Sala ya Pamoja katika kuenzi mwaka wa Tano wa Wosia wa Papa wa 'Laudato si' (16-24 Mei 2020) Sala ya Pamoja katika kuenzi mwaka wa Tano wa Wosia wa Papa wa 'Laudato si' (16-24 Mei 2020) 

INDONESIA#Wiki ya Laudato si’:Kard.Suharyo atoa wito wa kuwa na moyo wa ukarimu!

Katika 'Wiki ya Laudato si',kuanzia 16-25 Mei 2020,hata Kardinali Suharyo nchini Indonesia ametoa wito kwa Wakatoliki wote ili wawe na moyo wa ukarimu,wasiharibu na kupoteza vyakula hovyo wakati kuna maskini wengi na watu wenye njaa.Aidha anawatia moyo kulinda na kutunza ardhi ambayo ni nyumba yetu ya pamoja.

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Jumapili tarehe 17 Mei 2020, katika Misa yake Kardinali Ignatius Suharyo Hardjoatmodjo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Indonesia, katika ujumbe wake wa dakika saba uliotangazwa kwa maparokia yote ya Jimbo Kuu Katoliki la Jacarta, kwa njia ya video ametoa wito ili watu wawe  wakarimu kwa upande wa chakula.  Katika ujumbe wake amesema “tupokee mwaliko wa Papa Francisko wa kutafari na kujali kile chenye maana na kusikiliza wito kwetu wa kutunza na kulinda ardhi yumba yetu ya pamoja ili iweze kuwa mahali penye tarajio, amani kwa ajili yetu kama binadamu na kwa ajili ya kazi yote ya uumbaji.

Katika fursa ya mwaka wa tano tangu Papa Francisko atangaze Wosia wake wa Kitume wa ‘Laudato di’ na  katika ‘Wiki ya Laudato si’ ambayo imeanza tarehe 16-24 Mei 2020 kwa kuhamasishwa na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Watu, lengo lake ni kuwatia moyo, kuhamasisha matendo ya hakika kibinafsi na kijumuiya kwa ajili ya utunzaji wa nyumba yetu ya Pamoja. Kwa maana hiyo Kardinali amewaalika wakatoliki wote wawe na moyo mwema wa kutoharibu mambo ambayo yanaweza kuwa muhimu kwa wengine.

Ili kufafanua kinagaubaga kuhusu suala hili, Kardinali Suharyo, imesimulia hadithi moja kuhusu kasuku na ndege wengine walivyokuwa wanahisi wako salama kwa kukaa kwenye mti mkubwa. Na wakati,mti huo ulipoanza kuharibika kutokana na mshale uliokuwa na sumu ya mwindaji, ni kasuku peke yake aliyeamua kubaki kwenye mtu huo. Na mgeni mmoja alipomuuliza kwa nini amemua kubaki, kasuku alijibu kuwa alikuwa ameifanya hivyo kutokana na kwamba mti huo ulikuwa umesaidia familia yake. Basi mgeni, ambaye alikuwa na nguvu maalum,aliweza rudishia mti ule uhai, kiasi kwamba  ndege wengine pia waliweza kurudia mti ule.

Kwa kufafanua juu ya simulizi hiyo Kardinali amesema,“hadithi hii ni rahisi japokuwa ujumbe wake una nguvu. Kwa maana hiyo kwa wote tunaombwa kuwa na moyo wa ukarimu, kama ule wa kasuku. Tendo la kuwa na moyo mkarimu inawezekana kulinda, kutunza na kuwa na jitihada kwa ajili ya Ardhi  na ili paweze kuwa mahali pa maratajio kwa ajili ya uumbaji wote".

Tume ya Haki na Amani ya Jimbo Kuu hilo kupitia Padre Agustinus Heri Wibowo, Mwenyekiti wa Tume hiyo amewaalika maparoko wote kuanzisha uhamasishaji wa Wosia wa Papa na kuwatia moyo wanaparokia wote ili kufanya kazi kwa ajili ya Mazingira. Akizungumza na Kituo cha habari (UCA)cha  jimbo kuu hilo, amebainisha kuwa wakatoliki hawapaswi kuwa na uharibifu kuhusu chakula kwa kukitupa hovyo na hata kutupa nguo zao ambazo zinawakilisha matatizo makubwa ya kutumia hovyo. Kwa maana hiyo ameomba waamini waepuke uharibu wa  chakula kwa maana wapo maskini wengi na wenye njaa. Ameomba wapande miti na familia na kuwasaidia raia mahalia ambao sasa wanateseka, licha ya kuwapatia chakula watu ambao wanaishi barabarani.

19 May 2020, 12:49