Tafuta

Vatican News
Mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia (FABC)umeahirishwa ambao ulikuwa ufanyike Novemba mwaka huu sambamba na maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuunda shirikisho hilo Mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia (FABC)umeahirishwa ambao ulikuwa ufanyike Novemba mwaka huu sambamba na maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuunda shirikisho hilo  (Vatican Media)

ASIA#Coronavirus:Mkutano mkuu wa Baraza la maaskofu Asia Fabc umeahirishwa!

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki barani Asia(Fabc)limeahirisha Mkutano wake Mkuu uliokuwa ufanyike mwezi Novemba mwaka huu kuanzia tarehe 3-20,sambamba na maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo kutokana na hali halisi ya dharura ya kiafya duniani kwa janga la covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican  

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Barani Asia (Fabc) limeamua kuahirisha Mkutano Mkuu waouliokuwa ufanyike huko Baan Phu Waan, nchini Thailand. Mkutano huo ulikuwa ufanyika kuanzia tarehe 3-20 Novemba 2020. Na hii ni kutokana na kukosa uhakika wa maendeleo ya dharura ya Covid-19 smbslo limelazimisha waahirishe. Na wakati huo huo kwa sababu hiyo pia wameahirisha hata mikutano yote ya Kamati kuu na vitengo mbali mbali vya shirikisho hilo Fab iliyokuwa inatazamiwa kufanyika mwezi Juni Mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo hiyo  ya barua iliyotiwa sahini na Kardinali Charles Bo, Askofu Mkuu wa Kanisa Kuu la Yangon na Askofu Mkuu Oswald Gracias, wa Jimbo Kuu Katoliki la Bombay, wote wakiwa ni wenyeviti kwa upande wa Fabc  na wa maandalizi ya Mkutano kwa mwaka huu wanaandika kuwa kwa sasa hali ina msimamo japokuwa hawajuhi kile kitakachotokea baadaye.

Katika barua yao,viongozi wa Kanisa, iliyotajwa na Shirika la Habari za Kanisa canews, wanabainisha kwa dhati kwamba wataweza kuandaa tarehe nyingine za kufanya shughuli zao, ikiwa hali itarudia kuwa ya kawaida. Lakini licha ya ukosefu wa uwezekano wakuweza kuzunguka kutoka nchi mahalia kwenda nchi nyingine, Maaskofu barani Asia wameeendelea kuwasiliana na mikutano kwa njia ya video katika wiki hizi ili kukabiliana juu ya matatizo mbalimbali ya kichungaji ambayo kama makanisa barani Asia wanatakiwa kuendeleza mbele.

Yapo mambo mengi ya kutafakari wanathibitisha Kardinali Bo na Gracias katika barua yao ambayo inaonesha kuwa licha ya lockdown, makanisa washiriki wa Shirikisho la Fabc wanahisi kuunganika zaidi katika kipindi hiki cha giza duniani. Kipindi kama hiki wanasema, kimefanywa uzoefu mkubwa wa kumtegemea Mungu na ambacho kimeongeza nguvu ya imani yetu. Ni mategemeo kuwa wote wataondokana na mgogoro huu wakiwa na utambuzi zaidi wa maana ya kina ya kidini.

Mkutano Mkuu wao ulikuwa unatarajia kuadhimisha jubileo ya miaka 50 ya Shirikisho lao Fabc lililoundwa kunako mwaka 1970, wakati maaskofu 180 wa Bara la Asia walipoungana huko Manila katika Ziara ya Kitume ya Mtakatifu Yohane Pulo II nchini Ufilippini. Shirikisho hili linaunganisha Mabaraza ya Maaskofu 19  na vyama wanachama 8 kwa lengo la kuhamasisha mshikamano na uwajibikaji kwa washiriki wake kwa ajili ya wema na ustawi wa Kanisa na watu wote barani Asia.

Siku hii maalum ilikuwa pia imekumbukwa na Papa Francisko wakati wa Ziara yake ya Kitume nchini Thailand na Japan mwezi huo huo wa Novemba. Katika fursa yamkutano wao  tarehe 27 Novemba na maaskofu wa Thailand na wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Asia Fabc Katika Madhabahu ya Mwenyeheri Nicolas Bunkerd Kitbamrunghuko Bangkok, Papa Francisko alikuwa ametoa ushauri wa kujifungulia ujasiri kwa kuwa na roho ya kinabii na roho ya wakati ujao ambapo walialikwa kutoka na kujikita katika hali halisi na ili Kanisa kama ilivyo Jamii ya Asia ifaidike na matunda ya Kiinjili, kushirikishana na yaliyopyaishwa.

07 May 2020, 11:39