Tafuta

Vatican News
2020.05.05Namungongo katika  Madhabahu ya Wafiadini wa Uganda 2020.05.05Namungongo katika Madhabahu ya Wafiadini wa Uganda 

UGANDA#Coronavirus:hija ya kwa wafiadini Namugongo mwaka huu kuahirishwa!

Kufuatia na dharura ya janga la virusi vya corona au covid-19 ulimwenguni,hija ya kwenda kwa wafiadini huko Namugongo ifanyikayo kila mwaka tarehe 3 Juni imeahirishwa.Ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Uganda aliyotoa hivi karibuni.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa mujibu ta taarifa kutoka kwa Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Uganda Askofu Anthony Zziw alizotoa hivi karibuni kupitia vyombo vya habari mahalia, hija ya kila mwaka ya kwenda katika madhabahu ya wafia dini wa Namugongo  ambayo kila mwaka uanzia tarehe 29 Mei hadi Juni 3 mwaka huu haitafanyika kutokana na dharura ya kiafya ya janga la virusi vya corona au covid-19.

Kuahirishwa kwa tukio hili ambalo ni  moja ya maadhimisho muhimu zaidi ya kidini katika bara la Afrika, limekuja mara baada ya maagizo mpya ya Serikali ya Kampala Uganda ambayo imekataza mikusanyiko ili kuzui kuenea kwa janga la ugonjwa  wa virusi vya corona hata kama maambuziki katika nchi hiyo siyo makubwa mno kwani ikadiriwa kuwa kama watu 83 kuambukizwa na hakuna kifo hata kimoja.

Jimbo la Masaka ambalo mwaka huu lilikuwa limepewa jukumu la kuandaa tukio, linathibitisha kuwa liko tayari kuandaa hija hiyo mara watakapokuwa wamepanga tarehe nyingine tena mara baada ya kuisha kwa janga la virusi vya corona na kamati ya kuratibu  maandalizi, bado haijafutwa, kwa mujibu wa taarifa za msemaji mkuu wa jimbo, Padre Ronald Mayanja kupitia  gazeti la kila siku la Uganda “The Monitor”. Ili kuweza kukamilisha toleo la tukio hili, jimbo la Masaka lilikuwa limefanikiwa kukusanya shilingi za Uganda milioni  300(UGsh) zenye thamani ya Euro karibia 95,000.

Siku ya wafiadini wa Uganda mwaka huu imefikisha miaka 124, ambapo kila mwaka tarehe 3 Juni Mama Kanisa uwakumbuka wafia dini hao wa kutetea imani yao katika Kristo. Tukio hili kwa kawaida uwakusanya maelfu na maelfu wa mahujaji kutoka Uganda nzima lakini hata katika mataifa mengine ya Afrika na Ulaya ambao hukusanyika ili kufanya kumbu kumbu ya wakristo 45 ikiwa wakatoliki 22 na waanglikana 23 waliuwawa kwa chuki ya imani yao katika mwisho wa karne ya XIX kwa maagizo ya Mfalme wa Buganda wa wakati huo, Kabaka Mwanga II.

Kati ya wafiadini wa Uganda anayejulikana sana ni Karoli Lwanga. Yeye na wenzake 21 waliuwawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 17 Januari 1887. Wafiadni 22 wakatoliki walitangazwa kuwa wenye heri na Papa Benedikto  XV kunako mwaka 1920 na kutangzwa watakatifu na Papa Paulo VI kunako tarehe 8 Oktoba 1964 katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Wakati wa ziara yake ya kitume barani Afrika 1969 Papa Paulo VI, madhabahu ya Namungogo aliita kuwa kubwa kwa ajili yao na kwamba ni  eneo la wafidini

Kunako tarehe 7 Februari 1993 Mtakatifu Yohane Pulo II aliadhimisha misa katika madhabahu hiyo wakati wa ziara yake ya kitume huko Benin, Uganda na Karthoum-Sudan. Hata kwa upande wa Papa Francisko, alitoa heshima kwa wafiadini wa Uganda katika Madhabau hiyo ya Namugongo wakati wa fursa yake ya ziara ya Kitume barani Afrika mwezi Novemba 2015. Katika fursa hiyo Papa Francisko alikuwa amesititiza kuwa urithi wa Wafidini wa Uganda, ni uwakilishi wa maisha ambayo yanatokana na nguvu ya Roho Mtakatifu, maisha ambayo yanashuhudia hata sasa ule uwezo wa kubadilishwa na Injili ya Yesu Kristo Mfufuka.

Urithi huu uwezi kuubinafsisha alisema Papa Francisko, na kumbukumbu ya hali au kwa kuitunza kwenye makumbusho kana kwamba ni vito vya thamani. “Tunamuheshimu kwa dhati na tunawaheshimu Watakatifu wote, wakati tunatoa ushuhuda wao kwa Kristo katika majumbani mwetu na kwa majirani zetu, kazini na katika vyama vya kiraia, hata ikiwa tunabaki majumbani mwetu au tunakwenda mbali zaidi katika kila kona ya ulimwengu”.

05 May 2020, 11:03