Tafuta

Bila wazee hakuna wakati ujao.Ni lazima kuleta mabadililo ya kibinadamu katika jamii zetu.Hapana kuwepa uchaguzi wa huduma ya afya. Mchango wa wazee unakuza ustaarabu wa Ulaya. Bila wazee hakuna wakati ujao.Ni lazima kuleta mabadililo ya kibinadamu katika jamii zetu.Hapana kuwepa uchaguzi wa huduma ya afya. Mchango wa wazee unakuza ustaarabu wa Ulaya. 

Jumuiya ya Mt.Egidio,Coronavirus#:Hitaji la badiliko kibinadamu.Bila wazee hakuna wakati ujao!

Ni lazima kuleta mabadililo ya kibinadamu katika jamii zetu.Bila wazee hakuna wakati ujao.Hapana uchaguzi wa huduma ya afya.Mchango wa wazee unakuza ustaarabu wa Ulaya.Ni wakati wa kutumia rasilimali zote muhimu ili kulinda idadi kubwa ya maisha na upatikanaji wa tiba na utunzaji wa wote bila kubagua.Thamani ya maisha inabaki kuwa sawa kwa kila mtu.Ni katika tamko la pamoja la kimataifa,la Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na wadau wake katika kutetea wazee ambao wako hatarini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kutokana na wasiwasi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kuhusu wakati ujao wa jumuiya za sasa, ambazo zimejionesha katika siku hizi za mgogoro uliosababishwa na virusi vya corona au covi-19, ndiyo umetoa mwamko wa kuweza kutoa tamko ambalo limetafsiriwa kwa lugha mbali mbali na kutangazwa tarehe 20 Mei 2020 kwa ngazi ya kimataifa. Wito huo umetiwa sahini na viongozi mbalimbali wa Ulaya, lakini miongoni mwao aliye mstari wa mbele ni  Andrea Riccardi, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,Parodi, Habermas, Sachs, Gonzalez, Pöttering, Zuppi, Bokova, De Rita ...na wengine.

Bila wazee hakuna wakati endelevu

Tamko hilo kwa ngazi ya kimataifa upewa jina:"Kuleta mabadililo ya kibinadamu katika jamii zetu.Bila wazee hakuna wakati ujao.“Kwa maana hiyo wanapinga kwamba "Hapana uchaguzi wa huduma ya afya". Wito huo unawalenga kila mtu, raia na taasisi, katika mabadiliko ya kiakili ambayo yalete pamoja ile mipango mpya ya kijamii na kiafya mbele ya watu walio wazee.  Katika janga la  Covid-19, wazee wako hatarini katika nchi nyingi za Ulaya na kwingineko.I dadi ni kubwa ya vifo inayofanya utetemeke katika taasisi za kutunzia wazee. Aidha wanabainisha kwamba "Kutakuwa na mengi ya kukagua katika mifumo ya afya ya umma na katika uzoefu mzuri wa lazima ili kufikia na kutibu kila mtu, bila kujali kwani wanasikitishwa na vifo vingi vya wazee vilivo tokea katika taasisi nyingi za kutunzia wazee.

Kuibuka kwa huduma za afya za upendeleo

Katika tamko lao wanabainisha hatari kwamba "Wazo ambalo linasikika ni le la uwezekano wa kuondoa maisha yao kwa ajili ya wengine kushikilia nafasi yao. Lakini Papa Francis anaizungumzia juu ya utamaduni wa ubaguzi ambapo kuwaondolea mbali wazee haki yao bila kuwafikiria na kuwaona kama namba, jambo ambalo halikubaliki". Katika nchi nyingi zinazokabiliwa na hitaji la utunzaji, kwa sasa mfano wa hatari unaibuka ambao unapendelea huduma za afya za kuchagua, ambamo huchukulia maisha ya wazee kama mabaki. Kuathirika kwao, kutokana na umri wao, uwezekano mwingine wa maradhi ndiyo unasababisha kuhalalisha aina ya chaguo kwa niaba ya walio vijana na wenye afya zaidi", tamko hilo linasisitiza.

