Tafuta

Kumbu kumbu ya Miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II Kumbu kumbu ya Miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II  

MAREKANI:Kumbukizi la Mt.Y.Paulo II katika maisha ya Ask.mkuu wa Los Angeles!

Katika kumbukumbu ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane II,Askofu Mkuu wa Los Angeles,ameandika kuwa Yesu aliwambia wafuasi wake usiku ule wa Pasaka kwamba wasiwe na hofu.Na Mtakatifu Yohane Paulo II,mara kwa mara alirudia maneno hayo na zaidi kusisitiza kuwa “Msiogope.Fungulieni milango Kristo".Maneno haya yamemsaidia katika tafakari kwenye kupindi hiki cha dharura ya ulimwengu.

Na Sr. Angela Rwezaua – Vatican  

Katika makala ya wiki inayotolewa katika lugha ya kingereza na kusipanyola kwenye tovuti ya jimbo Kuu Katoliki la Los Angeles, Askofu Mkuu wa jiji hilo ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani, José H. Gomez, ametoa ushuhuda wake wa kumbukizi ya Mtakatifu Yohane Paulo II katika fursa ya kutimiza miaka 100 tangu kuzaliwa kwake, tukio lilofikisha kilele tarehe 18 Mei 2020. Katika kumbukumbu hiyo Askofu Mkuu ameandika kuwa “Yesu alikuwa amewambia wafuasi wake usiku ule wa Pasaka ya kuwa “msiwe na hofu”. Na Mtakatifu Yohane Paulo II, mara kwa mara alirudia  maneno hayo na zaidi kusisitiza kuwa “Msiogope. Fungulieni milango Kristo”.

Kuzingatia neno la ‘msiwe na hofu’

Katika maneno hayo ya kina, Askofu Mkuu Gomez amesema kuwa yuko anazingatia kwa namna ya pekee maneno hayo katika sala zake kwa kipindi hiki cha covid-19,  hivyo anasema “Ninasali kwa ajili yenu ninyi ambao mnahangaika na mambo yenu, kwa ajili ya kazi zenu, kwa ajili ya kufikiria itakavyokuwa wakati endelevu wa watoto wenu na wapendwa wenu, kwa ajili ya uchumi wetu na kwa ajili ya mtindo wetu wa maisha. Ninasali kwa ajili ya ninyi nyote mnaoomboleza na kuhisi kuwa mmeachwa peke yenu.  Tumo ndani pamoja katika hali hii na kuteseka wote. Katika huruma yake Mungu yupo anaruhusu janga hili kugusa sisi sote na anatuomba tuwe na uvumilivu wa kushinda lakini bila kuwa na faraja ya Sakramenti, bila ya kuja kanisani kwa wiki nyingi. Huu ni huzuni wa kina kwangu mimi na kama ilivyo kwenu ninyi”.

Matukio muhimu katika maisha yake yanayohusiana na Papa Yohane Paulo II

Katika kurudi kwenye  tukio la Papa Wojtyla, yaani Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye ametimiza miaka 100 tangu kuzaliwa kwake, Askofu Mkuu José H. Gomez, wa Los Angeles amebainisha kwamba “ninahisi muungano wa kina na Yeye na ninasali sana kwa ajili ya maombezi yake, hasa  nikitafakari jinsi gani maisha yangu katika huduma yangu ya kichungaji imekuwa na uhusiano wa karibu. Nilipewa daraja la upadre miezi miwili kabla ya kuchaguliwa kwake kuwa Papa kunako mwaka 1978, na ni yeye aliyenichagua kuwa Askofu kunako mwaka 2001. Kunako mwaka 2004 hatimaye ni yeye akaniteua kuwa Askofu Mkuu miezi michache kabla ya kifo chake.”

Lengo kuishi ni kumjua,kumpenda Yesu na kushirikishana wengine maisha yake

Aidha Askofu Mkuu Gomez, anaandika kwamba “Mtakatifu Yohane Paulo, alitukumbusha sisi sote ya kwamba lengo la maisha yetu ni kumjua Yesu, kumpenda na kushirikisha maisha yake kwa wengine. Katika kipindi hiki cha Pasaka, tumerudia mara nyingi kusoma Kitabu cha Matendo ya Mitume na historia ya mwanzo wa Kanisa. Wafuasi wa Kwanza wa Yesu walitoa kila kitu na misha yao kwa ajili ya kumfuata Yesu na kuendeleza utume wake”. Kwa maana hiyo “upendo wao kwa ajili yake ulikuwa na nguvu sana hadi kuweka pembeni kila aina ya hofu. Kumfuata Kristo maana yake ni kushirikishana maisha yake. Maana yake ni kubeba naye msalaba. Maana yake ni kukubali kuwa sisi tuteseka kama Yeye alivyoteseka kwa ajili yetu”.

Katika kitabu chake chenye kichwa cha habari: 'Kuvuka kizingiti cha tumaini', Mtakatifu Yohane Paulo II aliandika kuwa, “upendo ulijifanya mtu, Upendo ulisulibiwa na kufufuka, upendo daima upo kati ya watu”. Ni upendo wa Ekaristi”… Kwa maana hiyo Askofu Mkuu  anaongeza “Ni yeye peke yake anaweza kutoa usalama wa hakika kwani alidhibitisha kuwa ‘msiwe na woga! Yesu anatuita muda huu ili kupenda bila kubakiza lolote. Tunatakiwa kusaidia jirani ili asimame. Tunatakiwa kuwasadia kulilia marehemu wao na kuwaponya majeraha yao na ili waanze kwa upya maisha yao.

Maskini wasisahaulike

Tunatakiwa kufanya kila njia kwa namna kwamba maskini hawasahauliki. Sisi sote tumo ndani. Kwa sasa tunayo nguvu mpya zaidi ya awali kwa pamoja ili kuweza kufanya vizuri. Kwa kuhitimisha amesema, tuombe kwa Mama yetu Maria kwa maombezi yake wakati tunajiandaa kufujungulia kwa upya katika jamii na makanisa yetu. Tumkabidhi maisha yetu katika Moyo safi , kama alivyo fanya Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili. Tusema kama yeye alivyosema ‘Totus tuus’. ‘Yote kwa Mama Maria”.

23 May 2020, 10:35