Tafuta

RWANDA:Maaskofu nwanahimiza makuhani kuwa karibu na watu wao na watu wa Mungu kufuata maelekezo ya Mamlaka na na ya Kanisa katika kukabiliana na janga la covid-19 RWANDA:Maaskofu nwanahimiza makuhani kuwa karibu na watu wao na watu wa Mungu kufuata maelekezo ya Mamlaka na na ya Kanisa katika kukabiliana na janga la covid-19 

RWANDA#coronavirus:Baraza la Maaskofu wahamasisha makuhani kuwa karibu na waamini!

Ni lazima kabisa kuwa na bidii katika Kristo ambaye ni Njia,Ukweli na Maisha kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Rwanda katika ujumbe wa kipindi hiki kigumu cha usambaaji wa virusi vya covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican News

Katika Kipindi hiki cha janga la virusi vya COVID-19, Baraza la Maaskofu katoliki nchini Rwanda wametoa ujumbe wao  wakikumbusha makuhani wote  kuwa utume wao unajikita katika nyanja kuu tatu za huduma kuchungaji ambayo ni kufundisha, kutakatifuza na kuongoza watu wa Mungu na kwa maana hiyo li lazima kuwa na jitihada katika Kristo ambaye ni Njia, Ukweli na Maisha.

Shukrani kwa makuhani kwa ajili ya maadhimisho ya Misa kila siku

Vile vile Maaskofu wa Rwanda awanatoa shukrani kwa mahuhani kutokana na kuendelea kuadhimisha ibada za misa ambazo zimewezesha waamini kufuatilia  moja kwa moja kwa njia mpya za kiteknolojia, jambo ambalo linachangia kukuza ule muungano wa kiroho na kuwahimiza wabaki karibu na waamini wao.  Maaskofu wanasema : “Roho wa Mungu aonyeshe njia ya kupitia ili wema uweze kushinda ubaya, matumaini yashinde hofu na upendo wa Kristo uweze kutawala daima zaidi ulimwenguni.

Wito kwa waamini wawe na uvumillivu

Kwa upande wa waamini,  watu wa Mungu, maaskofu wa Rwanda wanatoa mwito wa kuwa na uvumilivu katika sala bila kuchoka ndani ya familia na kwa njia ya vyombo vya mawasiliano  ili wasijiachie kushindwa na hofu. “Katika kipindi hiki cha majaribu, Mungu aweze kuwasaidia watu wote kupyaisha uhusiano wetu na Mungu na kuzidisha zaidi uhusiano wa karibu na umoja kati yetu, na wanaongeza katika ujumbe wao kuwa- “ kaeni na utulivu kwani Mungu yuko karibu na anataka kutuokoa.”

Madakatari wanatenda kazi ya Mungu na ya ubinadamu

Baraka kwa namna ya pekee  ya maaskofu wa Rwanda imewaendea madaktari, wahudumu wote wa afya na wale wote ambao wanajikita katika mapambano dhidi ya covid-19 na ambao pia wamewapongeza kwa kazi kubwa wanayoitenda na kwamba “kuweni na uhakika ya kuwa tunawasindikiza katika kazi ngumu mnayoifanya ya kutoa huduma ya Mungu na ubinadamu”.

Kufuata maelekezo ya Mamlaka na Baraza la Kipapa la ibada na Nidhamu ya Sakramenti

Katika ujumbe wao Maaskofu wanaelekeza hata waamini namna ya kuadhimisha siku kuu tatu za Wiki kuu, ambazo zinakaribia  kwa kuzungatia kanuni na hatua zilizotolewa na Mamlaka ya raia katika harakati za  kuzuia maambukizi ya corona na kwa mujibu wa amaelekezo ya Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti. Maaskofu wanabanisha kuwa: “Awali ya yote Luninga na radio vitasaidia kufuatilia maadhimisho yote ya Alhamisi Kuu, Ijumaa Kuu, Jumamosi Kuu na Pasaka: Baraza la Maaskofu na majimbo yote watatumia pia zana zote za kiteknolojia zilizopo ili kuwasaidia watu wa Mungu  kusali katika jumuiya zao, familia na binafsi. Hatimaye Baraza la Maaskofu nchini Rwanda wametoa sala ya kuomba Mungu ulinzi na uponyeshaji wa virusi vya corona:

Ee Mungu Mwenyezi Baba wa Huruma, Wewe unayeonyesha upendo kwa kila kiumbe, utuhurumie na kusikiliza maombi yetu ambayo tunakutolea kwa ajili ya wale waliombukizwa na janga la virusi vya corona katika kila pemebe ya dunia. Tunakusujudia mbele yako na kukuomba kwa sababu Wewe unaweza kutusaidia kusimamisha kusambaa kwa haraka janga hili. Kwa sasabu wewe unaweza kuponyesha wote walio ambukizwa. Uwapokee katika Ufalme wako wote waliokufa ,na uwape nguvu familia zao. Tunakuomba tena kwa sababu inawezekana kabisa kupata tiba ya ugonjwa huu. Na ili viogozi wa nchi na wataalamu wa afya ya umma waweze kuchukua uamuzi wa busara ambao unaokoa maisha ya watu. Tunakuomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

 

02 April 2020, 15:43