Tafuta

Kwa mwezi mzima wa Mei hadi mwanzo wa mwezi Juni, Shirika la habari Katoliki nchini Uswiss ‘Cath-info’ litajikita kusimulia historia za mashujaa wa kipindi cha janga la covid-19 ambao hawajulikani. Kwa mwezi mzima wa Mei hadi mwanzo wa mwezi Juni, Shirika la habari Katoliki nchini Uswiss ‘Cath-info’ litajikita kusimulia historia za mashujaa wa kipindi cha janga la covid-19 ambao hawajulikani. 

USWISI#Coronavirus:Dominika ya vyombo vya habari:Kusimulia historia za mashujaa wa kila siku!

Kila mwaka katika mwezi Mei Shirika la habari katoliki nchini Uswisi chini ya Uongozi wa Baraza la Maaskofu nchini humo,uhamasisha Dominika kwa ajili ya vyombo vya habari.Mwaka huu tukio linaangukia katika janga la virusi vya corona hivyo Dominika tarehe 24 Mei maaskofu wanaomba waamini kutoa sadaka yao kwa njia ya mitandao ili kufadhili vyombo vya habari katoliki nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Shirika  la habari Katoliki la Uswisi huko Lausanne limeandaa kusherehekea Jumapili ya vyombo vya habari tarehe 24 Mei 2020 ambalo ni  tukio la kila mwaka, liliopitishwa na Kanisa mahalia yaani Baraza la Maaskofu nchini humo, kwa lengo la kufadhili vyombo vya habari Katoliki katika nchi hiyo. Ni katika jitihada za wanahabari katoliki nchini Uswisi kwa ajili ya kusimulia historia za mashujaa wa kila siku katika kipindi cha janga la virusi vya corona kwa mujibu wa taarifa yao.

Hata hivyo ni “kusimulia historia njema ambazo zinajenga na siyo za kuharibu na kuwezesha kusimulia ubinadamu ambao unasukana kama uzi  ili kuweza kuunganisha na wengine”. Huo ndiyo kiukweli ulikuwa mwaliko wa Papa Francisko aliotua katika Ujumbe wa Siku ya 54 ya Upashanaji Habari Duniani 2020 ukiongozwa na kauli mbiu: “ili uweze kusimulia na kufanya kumbukumbu:Maisha ni historia”kutoka katika kitabu cha Kutoka 10,2. Papa alisisitizia umuhimu wa thamani ya mwanadamu katika kusimulia historia tangu mwanzo hadi mwisho wa maisha yake. Alichagua mada ya kusimulia kwa sababu anaamini kuwa ili tusiweze kupotea, tunahitaji kupumua ukweli wa historia nzuri; historia zinazojenga, na siyo za kuharibu, historia zinazosaidia kuota mizizi na nguvu ya kwenda mbele kwa pamoja”.

Kwa maa hiyo hiyo njia hii inakuwa kwa mara nyingine tena mwaliko wa sasa katika kipindi cha janga la virusi vya corona,uliopendekezwa na Shirika la Habari Katoliki nchini Uswisi tarehe 24 Mei 2020 iwe Dominika ya Vyombo vya mawasiliano. Hii ni siku ambayo imewekwa na Kanisa Mahalia katika kukusanya fedha kwa ajili ya kufadhili njia za mawasiliano katoliki katika nchi hiyo, kupitia kauli mbiu ambayo inataka kueleza kuwa mawasiliano siyo ya kweli ikiwa hayachangii kusuka ule uhusiano ambao leo hii unahitajika kama ulivyoibuka katika wiki hizi za kufungwa karantini kutokana na janga. Ni hali ambayo imeongeza jukumu na uwajibikaji wa vyombo vya habari, hasa vile vya  kikristo ambavyo leo hii vinaitwa zaidi ya hapo awali kukabiliana na kupinga uwongo wa habari zinazodanganya kwa sababu za kisiasa au kiuchumi.

Kwa mwezi mzima wa Mei hadi mwanzo wa mwezi Juni, Shirika la habari Katoliki nchini Uswiss ‘Cath-info’ kwa maana hiyo linapendekeza historia za maisha ili kuweza kuwafanya waonekane hawa mashujaa wasiojulikana wa kila siku ambao hata Papa Francisko amewataja katika ujumbe wake na wamekuwa kwa dhati mstari wa mbele katika shida ya sasa. Historia hizi zitaambata na ushuhuda wa watu watatu muhimu katika ulimwengu wa habari nchini Uswisi. Hao ni Marc-Henri Jobin, mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Uandishi wa Habari na Vyombo vya Habari (CFJM) cha Uswisi-Ufaransa; Silvana Bassetti mhusika wa  habari za Kanisa Katoliki Geneva(Ecr) na Jean-Claude Boillat, mhusika mkuu wa Huduma za mawasiliano kichungaji (SCJP), na Marc-Henri Jobin, Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo na Uandishi ambaye atazungumzia juu ya maono yao ya vyombo vya habari kwenye huduma ya Jumuiya.

Kama ilivyo makusanyo mengine ya kila mwaka yaliyohamasishwa katika kipindi cha Kwaresima, hata kwa  Jumapili hiyo kwa ajili ya  vyombo vya habari haitawezekana kufanyika katika makanisa na kwa maana hiyo waamini wamealikwa kutoa sadaka zao kupitia mtandaoni. Fedha zitakazo patikana pia zitatumiwa kufadhili Tuzo la Vyombo vya Habari, toleo ambalo hutolewa kila mwaka na Baraza la Maaskofu la Uswisi (Ces),liitwalo “Tuzo la Habari Njema” ambalo upewa kila mkoa wa lugha ya Shirikisho na shughuli za Tume ya Vyombo vya Habari za Baraza hilo la maaskofu Uswisi (Ces).

07 May 2020, 13:54