2020.04.11 Askofu  Moses Hamungole wa Jimbo katoliki la Monze, Zambia 2020.04.11 Askofu Moses Hamungole wa Jimbo katoliki la Monze, Zambia 

Zambia:Askofu Hamungole:Tuwe kama wanawake chini ya Msalaba wa Yesu!

Kwa kuongozwa na ibada ya Mateso ya Bwana wetu,Askofu Moses Hamungole wa Jimbo Katoliki la Monze nchini Zambia amewaalika wakristo kutumia muda huu ili kugundua namna nyingi ambazo Yesu anasalitiwa na kukataliwa.Anawahimiza wafuate mfano wa Mama Maria na wanawake waliokaa chini ya Msalaba hadi mwisho.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican  

Kujifunza kutoka kwa Mama Maria na wanawake wanaliomfuata Yesu hadi Kalvari ndiyo ujumbe ulitolewa kwa waamini wote na Askofu Moses Hamungole, wa jimbo katoliki la Monze, nchini Zambia, wakati wa ibada  ya Ijumaa Kuu tarehe 10 Aprili 2020. Kwa kuongoza ibada ya Mateso ya Bwana wetu, Askofu Hamungole amewaalika wakristo kutumia muda huu ili kugundua namna nyingi ambazo Yesu anasalitiwa  na kukataliwa. “Nikitafakari Mateso ya Bwana Yesu Kristo amesema, zinajitokeza fursa nyingi na uchaguzi wa Pilato na watu wa Israeli walikuwa wanatambua vema kuwa Baraba alikuwa ni mwizi, lakini wakachagua ahukumiwe Yesu. Wakati mwingine ni vigumu kutambua jinsi gani mifumo ya majaji inavyo fanya kazi kwa sababu, tunaona watu wasio kuwa na hatia wanahukumiwa na wenye makosa wanaachiliwa huru”, amebainisha Askofu.

Ni huzuni kuona viongozi wanashindwa kisiadia na kutetea haki za kisheria za raia

Askofu Hamungole katika tafakari hii aidha amesema, “mara nyingi tunajiuliza ni kosa gani lilijitokeza kwa Pilato, mbaye alikabidhiwa majukumu ya kuongoza na kutoa hukumu kwa usawa na haki? Hawa walikuwa wanajua kwa hakika kipi chenye haki na jinsi sheria inavyotakiwa kutumika kwa usawa na bila kuwa na hofu. Pamoja na hayo yote ni huzuni kuona taasisi yase rikali haziwezi kuhakikishia imani na haki za raia wao. Tumeona viongozi wakishindwa na kutoweza kusaidia utawala wa sheria kama wanavyotakiwa kutenda wajibu wao. Kiukweli inasikitisha sana, amesisitiza. Swali jingine ambalo amejiuliza: “je ni kitu gani ambacho hakiendi ikiwa  tunaona raia wanachagua kuwa sehemu ya kushuhudia uongo, kinyume na thamani za kikristo?

Onyo dhidi ya kugeuza kichwa sehemu nyingine

Katika kujibu swali hili, Askofu Hamungole anatoa onyo la “kuwa macho dhidi ya tabia ya kugeuza kichwa mahali pengine, ukijifanya usione, kwa sababu hakuna fadhila katika ukimya, wakati sauti ya mtu binafsi inaweza kuleta tofauti”. Kuna baadhi ya wengine wetu  amesema, ambao ni kama wale waolipiga kelele: ‘Siyo huyu mtu, bali  Baraba, msulubishe, msulubishe!' Tunawezaje kuishi na dhamiri zetu wakati tunajua kuwa tunafanya maamuzi mabaya?, amejiuliza  Askofu  Hamungole. Aidha ameongeza “Wakati mwingine tunakaa kimya, lakini kwa kufanya hivyo tunaendeleza ukosefu wa haki. Ndiyo, kuna athari katika kuzungumza, hii inapunguza hatari zinazo husiana na kusema mambo kwa sauti. Lakini tunasikia watu wakisema: “Jambo  moja muhimu kwa ajili ya ushindi wa mabaya ni kwamba watu wazuri hawafanyi lolote.”

Wakristo washirikiane na mamlaka kupambana na virusi

Askofu Hamungole pia ametoa wito kwa wakristo ili washirikiane na mamlaka ya nchi katika mapambano ya janga la virusi vya corona, kwa sababu ni jambo la haki kufanya hivyo katika nyakati ngumu. “Wote wachukue wakati wa kutafakari juu ya kujitoa kwetu binafsi kwa kufuata sheria ndani ya jamii zetu. Kwa mfano, chaguo kama la kukaa nyumbani linaweza kuleta mabadiliko katika maisha ya watu wengine wengi”. Na akaongeza: “Nchini Zambia na nchi nyingine nyingi, serikali zimetoa mwongozo ambao lazima uheshimiwe. Wakati watu wanadharau sheria hizi, wanaweka wengine hatarini. Kama Pilato na Wayahudi walifanya uchaguzi ambao ulisababisha kifo cha Yesu msalabani, vivyo hivyo,  Askofu ameonya  kuwa “ambaye hatii sheria za lazima za kuzuia maambukizi ya Covid-19  nahatarisha kueneza virusi au hata kusababisha vifo vya watu wengine, kwa sababu ya tabia mbaya.

Tuwe na ujasiri wa mama Maria na wanawake waliokaa msalabani

Ijumaa kuu, kwa maana hiyo iwe  ni “fursa ya kujihoji dhamiri zetu, majukumu yetu na uchaguzi wetu wa kila siku. Tunapo kuwa unatafakari juu ya Mateso  ya Bwana Yesu Kristo wa Jimbo la  Monze ametoa wito kuwa “ tukiri pia uchaguzi wetu mbaya na hofu zetu za kukosa  kutetea kilicho cha haki na sahihi. Tuombee ili tuwe na ujasiri wa kuwa kama Mama wa Yesu na wanawake wote  waliomfuata Bwana na kubaki katika msalaba Wake. Wanawake wanatupatia  mfano mzuri kwetu kwa sababu wamekuwa na Yesu hadi mwisho, hata wakati walikuwa wanajua kuwa ilikuwa ni hatari kwao. Na ili tuweze kuwa mashuhuda wa kifo chake na ufufuko wake.  Amehitimisha Askofu Hamungole

11 April 2020, 14:08