Tafuta

Siku ya Alhamisi Kuu ambayo inakumbusha Karamu Kuu ya Yesu na Mitume wake,Kardinali Vincent Nichols,Askofu Mkuu wa Jiji la Westminster na Walles nchini Uingereza anawaalika waamini kusali kwa ajili ya makuhani. Siku ya Alhamisi Kuu ambayo inakumbusha Karamu Kuu ya Yesu na Mitume wake,Kardinali Vincent Nichols,Askofu Mkuu wa Jiji la Westminster na Walles nchini Uingereza anawaalika waamini kusali kwa ajili ya makuhani. 

Uingereza#coronavirus:wito wa Kad.Nichols:Wiki Kuu kusali kwa ajili ya makuhani!

Kardinali Vincent Nichols,Askofu Mkuu wa Jiji la Westminster na Walles nchini Uingereza ametoa mwaliko wa kusali kwa ajili ya makuhani hasa siku Alhamisi Kuu Takatifu ambayo imetolewa kwa ajili yao ili waweze kutenda wajibu wao kwa uaminifu na ukarimu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wito wa kusali kwa ajili ya makuhani, ni ujumbe uliotolewa na Kardinali Vincent Nichols, Askofu Mkuu wa Jiji la Westminster na Mkuu wa Kanisa la Uingereza na Walles katika Wiki hii Kuu Takatifu na zaidi katika Alhamaisi Kuu. Kupitia katika Tovuti ya Baraza la Maaskofu wa Uingereza, kwa namna ya pekee, Kardinali anawashauri kukumbuka kwa dhati katika sala zao, Makleri wote katika maadhimisho ya Alhamis Kuu, siku ambayo kiutamaduni, imetolewa kwa ajili yao na ambapo ni siku muhimu kwa kawaida ikiadhimishwa misa mbili, ya kwanza ni muktadha wa kubariki mafuta ya Krisma na misa nyingine ni “Missa in Coena Domini” yaani misa ya Karamu Kuu ya mwisho ambayo inakumbusha meza kuu ya mwisho Yesu akiwa na mitume wake ambayo inafafanuliwa kuwekwa kwa Ekaristi Takatifu.

Wakati wa maombi, waombee makuhani

Mwaka huu Kardinali   Nichols amebainisha “hatuadhimishi Misa ya Krisma”. Kwa sababu ya dharura ya virusi vya covidi-19, maadhimisho haya yanaweza kupangwa  katika tarehe nyingine kaka ilivyoelekeza Hati Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa iliyotangazwa tarehe 25 Machi 2020. Misa ya Karamu Kuu ya Bwana itaadhimishwa bila kuwa na sehemu ya ibada ya kuosha miguu na itafuata mara moja kipindi cha maombi . Kwa njia hiyo katika kipindi hiki cha sala mbele ya Ekaristi Takatifu, Askofu Mkuu wa Westminster ameeleza kuwa wanaomba makuhani wapyaishe ahadi zao, ahadi walizofanya wakati wamapewa daraja takatifu la upadre kwa namna ya binafsi na ibada ya kina.

Makuhani wanatoa maisha yao kwa Bwana

Kadhalika Askofu Mkuu anawashauri waamini wote kwa kutumia muda huo wa Missa Coena Domini’ kuwaweka mapadre wote katika sala zao. Wao wanatoa maisha yao kwa Bwana katika huduma yao. Ameandika na kuongeza “Ninaomba tafadhali katika Juma Kuu hili Takatifu kusali kwa ajili yao ili waweze kuwa waaminifu na wakarimu, na kama ilivyo kwa makuhani wanasali kwa ajili yenu”.

Maombi ya pamoja yanapelekwa na Yesu mbele ya baba yake na baba yetu

Kardinali Nichols ameadika “Sala ya hii ya maombi inatuunganishwa kwa Yesu , kwani Yeye pia anomba kwa ajili yetu bila kuanza mbele a Baba yake. Kwa maana tunaposali kuombea mmoja na mwingine, maombi yetu yanapelekwa na Yesu mbele ya Bwana, Mungu wetu wa upendo. Salini kwa ajili ya makuhani wenu na wao pia wanasali kwa ajili yenu”. Tafadhali msisahau kusali hata kwa ajili yangu” amehitimisha Mkuu wa Kanisa la Uingereza na Walles.

 

09 April 2020, 10:53