2020.05.05 Kanisa kuu la Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili (Urakami)Nagasiki,Japan. 2020.05.05 Kanisa kuu la Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili (Urakami)Nagasiki,Japan. 

JAPAN#coronavirus:katika harakati za msaada,caritas yazindua mfuko maalum!

Wakati Kanisa linangojea mwisho wa hali ya dharura ili kuanza kwa upya maadhimisho ya misa kwa umma,Caritas nchini Japan imezindua mfuko maalum kwa ajili ya janga la virusi vya corona ili kuweza kutoa msaada katika sekta mbali mbali za kijamii kufuatana na shida iliyojitokeza kwa sababu ya janga hili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya mfuko maalum kwa ajili ya dharura ya janga la virusi vya Corona ndiyo uzinduzi wa Caritas nchini Japan ambapo fedha hizo zitakwenda kusaidia maeneo yote yenye dharura. Kwa namna ya pekee mfuko huo utasaidia kuwapatia mahali pa kulala wale wasio kuwa na makazi, wahamiaji na wale wote ambao wamepoteza nyumba zao kutokana na kipeo cha mgogoro huu ambao tunafanya uzoefu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti ya Baraza la Maaskofu Japan, wanabainisha pia kuwa Mfuko wa fedha hizo utasaidia kutoa chakula na nguo kwa watu ambao wamebaki bila kuwa na kipato kwa sababu wamepoteza kazi au shuguli zao za kila siku zimefungwa.

Aidha kuongneza mifumo ya majengo mengine kwa ajili ya kuwakaribisha waathirika wa vurugu za majumbani. Na misaada hiyo itatumika kusaidia raia wa kigeni (wafanyakazi, wafanya mazoezi, mafundi, lakini pia wafungwa na wanaotafuta hifadhi) ambao hujikuta wamekwama nchini kutokana na dharura na kutoa msaada kwa watu walio katika mazingira magumu, kama vile walemavu na wazee. Mwishowe, watasaidia kuunda vituo vya habari kwa wale ambao, kwa sababu ya lugha, uzee au mlemavu, wana ugumu wa kupata habari na kusaidia vituo vya huduma ya afya ambavyo haviwezi kupokea vifaa vya kutosha vya matibabu.

Hata hivyo nchini Japan inasubiri kwa hamu kubwa  kwa  kile kiitwacho hatua ya pili. Kuanzia tarehe 6 Mei 2020, Serikali nchini humo itaweza kutoa taarifa kama ni kuongeza muda tena au bado kutokana na dharura iliyotangazwa mwezi mmoja uliopita kwa udhibiti usambaaji wa virusi vya corona. Maamuzi hayo yanasubiriwa kwa hamu hata katika jumuiya ndogo ya kikatoliki nchini humo huko Sol Levante, mahali ambapo misa zote zilisitishwa katika jimbo lote kwa mujibu wa sheria zilizowekwa. Kwa mujibu wa maamuzi ya viongozi wa serikali, maaskofu nao wataweza kutoa uamuzi na jinsi gani ya kuweza kurudia kufanya liturujia kwa umma na shughuli nyingine za Kanisa.

Kwa maana nyingine hata waamini katoliki nchini Japan walialikwa kuishi kipindi hiki cha wasi wasi mkubwa kwa sala za kina, huruma, ushirikiano na kufuata sheria zilizowekwa za kuziui kuenea kwa virusi vya corona na kuwa makini katika nafasi na kumlinda mwingine. Katika ujumbe ulitangazwa wa kichugaji wakati wa  Pasaka, Rais wa Baraza la Maaskofu, Askofu Joseph Sanmei Takami alikuwa amewashauri waamini kutumia fursa ya kipindi hiki kutafakari juu ya maisha yao ya imani yao na juu ya uhusiano walio nao kwa  wengine ikiwa ni pamoja hali halisi ya viumbe katika mazingira kwa ujumla.

05 May 2020, 11:20