Tafuta

ETHIOPIA:Wamehitimisha mwezi wa maombi ulioandaliwa na Baraza la Majadiliano ya Kidini nchini Ehiopia kuomba Mungu janga la corona liishe,kwa ajili ya madaktari na wahudumu na wagonjwa. ETHIOPIA:Wamehitimisha mwezi wa maombi ulioandaliwa na Baraza la Majadiliano ya Kidini nchini Ehiopia kuomba Mungu janga la corona liishe,kwa ajili ya madaktari na wahudumu na wagonjwa. 

ETHIOPIA#coronavirus:Baraza la Kidini limehitimisha mwezi wa maombi!

Tangu tarehe 4 Aprili hadi 5mei umefanyika mwezi wa maombi katika nchi ya Ethiopia ulioanzishwa na Baraza la Majadiliano ya Kidini nchini humo huko wakiomba Mungu aepushe janga la corona na kuwaombea madaktari na wahudumu wote wa afya walio mstari wa mbele katika janga ili ikiwa ni pamoja na waathirika wote nchini humo na duniani kote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 5 Mei 2020 umehimitimishwa mwezi wa Maombi uliokuwa umeanzishwa na Baraza la Kidini Nchini Ethiopia (Irce) kunako tarehe 4 Aprili 2020  kwa ajili ya kupambana na janga la virusi vya corona. Jambo katika hitimisho lake limeshirikisha uwezo wa viongozi wa serikali, meya wa Jiji la Addis Abeba  na viongozi wakuu wa dini katika nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Tovuti ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya Mashariki (Amecea) linabainisha kuwa siku 30 za mwisho, vyombo vya habari vya umma na baadhi ya vyombo vya mawasiliano binafsi vimeweza kujikita kwa masaa 240 katika maombi na mafundisho ya kijamii.

Shughuli hii ilipokelewa vema na waamini ambao wameshiriki idadi kubwa wakiungana kwa pamoja katika maombi kwa njia ya mitandao, shukrani kwa teknolojia mpya za kisasa. Kwa njia hiyo wahudumu na wataalam wa mawasiliano wamepongezwa rasmi na viongozi wote wa kidini kwa ajili ya jitihada zao zisizo na kifani. Mwezi wa maombi kitaifa umetolewa kwa ajili ya wahudumu wote wa afya ambao wanapambana wakiwa mstari wa mbele katika kudhibiti covid-19 (madaktari,wahudumu wote na watafiti) na wale wote ambao wameambukizwa na janga hili iwe nchini Ethiopia na ulimwengu mzima.

Hadi sasa  taarifa inabinisha kuwa katika nchi hiyo, idadi ya maambukizi ni 195,  waliopona ni 94 na vifo vya watu 4. Baraza la majadiliano ya Kidini liliundwa kunako mwaka 2010 nchini Ethiopia na kutambuliwa na Wizara ya Mambo ya Kitaifa ya Shirikisho na linawakilishwa kwa ngazi ya shirikisho, kikanda na wilaya. Malengo yake ni kukuza mazungumzo na kushirikiana kati ya dini na kuhimiza watu juu ya maswala maalum,kama vile uhuru wa kidini,usawa,amani,upendo na uvumilivu,kwa jina wema na ustawi wa kawaida kwa wote

09 May 2020, 13:59