Kipindi cha janga la virusi vya corona nchini Brazil limeathiri watu wengi na zaidi watu Asilia wa Amazonia. Kipindi cha janga la virusi vya corona nchini Brazil limeathiri watu wengi na zaidi watu Asilia wa Amazonia. 

NORWAY#coronavirus:mshikamano wa Makanisa ya Kiluteri&Katoliki kwa Amazonia!

Makanisa ya nchini Norway ya Kiluteri na katoliki wamekuwa na mshikamano kwa watu wa asilia wa huko Amazonia kufuatia na dharura ya covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Makanisa nchini Norway yameelezea wasiwasi wao mkubwa kwa watu wa Asilia wa huko  Amazonia  nchni Brazail ambao wamekuwa katika mazingira magumu, hasa baada ya maambukizi ya virusi vya corona. Katika barua yao waliyoituma katika ubalozi nchini Brazil, Makanisa ya Kiluteri pamoja ya ya Wakatoliki wameeleza mshikamano wao kwa nchi hiyo na kwamba wanahisi kuwa na huu wasiwasi hivyo ni lazima kudhibiti virusi vya covid-19 huko Amazonia ambavyo vimepigisha magoti katika maeneo kutokana na kutokuwa na miundo mbinu ya viruo vya afya.Huo ni ujumbe uliotiwa sahihi na Rais wa Kanisa la Kiluteri wa Norway na Askofu Olav Fykse Tveit, na Askofu wa Jimbo la Oslo Markus Bernt Eidsvig.

Tarehe 4 Mei 2020 Baraza la Kiekumene la Makanisa, Baraza la Maaskofu nchini Brazil katika tamko lao wanabainisha kuwa vipmo vilivyochukulia hadi sasa haivonesha takwimu halisi ya maambukizi ya virusi na ambapo watu wengine wenye dalili za ugonjwa huo wanakufa katika nyumba zao bila kuwa na huduma yoyote ya kimatibabu.

Watu asilia na Jumuiya nyingine za Amazonia, wako hatari kubwa na kama ilivyo kwa watu wote wanaoishi mijini lakini pembeni, mahali ambao wanakosa kila hai ya huduma ya usafi msingi, malazi yenye hadhi, chakula na ajira.Hata hivyo Meya wa jiji kubwa nchini Brazili, São Paulo la Sao Paulo amesema kuwa mfumo wa afya unaweza kuporomoka huku pakikwa na ongezeko la mahitaji ya vitanda vya dharura ili kuwahudumia wagonjwa wa corona. Bwana  Bruno Covas amesema hospitali za umma za jiji hilo zinaweza kujaa katika kipindi cha wiki mbili zijazo. Sao Paulo ni moja kati ya miji iliyoathirika zaidi nchini Brazil kukiwa na watu 3,000 waliopoteza maisha mpaka sasa kutokana na virusi vya corona.

Siku ya Jumamosi tarehe 16 Mei 2020, nchini Brazil ilizidi nchi ya Uhispania na Italia na kuwa taifa la nne lenye idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya corona. Hata hivyo Wizara ya afya imeripoti maambukizi mapya 7,938 katika kipindi cha saa 24, jumla ya watu walioambukizwa ikifikia 241,000. Marekani, Urusi na Uingereza ndizo zilizo na idadi kubwa zaidi ya watu waliopatwa na maambukizi. Idadi ya waliopoteza maisha katika nchi hiyo ya Amerika ya Kusini katika kipindi cha saa 24 ni watu 485, ikiwa na jumla ya vifo 16,118, takwimu zinazolifanya taifa hilo kushika nafasi ya tano kati ya nchi zenye idadi kubwa ya vifo.

18 May 2020, 16:32