Tafuta

Vatican News
Usambazwaji wa misaada wakati wa kipindi cha dharura ya covid-19 katika mji wa Dakar nchini Senegal Usambazwaji wa misaada wakati wa kipindi cha dharura ya covid-19 katika mji wa Dakar nchini Senegal 

SENEGAL#coronavirus:uamuzi wa Mfuko wa Caritas kwa waathirika wa kiuchumi!

Caritas nchini Senegal imeamua kuwa mfuko wa fedha uliokuwa umezinduliwa na kukusanya fedha kwa lengo la kusaidia dharura za mafuriko,kipindi cha baridi na dharura nyingine za nchi kunako mwezi Machi mwaka huu kwa sasa wanauelekeza mfuko huo kwa watu waliopata pigo la kiafya kijamii na kiuchumi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mfuko Katoliki  wa dharura wa Caritas uliokuwa umezinduliwa mwezi Machi iliyopita kwa ajili ya kusaidia watu wa Senegal waliokuwa wamepata pigo la dharura iliyosababishwa na mvua, kipindi cha baridi au mafuriko na kuongeza uwezo wa kukabiliana na hali halisi  iliyokuwapo wakati ule, kwa sasa, wameamua mfuko huo kuuelekeza katika mgogoro wa afya kijamii wa sasa.

Kutokana na dharura ya sasa ya kiafya katika janga la virusi vya corona, Mfuko Katoliki wa dharura kwa upande wa Caritas nchini Senegal utawasaidia watu wenye shida sana na zaidi wazee ambao wanajikuta katika hali ya matatizo makubwa kutokana na janga la Covid-19. Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na vyombo vya habari mahalia, pia wamesitisha ukusanyaji wa fedha ambao ulikuwa uwaunganishe majimbo yote ya Nchi kwa ajili ya kusaidia watu wenye shida zaidi.

Lengo la Caritas ni lile la kuwasaidia hasa wale ambao hawana  zana na mahitaji msingi kwa sababu ya mgogoro wa kiuchumi- kijamii uliosababishwa na dharura ya kiafya. Mfuko wa fedha ulikuwa umekusanya hadi sasa zaidi ya milioni 10 za kifranki na sasa ambazo zitatumika kwa ajili ya matumizi ya familia zilizo na shida sana. Aidha katika taarifa hiyo inabanisha kuwa miundo ya majengo ya kiafya ya Kanisa Katoliki mahali ambamo wamelazwa wagonjwa wa virusi vya corona watapokea misaada mingine na wakati huo huo kandoni mwa misaada kwa ajili ya kusaidia dhaura ya vyakula kwa ajili ya miezi ijayo.

Hatimaye wanashukuru sana kwa wale ambao hadi sasa wameweza kuonesha mshikamano wao na hivyo Caritas nchini Senegal, inawaalika watu wote  kuendelea kujikita kwa dhati ili kuwasaidia maskini zaidi katika kipindi hiki kigumu na kuendelea kusaidia Mfuko Katoliki wa dharura ili upate kuendelea kwa kina kisaidia walio athirika zaidi.

06 May 2020, 12:48