimisionari nchini Australia, ametafakari ujumbe wa Papa Francisko alioutuma  tarehe 21 Mei 2020 katika Siku Kuu ya Kupaa kwa Bwana kwa Shirika la Kipapa la Utume wa Kimisionari. Kwa mjibu wa Shirika la Habari za Kimsionari Fides Padre Lucas anamesema “Ujumbe wa Papa Francisko ni ujumbe wa kutia moyo sana  kwa sababu unatualika kupokea na kukaribisha kwa furaha ya Injili. Tangazo lake la wokovu na zawadi ya imani vinatuletea zawadi ya Roho Mtakatifu ambayo inajumuisha undani wa zawadi ya imani na ambayo ni tunda la kuvutia. Yesu anajionesha kwa kutuvutia na anatukaribia katika uelewa wa ahadi ya Ufalme wa Mungu”.

Padre Lucas akiendelea kuutafakari ujumbe wa Papa amesema “kati ya mambo ambayo yamenigusa sana ni  lile linalohusu namna  ambayo Injili inashirikisha kwa mtazamo wa uzuri. Sisi hatufanyi propaganda, zaidi ya kuelekeza waamini kutazama Fumbo la Kristo na kuwa na ulewa wa ahadi ya Ufalme wa Mungu, kwa njia ya uzuri wa ujumbe huo na kufikia kuwa na uhusiano ambao tunautengeneza, na ambao unajitokeza moja kwa moja kupitia sisi wenyewe tunaposhirikishana imani yetu”.

Katika ujumbe wa Papa unavyoweza kusaidia upyaisho wa utume wa Kimisionari huko Australia, Padre Lucas amethibitisha “mimi ninafikiri kwamba katika mkutadha wa jamii ya Australia, changamoto zinazotusubiri zinawakilishwa na ukiritimba na kuwatwisha mizigo waamini ambapo Papa Francisko anafafanua bayana kwani anaposema kuwa “tunapaswa kuzuia mipango ya mafunzo ambayo yanaleta madhara makubwa na watu hawana haja nayo, zaidi ya kuwapa uwezekano wa kushirikisha imani yao binafsi na kuwa na msimamo wa uhusiano na watu wanaowazunguka”.

Kuhusiana na  lengo la Shirika la Kipapa la Kimisionari (PMS ) katika Kanisa kwa ngazi ya ulimwengu, Padre Lucas  amesema kuwa mwelekeo ambao lazima tuendeleze ni kwamba “tunaweza kujenga Ufalme wa Mungu kwa pamoja katika  kueneza tangazo la Injili kupitia uwezo wa kuwasiliana na kuanzisha uhusiano wa kibinafsi na waamini; kupeleka  ujumbe wake  kwa watu tunaokutana nao. Utume  siyo kitu cha kisasa au cha hali ya  juu, lakini pia ni ushiriki wa kila mmoja wetu katika maisha ya Kanisa ulimwenguni”.

17 June 2020, 13:01