Cei: Bassetti, Sinodo probabile ma percorsi sono lunghi Cei: Bassetti, Sinodo probabile ma percorsi sono lunghi 

ITALIA#coronavirus:Liturujia za misa kuanza tena tarehe 18 Mei 2020 nchini Italia!

Makubaliano yaliyosainiwa kati ya Kanisa la Italia na serikali yake yanalenga kuhakikisha usalama wa kila mwamini na utumiaji wa kila jamuiya ya kikanisa.Hiyo ni hatua muhimu iliyowezekana kwa ushirikiano ambao haukukatika kamwe.Tarehe 18 Mei 2020 itakuwa siku rasmi kuanza tena maadhimisho ya liturujia katika Makanisa nchini Italia baada ya miezi hii ya janga la corona.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Itifaki itakayoruhusu kuanza tena kwa maadhimisho ya liturujia na watu mesainiwa asubuhi Alhamisi tarehe 7 Mei 2020, katika Jumba la Chigi jijini Roma. Hayo ni Maandishi yanayohitimisha mchakato wa njia ambayo imeona ushirikiano kati ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI), Waziri Mkuu wa Italia, Waziri wa Mambo ya Ndani hasa kaktika maelekezo, Mkuu wa Kitengo cha uhuru wa Raia na Uhamiaji, Michele di Bari, Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Alessandro Goracci na Kamati ya Ufundi-Sayansi.

Kwa kufuata kanuni za kiafya zilizotayarishwa kwa ajili ya kuzuia na usimamizi wa dharura ya janga kutoka SARS-CoV-2, Itifaki inaonyesha hatua kadhaa zinazopaswa kufuatwa kwa uangalifu, kuhusu ufikiaji wa maeneo ya ibada wakati wa maadhimisho ya liturujia; Usafi wa mazingira ya mahali na vitu; Umakini unaopaswa kuzingatiwa katika maadhimisho ya kiliturjia na sakramenti; mawasiliano yatakayo tayarishwa kwa waamini na maoni kadhaa kwa jumla. Maandishi hayo yamezingatia kuunganisha mahitaji ya kulinda afya ya umma kwa maelekezo yaliyo wazi na ili kuwafikia kila jumuiya ya kikanisa.

Itifaki umesainiwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI), Kardinali  Gualtiero Bassetti, Waziri Mkuu wa Italia Bwana Giuseppe Conte na Waziri wa Mambo ya Ndani Bi Luciana Lamorgese ambayo itaanza kutumiaka rasmi siku ya Jumatatu tarehe 18 Mei 2020.

Kwa mujibu wa Kardinali Bassetti akielezea kwa mara nyingine tena jitihada za Kanisa katika kuchangia kushinda shida hii inayoendelea amesema "Itifaki hiyo ni matokeo ya ushirikiano wa kina  na mkakati kati ya Serikali, Kamati ya Sayansi ya Ufundi na Baraza la Maaskofu Italia (CEI), ambayo kila mmoja amefanya jukumu lake. 

NayeWaziri Mkuu Conte  amesisitza kuwa “Hatua za usalama zilizotolewa katika maandishi zinaelezea yaliyomo na njia bora ili kuhakikisha  kuanza tena kwa maadhimisho ya liturujia na watu ili iweza kufanyika kwa njia salama. Kadhalika ameshukuru Baraza la Maaskofu (CEI) kwa msaada na maadili ambayo wanaendelea kuwapa jamii nzima katika wakati huu mgumu wa nchi. Na kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Italia,  Bi. Lamorgese amesema kuwa tokea mwanzo wamefanya kazi ili kufikia Itifaki hiyo na kwamba kazi iliyofanywa pamoja imetoa matokeo mazuri. vile vile jitihada hizo hizo na ahadi moja  imefanyika kwa madhehebu mengine ya kidini.

08 May 2020, 14:57