Tafuta

Vatican News
Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa Mkutano wa 26 kuhusu hali ya hewa (COP26) umeahirishwa  kwa kipindi kisicho julikana kwa sababu ya janga la virusi vya corona. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa Mkutano wa 26 kuhusu hali ya hewa (COP26) umeahirishwa kwa kipindi kisicho julikana kwa sababu ya janga la virusi vya corona. 

Uswiss:Shirikisho la kiluteri duniani kuhusu janga na dharura ya tabianchi!

Shirikisho la Kiluteri duniani kwa kutazama janga la sasa la covid-19 na dharura ya tabiachi,linasisitiza ulazima wa kukabiliana na mgogoro.Linaalika serikali zote,vyama vya kiraia na Makanisa yote kubaki karibu na watu katika hali hii ngumu,lakini pia kuongeza bidii kama hizo katika kukabiliana na matatizo ya tabianchi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mbele ya ukubwa na uzito wa hali hii la janga kutokana na virusi vya corona vinavyozidi kusambaratika kila kona ya sayari, Lutheran World Federation yaani Shirikisho la Kiluteri Duniani linawaalika serikali zote, vyama vya kiraia na Makanisa yote ili kubaki karibu na watu katika hali hii ngumu na watu walioshambuliwa na mgogoro huu. Wakati huo huo, ni muhimu kuweka bidii ya kuongeza matarajio yetu ya kukabiliana na shida ya tabia nchi. Ushauri huu umetoka na  Elena Cedillo, mkuu wa mpango wa haki za hali ya hewa wa Shirikisho la Kiluteri Ulimwenguni ambaye anatazama ni kwa jinsi gani maeneo mengi ya janga lililotangulia kwa kipindi kirefu cha ukame. Kwa maana hiyo  anauliza swali, hawa hawakuwa na maji ya kutosha, je  watawezaje kushinda shida hii mpya?

Janga hili liko linaaathiri kila mtu, bila kujali hali ya kijamii, umri au jinsia, amesema hayao Pranita Biswasi, wa mpango wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni kwa ajili ya vijana, akiamini kwamba mgogoro wa hali ya hewa unapaswa kushughulikiwa kwa njia ile ile ya pamoja. “Tunategemea sayansi  katika kuthibiti virusi, kwa maana hiyo tusisahau ripoti ya Kikundi cha Serikali kuhusu  Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC),ambayo inategemea matokeo ya kisayansi”. Wakati nchi zinajiandaa kujumudu kiuchumi, kuna hata fursa nzuri ya kujumuisha hatua za matendo ya dhati kwa ajili ya hali ya hewa na kupata fedha kwa ajili ya  mipango ya hali ya hewa, amasisitizae. Siku chache zilizopita, kama inavyojulikana, Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba Mkutano wa 26 kuhusu hali ya hewa (COP26) uliahirishwa  kwa kipindi kisichojulikana kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Baraza hili lilikuwa lifanyike huko Glasgow, Uingereza mwezi Novemba mwaka huu. Zaidi ya hayo, mikutano ya mashirika wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabianchi, kwa kile kiitwacho ‘mazungumzo ya Bonn’, yameahirishwa hadi tarehe 4 mpaka 14 Oktoba. Mikutano kabla ya kikao hicho  itafanyika kuanzia tarehe 28 Septemba hadi 3 Oktoba 2020. Mada mbili kuu zinazo tarajiwa kuwekwa katika meza ya wataalam ni uchunguzi wa suluhisho za nishati “off-grid”,ambayo ni mifumo yenye uwezo wa kutoa umeme safi wakati wa kukosa mtandao wa usambazaji na utumiaji wa maji katika muktahda wa chakula na kilimo. Nchini Italia tukio la Vijana kwa ajili ta tabianchi, ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa utapangwa tena wakati wake.

Kuahirishwa kwa mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa kuhusu  hali ya hewa, Cedillo anaamini, kuwa haipaswi kuwa sababu ya kupunguza ahadi au juhudi za kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.  Baada ya matokeo ya Cop25 huko Madrid, matarajio ya Cop26 ni ya juu, kama anaoonyesha Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni, likikumbusha kwamba serikali zote ulimwenguni zinapaswa kuongeza malengo yao ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafusi ili kupunguza joto ulimwenguni hadi kufikia nyuzi joto 1.5 ° na uzuie athari mbaya zaidi isiyokuwa ya kawaida kwa  maskini zaidi na walio katika mazingira magumu zaidi. Kurudiwa kwa mikutano hiyo unatazamia kuhakikisha ujumuishwaji na ushiriki wa wote kwa kila ngazi ikiwemo kizazi cha vijana kwana hakuna yoyote achwe nyuma kwa mujibu wa Shirikisho la Kiluteri Ulimwengungu. Limekumbusha katika tukio kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi zilizoandaliwa na Umoja wa Mataifa na uwakilishi wa vijana tangu 2011, hata wakati COP17 ilipofanyika jijini Durban, Afrika Kusini walishiriki.

23 April 2020, 12:57