2020.05 08 Baraza la Maaskofu nchini Uganda wametoa tani kumi za vyakula kwa kikundi cha Nguvu Kazi cha kitaifa kwa ajili ya kusaidia waathirika wa covid-19. 2020.05 08 Baraza la Maaskofu nchini Uganda wametoa tani kumi za vyakula kwa kikundi cha Nguvu Kazi cha kitaifa kwa ajili ya kusaidia waathirika wa covid-19. 

UGANDA#coronavirus:Maaskofu watoa tani 10 za chakula kwa mshikamano na Tataifa!

Maaskofu nchini Uganda wametoa mchango wao kwa kikundi maalum cha nguvu kazi kilichoundwa na Taifa kwa ajili ya kupambana na janga kubwa la covid-19.Msaada huo ni tani kumi za vyakula ili kuwagawia watu wenye shida na waishio katika mazingira magumu katika kipindi hiki kigumu cha janga la dunia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika harakati mbalimbali za kuingilia kati kutoa msaada wakati huu wa hatari inayokabili ulimwengu mzima, hata wa upande wa Kanisa mahalia, mchango mkubwa na muhimu umetolewa na Baraza la Maaskofu wa Uganda (Uec) kwa “Kikundi cha Nguvu Kazi Covid-19” kilichundwa na Serikali ya Nchi hiyo katika  harakati ya kupambana na Janga la virusi vya Corona. Kwa maana hiyo maaskofu wametoa mchango wake kwa kikundi hicho maalum kiasi kikubwa cha vyakula kwa ajili ya kuwagawia watu wenye shida sana na waliothirika.

Siku ya Jumanne tarehe 5 Mei, Rais wa Baraza la Maasofu Uganda (Uec), Askofu  Anthony Zziwa Aliwakabidhi tani kumi za chakula kwa chombo hicho kilichundwa kwa ajili ya majukumu ya kukusanya na kugawanya msaada kwa waathiriwa wa janga. Kwa mujibu wa Gazeti la “La Croix Afrique” linataarifu kuwa, kwa namna ya pekee msaada wa Kanisa Katoliki unajumuisha tani tano za unga wa mahindi na tani tano za maharage,vitu hivyo vyote vilipokelewa mjini Kampala na Waziri Mkuu Ruhukana Rugunda na ambaye ametoa shukrani kwa maaskofu kwa mshikamano wao.

Kwa mujibu wa Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Uganda Askofu Zziwa,aliyekuwa amesindikizwa kwa fursa hiyo na Monsinyo Baptist Kauta,Katibu Mkuu wa Baraza la MaaskofuUec, na Bwana Gervase Ndyanabo, Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya walei  amefafanua na kuhamasisha juu ya matatizo ambayo yametokana na virusi vya corona kati ya watu walio katika mazingira magumu, na kuwashauri kuwa na utambuzi mkuu na uwajibikaji wa kuheshimu sheria za usalama wa kiafya wa kuzuia maambukizi. Kadhalika amesema uwepo wa virusi vya corona au covid-19 katika Nchi ni wa kweli na kama ilivyo hatari ya kweli ya matokeo yake, hivyo amealika watu wasidharau hasa wale wanaodai kuwa Uganda hakuna virusi. Tarehe 4 Mei nchini Uganda rekodi zimeonesha kesi 97 za watu na watu 55 wamepona.

08 May 2020, 12:15