Kipindi cha janga la virusi vya corona,caritas nchini Nigeria imeanza kutoa msaada kwa familia zenye matatizo katika pembezoni mwa mji wa Lagos Kipindi cha janga la virusi vya corona,caritas nchini Nigeria imeanza kutoa msaada kwa familia zenye matatizo katika pembezoni mwa mji wa Lagos 

NIGERIA#coronavirus:caritas kugawa vyakula kwa maskini wasioweza kutoka ndani ya nyumba zao!

Ikiwa uongozi wa kiwango cha chini ukichanganya na tabia inayoonekana wazi kuwa isiyozuilika ya kuiba na kufuja pesa za Nigeria,unajikuta katika nchi ambayo hospitali zao hupunguzwa kuwa vyumba vya ushauri tu.Ni usemi wa Kardinali Okogie wa Jimbo Kuu la Lagos, mahali ambapo Caritas nchini humo iko mstari wa mbele kusaidia vyakula kwa watu maskini katika janga hili la covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Nchini Nigeria kama ilivyo katika nchi nyingine zilizo maskini, waathirika wengi ni maskini  zaidi  walio pembezoni mwa miji katika janga hili la virusi vya corona kufuatia na hatua za kuzuia maambukizi zilizo wekwa na mamlaka, kwamba watu wabaki ndani ya majumba yao, kama ilivyo jitokeza nchini Nigeria. Kwa  kwa maana hiyo  Kanisa  nchini humo linaendelea kuongeza jitihada zake katika nchi ili kusaidia hali halisi ngumu ya watu wanaokabiliwa na hali ngumu sana kwa kwa amna ya pekee kwa wale wanaoishi pembezoni mwa mji wa Abuja na Lagos, na ambao Caritas kwa sasa  inaendelea kutoa msaada wa vyakula kwa mamia ya familia wenye shida karibu na wilaya ya Durumi na wanaozungukia maeneo hayo kwa sababu ya kuzuia kutoka nje. Msaada huo umetangazwa na Katibu Mkuu wa Caritas Padre  Zacharia Samjumi.

Wafadhiliwa wa zawadi ya Caritas ni wafanyakazi hasa ambao wanaishi kwa kawaida na shughuli ya siku na ambao kwa kipindi hiki hawana kipato yaani ni zero kwa sababu ya vizuizi hivi n hawawezi kufanya lolote. Mpango wa kugawa vifaa vya vyakula mwanzoni walitazamia kuwasaidia familia 200, lakini baadaye ikaongezeka kutoka 500 hadi kufikia 1000. Padre Samjumi  kwa maana hiyo ametoa wito kwa wanaigeria wote wenye hali nzuri kimaisha ili waweze kuchangia mpango huo wa kutoa huduma kwa Caritas hata kwa mashirika mengine yenye mapenzi mema. Kwa mujibu wa Padre Sanjumi amesema “ tunategemea mashirika aminifu, wanaweza kweli kuwafanya maskini zaidi  wa kijamii wafikiwe msaada kutokana na kuzuiwa nyumbani na wanakumbana na hali ngumu majumbani mwao.

Na kwa upande wake Askofu Mkuu Alfred Adewale Martins, wa Jimbo Kuu  Lagos, mji ambao kwa namna ya pekee umepata pigo la janga la virusi, ametoa wito wake wakati wa fursa ya Misa ya Jumapili ya Huruma katika Kanisa Kuu la Msalaba Mtakatifu, akiomba kuwa na upendo wa jirani na hisani kuu. Mbele ya waamini wachache waliokuwa katika misa hiyo iliyotangazwa moja kwa moja na televisheni alifurahia ushiriki wa wakristo kwa wito wake wa kuwa na mshikamano kwa ajili ya watu walikumbwa na janga. “Muwe na neno la huruma kwa wote, msali kwa ajili ya jirani zenu na kuwatendea mema, kwa kuwaonyesha upendo wa Mungu ambaye ni mwingi. Aidha alisisitiza,“wakati wa kipindi chote cha vizuizi, tumeona kuwa watu wengi wanaonesha upendo wao kwa njia ya zawadi na zana mbalimblai za msaada kwa wenye shida. Tuwashukuru wanaparokia yetu ambao wameweza kusaidia masikini. Kwa kuhitimisha askofu Mkuu amewaalika wahusika wanaogawa misaada kuhakikisha kuwa vitu hivyo vinawafikia watu ambao kweli wanahitaji.

Naye Kardinali Anthony Olubunmi Okogie, Jimbo Kuu  la Lagos, kwa upande wake amesisitiza kuwa covid-19 inaweka mwanga juu ya ukosefu wa majengo ya kiafya nchini Nigeria kutokana na ufisadi. “Ikiwa uongozi wa kiwango cha chini ukichanganya na tabia inayoonekana wazi kuwa isiyozuilika ya kuiba na kufuja pesa za Nigeria, unajikuta katika nchi ambayo hospitali zao hupunguzwa kuwa vyumba vya ushauri tu.”

06 May 2020, 12:37