Tafuta

Vatican News
Baraka kutoka kwa Msimamizi wa Kitume nchini Takatifu Yerusalam Askofu Mkuu Pier Battista Pizzaballa Baraka kutoka kwa Msimamizi wa Kitume nchini Takatifu Yerusalam Askofu Mkuu Pier Battista Pizzaballa 

Nchi Takatifu:Ask.Mkuu Pizzaballa:Yesu anatualika kuvaa kitambaa cha huduma ya unyenyekevu!

Yesu anatualika kuvaa kitambaa cha huduma ya unyenyekevu na kujitoa bila kujibakiza kwa maana mawazo ya Mungu ni tofauti na mawazo yetu kwa kufiriki kuwa kuhudumia ni kupunguza hadhi yetu.Ndiyo tafakari ya Askofu Mkuu Pizzaballa wakati wa Misa ya Karamu Kuu siku ya Alhamisi Kuu tarehe 9 Aprili 2020 katika Kanisa la Kaburi Takatifu,huko Nchi Takatifu Yerusalem.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kati Misa ya Kipapa ya Karamu Kuu ya Bwana iliyoadhimisha asubuhi na mapema katika Kanisa Kuu  la Kaburi Takatifu, Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki wa Kilatino Nchi Takatifu Yerusalem, siku ya Alhamaisi Kuu tarehe 9 Sprili 2020 Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, amekumbusha tendo la Yesu la kuosha miguu mitume wake na maana yake. Katika mabhubiri yake amesema, ishara ambayo Yesu anatimiza ni ishara ya mchakato wa hatua kutoka duniani kwenda mbinguni, kutoka duniani kwenda kwa Baba, kutoka kwa kile kinachoisha kuelekea kilicho cha milele. Kwa maana hiyo ili kuonyesha njia ambayo inapelekea kwa Baba, Yesu aliwaosha miguu wafuasi wake. Askofu Mkuu Pizzaballa amebainisha kwamba kama alivyodakia Petro mbele ya ishara hiyo, yeye anakanusha na kuonesha umbali ulipo kati ya mawazo ya  Mungu na kuwaza kwetu. Sisi tunafikiria kuwa kuhudumia kunatufanya kupunguza hadhi yetu.

Huduma inafanya uzaliwe umoja na kuondokana na utumwa

Kwa upande wa Yesu siyo kuhudumia siyo hivyo, bali ni wa milele, huduma hiyo inapita kutoka duniani kwenda katika dunia ya Baba  mhudumu katika unyenyekevu ambaye anajiweka chini ya miguu ya mwingine(…) Huduma inajenga muungano, inafanya kuondokana  na utumwa wa ubinafsi na kufanya uzaliwe katika umoja wa maisha ambayo hayafi tena.  Msimamizi wa kitume aidha ameelezea katika mahubiri yake kuwa, Petro anatuonesha ni kwa jinsi gani siyo kwa bahati mbaya kufanya vibaya(…), ni jinsi gani ilivyo ngumu kukubali mahataji binafsi hasa ya utambuzi wa kuwa umependwa na Bwana, wakati Yesu anatualika kumfuata, kuvua nguo na kuziweka pembeni hasa zile za  kujitosheleza na kujidai kana kwamba unaweza kufanya kila kitu  peke yako na ili kujitambua kuwa ni wadhambi na wahitaji wa msamaha; Yesu anatuomba tuvae kitambaa  cha huduma ya unyenyekevy na wa kujitoa binafsi

Siku hizi tumeshambuliwa na kujeruhiwa uhusiano

Askofu Mkuu Pizzaballa ameendelea  na tafakari, “Katika siku hizi tumeshambuliwa na kujeruhiwa kwa kile tukipendacho sana hasa kuhusu mahusiano yetu. Unaweza kufikiria kwamba Bwana ametaka kuyaondoa mahusiano hayo na ili aweze kuturudishia mengine yaliyotakasika zaidi”; “Labda Bwana anataka kututakasa na kila ambacho tumeshikilia kwa nguvu zote, na vurugu tulizo nazo katika uhusiano wetu; Labda anataka kutuambia kwamba tunaweza kuchagua na kusaidiana au kuwa wabinafsi(…). Kutengwa na upweke wa siku hizi unaweza ukawa na fursa ya kutufundsha kwamba inawezekana kubadili njia nyingine”. Kwa mujibu wa msimamizi wa kitumekatika  nchi Takatifu, amesema kuwa katika kipindi cha ajabu na uchungu wa kufunga, tunaweza labda kuwa na utumbuzi wa wito kwa kufikiria kwa upya na kutakasa mahusiano yetu”.

Injili leo hii inatoa mwaliko wa kuwa na ujasiri

Injili ya Siku leo hii inatoa mwaliko wa kufikiria kwa ujasiri juu ya nini tunajenga leo hii katika mahusiano binafsi, kifamilia, kikanisa na kijamii. Kifo na  kila kifo hakishindi kwa uriahsi maisha, bali kinashindwa na upendo mkuu anasisitiza Askofu Mkuu Pizzaballa. Kwa maana hiyo  sisi zaidi tunaitwa katika jitihada za kujeng a dunia iliyo mpya, ambayo ikiwa na mfufuka aliye mwanzo na mwenye upendo wa bure na mtindo wake ulio huru.

Tuanze safari kwa maana tunajua njia sasa

Kwa kuhitimisha mahubiri yake, Msimamizi wa kitume Nchi Takatifu amebainisha kuwa katika maisha yetu, hatujuhi ni njia gani itatupeleka iliyoelekezwa na Yesu, lakini kwa kupokea wito wake, asema “ hata ninyi mnapaswa kunawisho miguu wengine na mwaliko wa kupendana sisi kwa sisi, “ kila kitu, kila uzoefu wa kuishi katika mtind huo utageuka kumzungukia Baba”. Kabla ya kuosha miguu, Yesu alikuwa amethibitisha kuwa hakuna yoyote ambaye angeweza kumfuata, lakini kwa kuwa alionesha namba ya kupenda, Yesu alisema: ‘Sasa mnaijua njia’. Hata sisi leo hii tuanze kwa upya safari na safari hiyo sasa tunajua njia”.

09 April 2020, 14:15