Tafuta

Vatican News
Pasaka ni siku kuu ya matumaini kwa sababu ya mpito kutoka mauti kuelekea katika maisha mapya Pasaka ni siku kuu ya matumaini kwa sababu ya mpito kutoka mauti kuelekea katika maisha mapya  (Vatican Media)

Pasaka 2020:Kard.Montenegro:tuache tushikwe mikono ili tuvuke bahari ya kutisha ya vurusi!

Katika ujumbe wa Pasaka 2020 wa Kardinali Montenegro,wa jimbo Kuu katoliki la Agrigento Italia ameshauri watu waache washikwe mkono na Mungu ili wavuke bahari ya kutisha ya vurusi.Anawaomba kuwa na imani na kuamini kuwa Mungu ni kitovu cha historia ya maisha licha ya mateso na kifo.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kutokana na kwamba tunaishi katika kipindi cha mateso, kumsema Heri ya Psaka ni matashi mema muhimu.Pasaka siyo sikukuu iliyotungwa na sisis, ni sherehe ya Mungu na kile ambacho kikitokea Mungu daima anao ujumbe  wa kuwatumia watu wake. Amesema Kardinali Francesco Montenegro, Askofu Mkuu wa Agrigento nchini Italia kwa njia ya video akiwatakia watu wa Mungu heri ya Kufufuka kwa Bwana weu Yesu Kristo, ambaye ameshinda mauti, kifo hakina nguvu tena.

Pasaka  ni siku kuu ya matumaini, ikiwa na maana ya mpito anaeleza Kardinali Montenegro. Hii ina maana kuwa inawezekana kupitia hali ya kifo, hali ya matatizo na kuingia katika hali tofauti. Lakini Bwana anatuomba kuwa na imani, na kuamini kuwa Mungu ni kitovu cha historia ya maisha yetu.

Hata hivyo Kardinali anaonya kuwa, “siyo kwamba  sisi tunahitaji Mungu  wakati tuna shida, hata kwa kipindi hiki ambacho tunasali ili atuponyeshe”, lakini pia “hata wakati janga likiisha kwa maana Mungu kammwe hatoi ahadi ya kuangaza njia nyeusi tutakazo kumbana nazo, bali hata njia zetu zenye mashimo ya giza yeye yupo ataendelea kukaa nasi karibu”.

Pasaka kwa maana hiyo ni kuacha ushikwe mkono na Mungu ili uweze kweli kupita katika bahari hii ya kutisha ya virusi na kuamini kwamba Mungu anapo kuwapo, hofu zote zinawekwa pembeni. Katika maneno ya Kardinali Montenegro, akitazama upande wa maadili anasema: “ sisi tunahisi kuwa mabwana wa kila kitu, lakini imetosha tu kuona virusi vilivyo jaribu Dunia”. Hii ina maana kuwa vile ambavyo tuliviita vyenye ‘thamani’ labda havikuwa hivyo! “Tunatakiwa kuegemea maisha , kwa kile ambacho ni msingi zaidi”. Amebainisha Kardinali Montenegro.

Hatimaye kuhusu suala la mshikamano katika siku hizi ambazo tunaishi lakini zaidi, Kardinali Montenegro anasema “ni matarajio ya kuishi namna hiyo hiyo hata baada ya janga hili kuisha”. “Ni matarajio kuwa baada ya umakini huu kwa maskini uweze kuendelezwa na zaidi. Itakuwa ni vuzuri sana ikiwa muda huu, katika familia wote wanajikuta na fuaraha ya kuwa pamoja”, amehimisha Kardinali Montenegro.

13 April 2020, 12:04