Tafuta

Vatican News
“Kumbu kumbu ya miaka 25 ya Ut unum sint inapaswa kutukumbusha kuwa uekumene ni njia moja tu ya Kanisa na kwamba wakatoliki wote wanaalikwa kukumbatiwa na sababu ya umoja wa wakristo na kufanya kila jitihada hai kwa ajili yake. “Kumbu kumbu ya miaka 25 ya Ut unum sint inapaswa kutukumbusha kuwa uekumene ni njia moja tu ya Kanisa na kwamba wakatoliki wote wanaalikwa kukumbatiwa na sababu ya umoja wa wakristo na kufanya kila jitihada hai kwa ajili yake. 

Marekani:Ut unum sint:jitihada kwa ajili ya umoja wa wakristo ni wajibu wa wakatoliki wote!

Kumbu kumbu ya miaka 25 ya Ut unum sint inapaswa kutukumbusha kuwa uekumene ni njia moja tu ya Kanisa na kwamba wakatoliki wote wanaalikwa kukumbatiwa na sababu ya umoja wa wakristo na kufanya kila jitihada hai kwa ajili yake. Ni kwa mujibu wa Askofu Joseph C. Bambera rais wa Tume kwa ajili ya masuala ya uekumene na kidini wa Baraza la Maaskofu nchini Marekani,(Usccb) katika fursa ya miaka 25 tangu kutangaza kwa Wosia huo na Mtakatifu Yohane Paulo II 1995.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Askofu Joseph C. Bambera wa jimbo la Scranton na  rais wa Tume kwa ajili ya masuala ya uekumene na kidini wa Baraza la Maaskofu nchini Marekani,(Usccb) wakati wa kilele cha kumbu kumbu ya miaka 25 ya Wosia wa  “Ut unum sint” unaohusu masuala ya  Uekueme iliyotangazwa na Mtakatifu Yohane Paulo II, kunako  tarehe 25 Mei 1995 amesisitiza juu ya jitihada za kwa ajili ya umoja wa wakristo kwamba  wosia huo ni wajibu wa wakatoliki wote.  “Kumbu kumbu ya miaka 25 ya Ut unum sint inapaswa kutukumbusha kuwa uekumene ni njia moja tu ya Kanisa na kwamba wakatoliki wote wanaalikwa kukumbatiwa na sababu ya umoja wa wakristo na kufanya kila jitihada hai kwa ajili yake.” Aidha amesema “juhudi kubwa bila kuchoka ya Papa wa kipoland ya kutaka kujenga uhusiano wa kiekumene, imeendelezwa na Papa mstaafu Benedikto XVI na Papa Francisko kwa kuruhusu Kanisa katoliki na jumuiya nyingine za kikirsto kugundua daima masuala ya undani ya kitaalimungu”, amethibitisha Askofu  Bambera.

Jitihada za kujenga madaraja na kusaidiana kwa upendo

Ni matumaini ya askofu Bambera kuwa katika mwaka huu uweze kuwa fursa ya kujenga madaraja kwa kujitahidi kusaidiana kwa upendo na ndugu, kaka na dada katika Kristo,na zaidi katika kipindi hiki cha janga na kwa maana ya kushirikiana sana na wakristo katika umoja, ili kushuhudia kwa pamoja amani ya Kristo katika ulimwengu wote ambao unahitaji sana”.

Safari iliyotimizwa hadi sasa ni njia njema ya kuponya majeraha yaliyopita

Kwa mujibu wa askofu Bambera, amekumbusha kuwa  hatua za mchakato uliotimizwa wa majadiliano ya kiekuemene katika miaka ya mwisho ili kuponya majeraha ya karne na milenia, yamekumbukwa na Papa Francisko katika barua yake aliyoiandika tarehe 24 Mei 2020 kwa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo ambapo Papa anashukuru sana mchakato wa safari uliotimizwa na kuthibitisha “kukubali ule uvumilivu mzuri wa kutaka kufanya zaidi na kukumbusha kuwa umoja siyo matokeo msingi wa matendo yetu, bali ni zawadi ya Roho Mtakatifu”.

 

26 May 2020, 14:21