Tafuta

Vatican News
Kipindi cha corona hakuna mipaka ya dini zote.Tunaweza kusali kwa pamoja kuomba Mungu aweze kutuhurumia na janga hili. Kipindi cha corona hakuna mipaka ya dini zote.Tunaweza kusali kwa pamoja kuomba Mungu aweze kutuhurumia na janga hili.  (AFP or licensors)

Religions for peace,Onaiyekan:mbele ya Covid-19,hakuna mipaka!

Viongozi wawakilishi wa tamaduni nyingi za dini wameunga mkono suala kuanzisha roho ya dini ya amani.Ni katika muktadha kusali kwa njia ya moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii kuomba Bwana aweze kusitisha janga la corona.Katika mahojiano na Kardinali John Olorunfemi Onaiyekan, amesema suala kama la janga hili, mipaka yote ya kidini imefutwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kipindi cha kiroho, cha ubinadamu wa kushirikishana katika kulinda afya ,huruma na nguvu katika dharura ya virusi vya corona duniani kote , ndiyo kimepewa kipaumbele kwa  siku ya Jumatano Mosi Aprili 2020 kwa Chama cha Kimataifa cha kidini ambacho kimeyoa mwaliko wa pamoja kwa jina la "dini kwa ajili ya amani" ambacho kinahesabu wanachama wake zaidi ya 900 wanaowakilisha  tamaduni tofauti za kidini.

Hlii ni tukio ambalo limefanyika kuanzia saa tisa alasiri kwa viongozi wakristo, waisal , wayahudi , wabudha na wajumbe wengine vingozi kwa kuungana kila mmoja nyumbani kwake, kwa njia ya tovuti yao: www.rfp.org, kwa  kuunganisha na mija kama vile Lima, New York,, London, Beirut, Tokyo na nyingine nyingi.

Wawakilishi wa Jumuiya katoliki ni Kardinali John Olorunfemi Onaiyekan, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Abuja, Nigeria, Rais mtunukiwa wa Chama cha Dini kwa ajili ya amani. Kati ya washiriki  wengine pia ni kiongozi mkuu Emmanuel mkuu  mji wa  Ufaransa, mwakilishi wa Upatriaki wa Kiekumene wa Costantinopoli, sheikh Shaban Ramadhan Mubaje, Kiongozi Mkuu wa Uganda, Kiongozi Mkuu wa Kiyahudi David Rosen, Mkurugenzi wa kimataifa wa Masuala ya Kidini  wa Kamati  ya Kiyahudi  wa Marekani, Kosho Niwano. Na mwenyekiti aliyechaguliwa wa Rissho Kosei-kai.

Kwa pamoja wameongoza waamini wote duniani na watu wenye mapenzi mema kuomba Mungu ili janga la virusi vya corona liishe. Kabla ya tukio hili kufanyika, vatican news imehojiana na Kardinali Onaiyekan ambaye amezungumzia juu ya kuanzishwa kwa chama hiki cha  dini kwa ajili ya amani  (Religions for peace) kama fursa ya kuonesha kuwa mbele ya dharura kama ya Covid-19 “mipaka yote kati ya dini imefutwa”.

Kardinali amesema kuwa ni kwa miaka mingi sasa kwa kufuata ushauri  wa Papa Francisko ambao mara kwa mara anasisitiza kukaa pamoja na ili kukuabiliana na matatizo ambayo yanaikumba dunia. Kwa bahati mbaya anasema virusi vya corona  vimefikisha ujumbe wake ambao umekuja moja kwa moja na wazi ya kwamba hakuna hata mmoja anaweza kuwa na sintofahamu.

Mipaka yote kati ya makundi yote ya dini imefunguliwa, anasema Kardinali . Haiwezekana kubaki na sintofahamu. Hii haihusu tu wakristo, waislam wabudha, wahindu na wala wanageria, waitaliano, au waspanyola, weusi au weupe, ubinadamu wote kwa sasa huko katika mtumbwi mmoja na mawimbi makali ya dhoruba ambyo ni virusi vya corona. Kwa kufuata mwaliko wa Papa Francisko  wa kipindi cha sala kwa viongozi wote wa dini duniani na kama ilivyo  jitokeza Ijumaa iliyopita, kuanzishwa kwa suala la dini ya amani, inajionesha katika kipindi muafaka na kwa kufuata kweli nyayo za Papa Francisko.Kwa upande wao, Kardinali amesema wanasali kwa Bwana ambaye ni Mungu wa wote  ili aweze kutuhurumia na janga hili.

Kardinal Onayeikan aidha ameto mwaliko kuwa kila mmoja mahali alipo anapaswa kufungua moyo wake kwa mungu kulingana na utamaduni wake. Inatosha dakika chache tu. Ni ishara muhimu lakini yenye maana na nguvu zaidi, ambayo wakati huu tunaweza kuungana kwa pamoja kila pande ya dunia, Roma, New York  na kila mahali na kila mmoja nyumbani kwake na pia kwa neema ya teknolojia na vyombo vya kisasa  kukutana mubashara.

Kwa maoni yake kuhusu maombi ya Papa Francisko ya kila siku katika dharura hii, Kardinali amesema kwa upande wake sala hii inakumbusha ulimwengu wetu leo hii kuwa ni muhimu kuchukua hatua na tahadhari ili kufanya utafiti mpya, kufanya kazi bila kuchoka na kwa ushujaa kama wafanyakazi wote wa afya wanavyofanya. Lakini hii yote haitoshi, na siyo mbadala wa kupiga magoti mbele za Mungu, kuomba msamaha wa dhambi zetu na kuomba huruma kwa wanadamu wote na kumbe hatua hizi zinawezekana kupelekwa mbele na Papa Francisko, viongozi wa kidini na watu wote kwa ujumla.  Hili ndilo jambo muhimu kwa namna ya pekee katika nchi ya Nigeria, mahali ambapo kwa ngazi ya kibinadamu ni kidogo, anasema  Kardinali na kuongeza kusema kuwa ikiwa hatutegemei msaada wa huruma ya Mungu ni hatari ya kupoteza matumaini yote.

Na kwa mujibu wa nchi yake Rais wa Nigeria Bwana Muhammadu Buhari alitangaza vizuizi katika mji wa Lagos na Abuja kutokana na kuzuia maambukizi zaidi ya covid, 19 ambapo hadi sasa wanahesabu mamia ya walioambukizwa , japokuwa mbele ya hateri kama hii hata nchini Nigeria inaanza kuwa kama nchi nyingine. Kwani wasi wasi mkubwa ni  ukosefu wa zana za kuweza kukabiliana na janga kubwa la namna hii na kwa maana hiyo amethibitisha Kardinali kwamba virusi vitakuwa na uwanja mkubwa na madhara hasa ya kufa kwa watu wengi.

Amehitimisha kwa kusema kuwa hawajuhi ni kitu gani kitatokea. Ni matumaini kwamba Mungu atatoa nguvu zaidi ili kweli watu masikini waweze kuishi, kwa maana bila Yeye hakuna lolote ambalo wanaweza kufanya. Na ikiwa itakuwa hivyo basi Pasaka ya Bwana ni matumani ya ufufuko wa wafu.

01 April 2020, 15:32