Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki Yerusalem Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki Yerusalem 

Yerusalemu-Ask.Mkuu Pizzaballa:wakati ujao utahitaji haki,mapatano na upendo!

Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki wa Yerusalemu amesema kuwa wakati endelevu unahitaji haki kuu,maridhiano na upendo.Amesema hayo tarehe 18 Juni wakati wa kuadhimisha Misa ya kubariki mafuta ya Crisma ambayo iliahirishwa wakati wa Pasaka kutokana na dharura ya virusi vya Corona.Tuchote kutoka katika Neno la Mungu nguvu na ujasiri wa ishara na maneno ya tumaini,yanayosimika mizizi kwa Mungu wa Agano.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki wa Yerusalemu, Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, Alhamisi tarehe 18 Juni 2020 ameadhimisha misa Takatatifu ya kubariki Mafuta iliyokuwa imeahirishwa wakati wa Pasaka kutokana na dharura ya virusi vya Corona au covid-19. Katika kusisitiza amesema wakati endelevu unahitaji haki kuu, mapatano na upendo.  Katika misa iliyoadhimishwa kwenye Kanisa Kuu la Getsemani Askofu Mkuu amesema  “Siwezi (...) kufikiria  sherehe yetu ya Misa ya leo ya Crisma kama iliahirishwa katika hali iliyokuwapo (...) kwa kipindi kigumu ambacho tumepitia kutokana na janga na matokeo yake, bali lazima pia kuona kama kwamba ni mwaliko wa kutufanya tufikirie upya wenyewe  kwa namna tofauti”.

Katika misa ambayo mafuta ubarikiwa na kutengwa kwa ajili ya wakatekumeni, mpako wa wagonjwa, kipaimara, mpako wa ubatizo na mpako wa daraja takatifu na ni wakati ambapo makuhani hurudia ahadi zilizowekwa siku ya daraja takatifu la upadre, Askofu Mkuu amewageukia kwa namna ya pekee makuhani huku akisisitiza kazi yao ya kwanza hasa ya kutangaza Neno la Mungu. Neno la Mungu hurekebisha maono ya kibinadamu ambayo yanaona kwa ufupi sana na  ambayo hujipanua katika mikakati nyembamba sana ya kisiasa na kijamii. Haya yanaonyeshwa kwa jamuiya zetu, zilizochoka na kukosa mwelekeo, ambazo zinahitaji kuwa na njia za kiinjili za imani na  muhimu  zenye usawa na kushirikishwa.  Kwa mujibu wa Askofu Mkuu ni lazima kuacha kukimbilia katika masoko ya tumaini la bei nafuu, badala yake lazima tuchote kutoka katika Neno la Mungu  nguvu na ujasiri wa ishara na maneno ya tumaini, yanayosimika mizizi yake kwa Mungu wa Agano ambaye (...) hapunguzi  kamwe ahadi yake ya kujenga tena juu ya vifusi vyetu.

Tunapaswa kumbuka pia kwamba maaskofu na mapadri lazima wajitambulishe kama Kristo hasa  kuachana na kila kitu kinachozuia uhusiano wa karibu sana  na Mungu Baba, kwa maana hiyo msimamizi wa kitume wa Upatriaki wa Yerusalemu amesema kwamba siku zijazo zinaweza kuleta umaskini na mateso ya zamani na mpya, lakini ambayo yatahitaji nyongeza ya haki, maridhiano na upendo, kwa hiyo itakuwa muhimu  kuwa zawadi kamilifu ya  binafsi katika maisha ya ulimwengu kwa  kuzingatia juhudi na kujitoa  kubeba mzigo wa kila mmoja, kwa furaha na uchungu, katika upweke wa huduma au kwa ushirikishano wa pamoja.

Katikati ya ulimwengu ambao unazungumza juu ya uhuru lakini unaibua aina mpya za utumwa, sisi sote tumeitwa kuwa huru amesisitiza Askofu Mkuu  Pizzaballa kwamba uhuru kwa ajili ya  Ufalme, uhuru dhidi ya mzigo wowote usiohitajika, wa kasumba na mila ambazo labda haziongei tena katika maisha kwa  sababu hazijui tena juu ya maisha, kwamba ni Wokovu ambao uko katika kila mkutano wa kweli na Kristo.

Hatimaye, Askofu Mkuu Pizzaballa ameomba kwa ajili ya Kanisa la kweli la unabii, la kikuhani kwa kina, la kweli  kisheria. Kanisa huru dhidi mantiki ya nguvu ya kibinadamu na kwa maana hiyo lenye uwezo wa kufariji, wa maono na ujasiri,  lenye uwezo wa kuzungumza katika moyo wa mwanadamu.  Kanisa lenye uwezo wa kuleta Mungu na kutoa maisha yake kwa ajili ya kuupenda ulimwengu na tena Kanisa la  kushuhudia ukuu wa Kristo juu ya ulimwengu, ukuu wa upendo, zawadi, uhuru na ufadhili.

19 June 2020, 15:57