Tafuta

Vatican News
Maaskofu chini Polond wameshauri waamini wawe makini na kuheshimu hatua zote za serikali katika kuzuia maambukizi ya virusi wakati wa kushiriki misa na huduma zote za dini. Maaskofu chini Polond wameshauri waamini wawe makini na kuheshimu hatua zote za serikali katika kuzuia maambukizi ya virusi wakati wa kushiriki misa na huduma zote za dini.  (ANSA)

POLAND#coronavirus:waamini kuwa waangalifu wakati wa kushiriki ibada!

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Baraza la Kudumu la Maaskofu katoliki nchini Poland wamewaalika waamini wakati wa ushiriki wa Misa na huduma zote za kidini kuheshimu na kuwa waangalifu wa miongozo ya kiafya iliyotolewa kwa wakati huu wa janga la virusi vya corona.Wanawakumbusha waamini wasikose kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II kunako tarehe 18 Mei.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kwa kila iwezekanavyo tunawaalika ushiriki wa Misa na huduma za kidini, ndiyo uthibitisho kutoka Baraza la Kudumu la Maaskofu wa Polond mara baada ya Mkutano wao mwanzo mwa mwezi Mei huko Jasna Góra,na kutangazwa katika tovuti yao ya kiaskofu, na wakati huo wanawakumbusha kuwa hatua zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya janga la Covid-19  bado na lazima yaendelee kuwekwa maanani wakati wa kufanya liturujia zote.

Maaskofu pia wanakumbusha kuwa katika wakati huu wa janga kwa waamini bado hawalazimishwi kuhudhuria misa na wakati huo huo wanashukuru vyombo vya habari na vya kiparokia kwa kutangaza moja kwa moja liturujia kwenye runinga, redio na mitandao yote ya kijamii, pampja na hayo yote wanasema hii haipaswi kudhoofisha mapenzi yao mema ya kuweza kupokea sakramenti katika makanisa yao moja kwa moja.

Katika uthibitisho wao, Maaskofu hao wanasisitiza juu ya umuhimu wa hatua za kiafya za kuzuia kutokana na kuenea kwa janga la virusi vya corona au covid-19, na kwamba ingawa kwa wengi bado ni ngumu, lakini mbele ya uamuzi wa serikali katika kuondoa hatua hizi za vizuri kabla ya ugonjwa kuishi kabisa, wanaamini kuwa ni muhimu  kuwa na umakini zaidi katika vigezo madhubuti sawa vya vizuizikuhusu idadi inayokubalika ya waamini katika makanisa na kama ilivyo kwisha tokea katika maeneo mengine.

Bila ubaguzi wa masharti ya mamlaka zote za afya na serikali, maaskofu kwa maana hiyo wanawaalika waamini, inapowezekana, kushiriki katika huduma za kidini kwa mwezi Mei. Wanaweza kuwa na fursa nzuri ya kichungaji kwa makanisa na kurudi kwenye maisha ya sakramenti kwa wale wanaopenda, wamewashauri.

Na hatimaye maaskofu wanawatia moyo waamini ili kuwasaidia watu walio katika mazingira magumu katika kipindi hiki na wanawashukuru wote ambao wanaendelea kujitoa kuwasaidia wagonjwa, watu walio katika karantini na wazee. Vile vile wametoa mwaliko wa nguvu kwa Jumuiya katoliki wasisahau kilele cha miaka 100 tangu alipozaliwa Mtakatifu Yohane  Paulo II, katika nchi hiyo, tarehe 18 Mei ili kuweza kuiadhimisha kwa kukumbuka mafundisho yake, ushuhuda wa maisha yake, huduma yake kuanzisha mambo ya kihisani kwa ajili ya wenye kuhitaji.

04 May 2020, 11:09