Haiwezekani kupunguza thamani za maisha 

Aidha kujiachia katika matokeo haya kibinadamu na kisheria halikubaliki. Pia hata katika maono ya maisha ya kidini, lakini pia  hata katika mantiki ya haki za binadamu na maadili ya matibabu. Haiwezekani kuhalalishwa kwa mtu yoyote au kuweka hali hiyo kuwa kanuni hizi zinazoweza kupitishwa. Katika nadharia  inayochukuliwa maisha mafupi na kusababisha kupunguza kwa kisheria thamani yake, kwa maoni ya kisheria ni upendeleo mbaya sana. Kile ambacho kinaweza kutokea kwa mujibu wa kuwekwa na Serikali au Mamlaka za afya nje ya utashi wa mtu, inawakilisha jambo lisilovumiliwa zaidi la haki za mtu mwenyewe.

Mchango wa wazee ni muhimu katika ustaarabu wa jamii

Katika tamko lao pia wanasema, mchango wa wazee unaendelea kuwa mada ya tafakari muhimu katika ustaarabu wote. Na ni msingi katika njama ya kijamii ya mshikamano kati ya vizazi. Kwa kukazia wanasema "Hakiwezi kuachwa kizazi kife kilichopigana dhidi ya udikteta, kilichojitahidi katika ujenzi mpya  baada ya vita na kujenga Ulaya".  “Tunaamini kuwa ni lazima kudhibiti tena kanuni za matibabu sawa na haki ya matibabu, ambayo ililèta ufanisi kwa karne nyingi. Ni wakati wa kutumia rasilimali zote muhimu ili kulinda idadi kubwa ya maisha na upatikanaji wa tiba na utunzaji wa wote. Thamani ya maisha inabaki kuwa sawa kwa kila mtu. Wale wasiowathamini wanyonge na dhaifu wa wazee, wajitayarishe kudharau kila kitu.

Vifo ni vingi vilivyotokea katika taasisi za wazee

Kwa kuhitimisha wito huo wanaelezea uchungu na wasiwasi kwa vifo vingi sana vya wazee katika miezi ya hivi karibuni na wanatumaini kuwa mabadiliko ya kimaadili yawepo katika mwelekeo wa utunzaji wa wazee, ili kwamba wale walio hatarini zaidi wasichukuliwe kama vile mzigo au mbaya zaidi na wasio kuwa na maana. 

Ikumbukwe Watia sahihi wa kwanza ni Andrea Riccardi, mwanahistoria na Mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio; Romano Prodi, Waziri Mkuu Mstaafu na wa Tume ya Umoja wa Ulaya; Jeffrey D. Sachs, Mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mtandao wa Suluhisho la Maendeleo Endelevu; Aleksandra Dulkiewicz, Meya wa jiji la Danzika, Poland; Simonetta Agnello Hornby, Mwandishi wa vitabu nchini Uingereza; Manuel Castells, Profesa wa Masuala ya kijamii katika Chuo Kikuu cha California Berkeley, kutoka Uhispania; Irina Bokova, Mkurugenzi Mtaafu wa UNESCO, na mjumbe wa Kamati Kuu ya Udugu  wa Kibinadamu, wa Bulgaria; Mark Eyskens, Waziri Mstaafu wa Ubalgiji; Hans Gert Pöttering, Spika Mtaafu wa Bunge la Ulaya wa Ujerumani;

Vile vile: Felipe González Márquez, Waziri Mkuu Mstaafu wa Uhispania; Marie De Hennezel, Mtaalam wa kisaikolojia wa Ufaransa; Jean-Pierre Denis, Mkurugenzi wa Gazeti la kila Wiki ‘La Vie’, Ufaransa; Kardinali Matteo Zuppi, Askofu Mkuu wa Bologna, Italia; Adam Michnik, mtunzi na kurugenzi wa Gazeti la Wyborcza, Poland; Michel Wieviorka, Mtaalamu wa masuala ya kijamii na Mwenyekiti wa Mfuko wa Nyumba ya Kisayansi huko Paris, Ufaransa; Giuseppe De Rita, Mwanzilishi wa CENSIS; Stefania Giannini, Mkurugenzi Mkuu wa mwandamizi wa UNESCO; Maria Antónia Palla, mwandishi wa habari nchini Ureno; Navi Pillay, Hakimu, Rais wa ICDP, Afrika Kusini; Annette Schavan, Waziri mstaafu wa Elimu na Utafiti katika Shirikisho la Ujerumani na Jürgen Habermas, Mwanafalsafa, Ujerumani.

20 May 2020, 11:31