Tafuta

Bwana amefufuka Aleluya Aleluya Bwana amefufuka Aleluya Aleluya 

Pasaka 2020,Kard.Bassetti:Hata kama tumo ndani ya nyumba zetu tunathubutu kusema Bwana amefufuka!

Katika mahubiri ya maadhimisho ya Pasaka tarehe 12 Aprili 2020 Kardinali Bassetti Askofu Mkuu wa Perugia na Rais wa Baraza la Maaskofu Italia amesema pamoja na janga hili ambalo utafikiri halina mwisho,tunathubutu kutamka kwa sauti ya kina na furaha ya imani yetu:Bwana amefufuka!Amebainisha jinsi ya kuguswa na historia ya ushuhuda wa tafakari ya Njia ya msalaba Ijumaa Kuu Takatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tunajitahidi kuamini kuwa leo ni Pasaka wakati tuko tunalazimika kukaa nyumbani, mahospitali yakiwa yamejaa wagonjwa na vivuli vya kifo kwa bahati mbaya vinaendelea kutuzunguka. Pamoja na janga hili ambalo utafikiri halina mwisho, tunathubutu kutamka kwa sauti ya kina na furaha ya imani yetu: “ Bwana amefufuka. Amesema hayo Kardinali Gualtiero Bassetti, Askofu Mkuu wa Perugia mji wa Pieve na Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (Cei) katika mahubiri ya Misa ya Pasaka taehe 12 Aprili 2020, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Lorenzo wa Perugia wakati Kanisa kuu likiwa tupu, kulingana na kanuni zilizowekwa za   kipindi cha virusi ya corona au covid-19.

Hata hivyo kama ilivyo katika makanisa mengi duninia , madhimisho ya misa ya takatifu yametangazwa moja kwa moja na Luninga ya Mkoa wa Umbria, Radio  ya Umbria na katika majukwaa ya mitandao ya kijamii ya Kikanisa.  Kardinali Bassetti akiendelea na mahubiri amesema “nimeshangazwa na kuguswa sana siku ya Ijumaa Kuu kwa  ushuhuda uliosikika  katika Njia ya Msalaba iliyoongozwa na Papa Francisko”. Ikumbukwe tafakari ya Njia ya Msalaba kwa mwaka huu imeandaliwa na wafungwa wa Gareza moja la Padua nchini Italia. Kwa hakika ilikuwa n ya kusisimua.

Akiendelea kufafanua, Kardinali amesema: “Ni  historia ngapi za uchungu na mateso! Historia za maisha ya kutisha, yanayooneshwa na uwepo wa uchungu na kukumbwa kimwili na kimaadili. Lakini mwisho wake wema umetawala! “Kazi ya roho Mtakatifu ilibadilisha maisha ya watu wengi:msalaba kama alivyo andika kuhani aliyesingiziwa uliangaza maisha yake na kufungua wazi njia ya ufufuko”, amesisitiza Kardinali Bassetti.

“Ufufuka ni jamboa halisi, wengi wetu wanafanya uzoefu huo katika mchakato wa safari ya  maisha yao, amesema Kardinali na kwamba, wengi  wetu tutaishi kikamilifu katika hali halisi ya siku ya mwisho kwa Bwana”.  "Katika siku hii takatifu, hatuwezi kuacha kuinua macho yetu lakini juu ya ubinadamu unaoteseka” amebainisha Kardinali.

Umbali kimwili siyo kizingiti cha maadhimisho yetu amesema ambayo yanapaswa daima kuwa sifa kuu ya muungano na kushirikishana. Ni matashi ya heri ya Pasaka ya  Kardinali   kwamba furaha ya Bwana mfufuka iweze kuwafikia watu wote majumbani mwao mahali ambapo wamo katika familia au katika upweke wa kujitenga na zaidi “nguvu ya roho Mtakatifu iwafikie wale wote wanaotoa msaada kwa ndugu wagonjwa na wanaoteseka. Uwaangazie marehemu wote mwanga wa Bwana Mfufuka.

13 April 2020, 11:22