Tafuta

Vatican News
Maaskofu nchini Ujerumani, wametuma ujumbe wao kwa Jumuiya ya Kiislamu inayoishi Ujerumani kuwatakia mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Maaskofu nchini Ujerumani, wametuma ujumbe wao kwa Jumuiya ya Kiislamu inayoishi Ujerumani kuwatakia mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.  (2020 Getty Images)

Ujerumani:Ujumbe wa Maaskofu kwa Jumuiya ya waislamu

Katika fursa ya kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa waislamu Baraza la Maaskofu Nchini Ujerumani wameandika ujumbe wao kwa jumuiya za kiislamu zinazoishi nchini humo kuwatakia matashi mema na ili wabaki wameungana pamoja kupinga kila aina ya vurugu na uhasama.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika fursa ya kuanza Mwezi mtukufu wa wa Ramadhani kwa Waislamu ambao Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ujerumani Georg Bätzing, ameandika barua kwa niaba ya baraza zima ili kuwatakia matashi mema jumuiya nzima ya kiislamu inayoishi nchini Ujerumani. Ujumbe wake umetangazwa katika tovuti ya Baraza la Maaskofu nchini humo. Katika ujumbe huo askofu anaonyesha kusikitishwa kwake kuhusu vizuizi ambavyo bado vipo vya kisheria juu ya  mikusanyiko kutokana na janga la virusi vya corona vinavyotishia dunia.

Askofu anandika: “ Kwa wakristo, vizuizi vya maambukizi ya corona, vimesababaisha uchungu mkubwa sana hata  kuacha kuadhimisha kwa pamoja Siku kuu ya Pasaka. Na sasa kwa upande wa ndugu waislamu watatakiwa kukabiliana na hali halisi isiyo julikana inaisha lini na ngumu wakati huu wa kipindi chao cha mfungo wa Ramadhani”.

Katika ujumbe wake pia amependelea kukumbusha juu ya muhimu wa maeneo ya misikiti, masinagogi na makanisa katika maisha ya kiroho. Amefafanua kuwa “Ni maeneno ya kufanyia ibada na tafakari binafsi, lakini pia hata nafasi za kuungana kijumuiya katika kumwelekea Mungu na kusali na vile vile  kama kumbi za kuunganika pamoja. Katika kipindi hiki ambacho kimekuwa tofauti ya ukawaida, askofu anabainisha kwamba kimefanya kutambua ni kitu gani kilicho muhimu na kile ambacho siyo muhimu. Kwa maana hiyo anaongeza:“bila mahali pa ibada, maisha ya kidini ya Waislamu, Wayahudi na Wakristo ni tofauti, kwa sababu mkusanyiko wa waamini ni jambo kuu katika dini zetu”.

Rais wa Baraza la Maaskofu aidha amekabiliana pia na tatizo la madhara yanayokumba maisha ya kidini kutokana na mashabulizi na uhasama.  Kufuatana na hili anaandika kwamba,“Misikiti, masinagogi na makanisa yamekuwa ni malengo ya ugaidi ulimwenguni kote pia huko Ujerumani,wanamgambo na wabaguzi wamekuwa wakishambulia maeneo ya ibada na kueneza woga na hofu huku wakidhoofisha namna ya kuishi  kwa amani ya waamini wa dini tofauti”.

Kwa maana hiyo “Mshikamano wetu unawaendea waathirika wa dhuluma hizi na familia zao. Lazima tuunganishe nguvu zetu kulaani na kukemea vitendo hivi vya ukatili na uovu, zaidi kukataa kila aina vitendo vibaya visivyo vya kihalali dhidi ya dini yoyote. Wakristo na Waislamu wanaamini kuwa Mungu yuko karibu nasi na tunaweza kutumaini msaada wake”. Amehitimisha ujumbe wake.

25 April 2020, 09:31