Tafuta

Vatican News
Zaidi ya maneno ya matumaini,kuna ulazima wa matendo ya dhati,kwa maana ya msaada wa dhati ambao unasadia kuwapa tumaini la  kuaminika Zaidi ya maneno ya matumaini,kuna ulazima wa matendo ya dhati,kwa maana ya msaada wa dhati ambao unasadia kuwapa tumaini la kuaminika  

ITALIA#coronavirus:Patriaki Moraglia:baada ya lockdown kipaumbele kiwe ni hadhi ya binadamu!

Wakati tunapokaa mezani kula chakula tujiulize ikiwa,kwenye sahani yetu,kuna chakula cha haki,yaani,ambacho hakitokani na mchakato ambao umesahahu utu, hadhi na ulinzi wa watu.Ni tafakari aliyopenda kuishirikisha Patriaki wa Venezia,Italia kuhusu dharura ya uchumi na kijamii iliyosababishwa na covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Patriaki Francesco Moravia wa Venezia nchini Italia ameamua kuandika barua na kuishirikisha kwa waamini baadhi ya tafakari kuhusu dharura ya uchumi na kijamii iliyosababishwa na janga la covid-19. Katika tafakari hiyo anaandika kuwa “Kile ambacho tutaitwa kutambua katika miezi ya hivi karibuni ni hadhi ya mtu; tunaitwa kuvuka jangwa kiukweli, kuvuka kwa tumaini lilo gumu; ni wakati wa matarajio, ya matashi, na siyo tuangukie kishawishi cha kukata tamaa ambayo ni njia isiyo ya kutoka; ni kwa pamoja tu na kwa msaada wa Mungu, itawezekana kuondokana na mtazamo huu wa kutisha sana”.

Patriaki Moraglia anaendelea kwamba, kwa kuzingatia hali ya kipekee ya wakati huu lazima kuunganisha nguvu kwa ngazi zote ambazo katika mwelekeo unaofaa kufuatwa ni hadhi ya mtu na zaidi ya yote, ya wale ambao wanalindwa kidogo na walio hatarini zaidi.  Na kwa sababu hiyo Patriaki Moraglia ametaka kukumbuka hasa kujiua hivi karibuni kwa mfanyabiashara wa Napoli nchini Italia ambaye alikuwa anasumbuliwa kwa muda mrefu na hisia mbaya ya huzuni ambao umezidi kuongezeka katika siku za hivi karibuni, labda kutokana na matokeo ya kufungiwa ndani.

Akiendelea kukazia Ptriaki Moraglia na tafakari hiyo, “Kila juhudi lazima zifanywe kuzuia uchungu wa kina na upweke ambao umewakumba wengi kama zamani na shida mbaya sana kuliko ile ya sasa na wafanyakazi wengi waaminifu ambao waliona kuwa hawawezi kustahimili”. Vile vile Patriaki wa Venezia amesisitiza kuwa janga la huyo Antony lisiweze kurudiwa tena.  “Zaidi ya maneno ya matumaini, kuna ulazima wa matendo ya dhati, kwa maana ya msaada wa dhati ambao unasadia kuwapa tumaini la  kuaminika na lihamasishe. Kwani katika hali ya sasa inaonesha kuwa “Hata aina fulani za tumaini za zamani zilizokuwa na nguvu, sasa hazipo tena zimewekwa chini ya jaribi gumu”

Kwa mujibu wa Patriaki Moraglia, hadhi ya mtu ni nyota kuu ambayo lazima isindikizwa katika kukatisha barabara hii na kuna hata masuala ambayo yanatazama mamia elfu ya watu wa Italia, wageni na ambao hawawezi kudharauriwa maisha yao. Onyo analotoa Patriaki ni ule “uwepo umakini sana hasa kwa wale ambao hawana haki na ndiyo inawezekana kutokuonekana kwa kijamii na kutengeneza kile kiitwacho rasilimali ya kusikitisha kwa watu wa chini au kama mtu anayeweza kufanya vitendo vya uhalifu “au kama” shabaha na mwathiriwa wa vitendo hivyo”.

Kwa kuzingatia hilo, Patriaki Moraglia anatoa mfano akitaja wafanyakazi katika mashamba ya wakulima wanaodhulumiwa na kwamba “hawapaswi kuzingatiwa kama rasilimali ya kiuchumi tu, na kwa namna ya imedhibitiwa kutoka kwa mtazamo wa tija tu. Lakini kumbuka kuwa wakati tunapokaa mezani kula chakula tujiulize ikiwa, kwenye sahani yetu kuna chakula cha haki, yaani,ambacho hakitokani na mchakato ambao utu, hadhi  na ulinzi wa watu umesahaulika”, ameandika Patriaki wa Venezia.

08 May 2020, 15:16