Tafuta

Vatican News
Lazima kukomesha ajira za utotoni na kuhamasisha haki ya watoto wote ulimwenguni Lazima kukomesha ajira za utotoni na kuhamasisha haki ya watoto wote ulimwenguni 

ASIA#coronavirus-Janga na haki za watoto:maelfu ya watoto wasukumwa katika soko la kazi!

Athari za hatua ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Covid-19 hasa kukaa karantini katika nchi nyingi na zaidi bara la Asia,kufungwa kwa shule na kuongezeka kwa mfadhaiko katika familia haviwezi na wala haifai kubadilishwa kuwa unyonyaji,unyanyasaji na dhuluma dhidi ya watoto.Ni kwa mjibu wa Rais wa Baraza la Kikristo Barani Asia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Watoto wanayo haki ya kulindwa dhidi ya kila aina ya mtindo wa ubaguzi, unyanyaswaji na vurugu. Athari za hatua ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Covid-19 kwa kukaa karantini katika nchi mbali mbali za bara la Asia na kwingineko,kufungwa kwa shule na kuongezeka kwa mfadhaiko katika familia haviwezi na wala haifai kubadilishwa kuwa unyonyaji, unyanyasaji na dhuluma dhidi ya watoto. Kusaidia na kukuza hadhi na haki za watoto lazima iwe kipaumbele kwa serikali, mashirika ya asasi za kiraia, makanisa na jamii zote za kidini.

Watoto lazima wawe ndiyo kitovu cha majibu ya dharura ya kiafya, kiuchumi na kijamii. Haya yamethibitishwa na wanaharakati wa haki za watoto na viongozi wa Makanisa barani Asia walioshiriki katika mkutano siku chache zilizopita kwa njia ya mtandao uliofuatiliwa na Shirika la Habari za kimisionari Fides, ulioandaliwa na Baraza la Kikristo  Asia (CCA) kwa kuongozwa na mada  “Kusaidia hadhi na haki za watoto katikati ya mgogoro wa Covid-19”.

Bwana Mathews George Chunakara, Katibu Mkuu wa Baraza la Kikristo barani Asia(CCA),amesema“mahitaji ya watoto katikati ya janga la virusi hayaonekana. Athari za virusi vya corona zinaweza kuharibu kabisa ustawi wa vizazi vijavyo. Kwa maana hiyo inahitajika kudai haki zao, kuhakikisha ustawi na hadhi ya utoto. Ustawi wa maisha ni haki kwa watoto wote”.

Mamilioni ya watoto katika  bara la Asia wako hatari ya kusukumwa kwenye soko la kazi. Mgogoro uliosababishwa na Covid-19 unaweza kusababisha ongezeko la kwanza la ajira za utotoni baada ya miaka 20 ya maendeleo, kwa mujibu wa , Shirika la Kazi la Kimataifa ILO  na Shirika la kuhudumia Watoto UNICEF ​​wakati wa kutoa ripoti yao katika muktadha wa  “Siku ya Kupinga Ajira za Utotoni Ulimwenguni, iliyoadhimishwa tarehe 12 Juni na kwa matazamio ya  mwa 2021, kama Mwaka wa Kimataifa wa Kutokomeza Ajira za watoto uliotangazwa na Umoja wa Mataifa (UN).

Kwa kuzingatia jitihaza zilizofanyika, wamepungua kutoka watoto 2000 hadi leo, lakini hali ambayo inaweza kurudisha ongezeko zaidi , kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa na mashirika hayo mawili huku yakiripoti kuongezeka kwa hali ya watoto huko Asia, na uharibifu mkubwa wa afya na usalama. Kanda ya Asia Mashariki na Pasifiki inakaribisha asilimia  70% ya watu walioathiriwa na majanga ulimwenguni. Kwa kuongezea hatari zinazohusiana na janga  la corona idadi ya watu wamekumbwa na mabadiliko ya tabianchi, uhamishwaji kwenda katika  jiji, na ni matukio ambayo ni kuzidisha mazingira magumu zaidi ya yale ambayo tayari yapo. Lakini pamoja na hayo yote Watoto ndiyo waathiriwa wa kwanza.

17 June 2020, 10:08