Niliona mateso ya watu wangu na nikasikia kilio chao. Manenp yaliyomo katika ujumbe uliotiwa saini na Askofu Mkuu Jean Pierre Tafunga,wa jimbo Kuu la  Lubumbashi, nchini DRC kufuatia na dharura ya ukosefu wa usawa. Niliona mateso ya watu wangu na nikasikia kilio chao. Manenp yaliyomo katika ujumbe uliotiwa saini na Askofu Mkuu Jean Pierre Tafunga,wa jimbo Kuu la Lubumbashi, nchini DRC kufuatia na dharura ya ukosefu wa usawa. 

CONGO#coronavirus:Askofu Mkuu Tafunga alalamikia dharura ya kiafya &ukosefu wa usalama!

Katika kukabiliwa na hali hii na kwa nguvu ya imani yetu,tunalaani vikali ukosefu wa usalama huu na tunapendekeza kwa watu wasipoteze matumaini ya kumwamini Mungu kwa sababu ‘tumaini halidanganyi’ na wasisahau kamwe Bwana kuwa asipoulinda mji, walinzi walindao ni wa bure.Ndiyo ujumbe wa Askofu Mkuu Tafunga wa Lubumbashi akilalamikia ukosefu wa usalama na dharura ya kiafya kuongezeka.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mbele ya hali halisi hii na nguvu ya imani yetu tunalaani kwa nguvu ukosefu wa usalama. Ndivyo ujumbe wake unavyo anza uliopewa jina kutoka aya ya kitabu cha Kutoka kwa maneno haya “Niliona mateso ya watu wangu na nikasikia kilio chao. Ujumbe huo umetiwa saini na Askofu Mkuu Jean Pierre Tafunga, wa jimbo Kuu la Lubumbashi, nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) na kuchapishwa kwenye tovuti ya Baraza la maaskofu.

Askofu kushirikishana mateso na waamini wake

Katika kufafanua hali halisi ilivyo Askofu Mkuu Tafunga ameandika kuwa “Kutokana na wasiwasi wa kichungaji kwa ajili ya watu wanaoishi Lubumbashi, ninashirikishana nao mateso na kwa fadhila ya utume wa kinabii uliounganishwa na jukumu letu la kichungaji, tumechunguza na kubaini hali ya kushangaza na ya kutia kiwewe cha mji”. Hata hivyo ameongeza “ikumbukwe kuwa hali hiyo hiyo imekuwa ikifanyika katika sehemu nyingine za Mkoa wa Haut-Katanga na imekuwa kwa muda mrefu”. Ameasema.

Uchumi kuzidi kuwa mbaya wakati wa covid-19

Askofu Mkuu Tafunga aidha ameandika “katika kipindi hiki kigumu wakati ulimwenguni kote umetetemeshwa na mgogoro wa kiafya kutokana na janga la virusi vya corona, afya ya uchumi katika wilaya yetu ni mbaya sana”. Inazidi kuwa mbaya sana kila siku. Tunashuhudia kupungua kwa kiwango cha ukuaji, hasa wakati tunajua kuwa tunategemea sana Afrika Kusini, ambayo haizuii mipaka yake kufungwa mara kwa mara na ambayo lakini husababisha bidhaa zake kuwa za gharama.

Hali halisi inazidi kuwa hatarini hasa ukosefu wa usalama

Hali ya maisha ya watu inazidi kuwa hatarini, amebainisha huku akizungumza juu ya nchi ambayo amesema dharura za kiafya kwa bahati mbaya ni za kawaida kwa kuongezea Covid, kiukweli, Ebola na surua pia vinaleta wasiwasi mkubwa. “Tunatambua kuwa idadi ya watu wa jiji la Lubumbashi wanakabiliwa na ongezeko la kila siku la ukosefu wa usalama ambapo imefikia kiwango ambacho mpaka sasa hakieleweki. Hakuna usiku inaopita bila kujua kuwa ubakaji, ujambazi, mauaji vinafanyika na zaidi nje kidogo ya jiji, mahali ambamo watu masikini zaidi wanaishi”.

Bwana asipoulinda mji wake waulindao wafanya kazi bure

Kwa kuhitimisha ujumbe wake ameandikia “Katika kukabiliwa na hali hii na kwa nguvu ya imani yetu, tunalaani vikali ukosefu wa usalama huu na tunapendekeza kwa watu wasipoteze matumaini ya kumwamini Mungu kwa sababu ‘tumaini halidanganyi’ (rej Rm 5: 5) na wasisahau kamwe Bwana kuwa asipoulinda mji, walinzi walindao ni wa bure’(Zab 127: 1). Kwa maana hiyo tunapendekeza kwa watu wetu wawe na uangalifu na kuwa na mshikamano katika nyakati hizi ngumu ambazo mji wetu wa Lubumbashi unapitia na kwa sababu tunakabiliwa na maadui wawili wa kutisha kwanza, virusi vya corona na majambazi wenye silaha, wote wawili ambao wanaondoa usalama.

21 May 2020, 16:04