Vatican News
Katika Ujumbe wa Pasaka kutoka kwa Mapatriaki na wakuu wa makanisa nchi Takatifu Yerusalem wanathibitisha kuwa ufufuko wa Kristo ni matumaini yetu! Katika Ujumbe wa Pasaka kutoka kwa Mapatriaki na wakuu wa makanisa nchi Takatifu Yerusalem wanathibitisha kuwa ufufuko wa Kristo ni matumaini yetu! 

Nchi Takatifu:Ujumbe wa Mapatriaki na viongozi wa Makanisa:ufufuko wa Kristo ni tumaini letu!

Kwa mjibu wa Ujumbe wa Pasaka kutoka kwa mapatriaki na wakuu wa makanisa huko Nchi Takatifu,Yerusalem wanasema nguvu na neema ya ufufuko italeta matumaini,uponyeshwaji na ushindi dhidi ya janga na kila hali halisi yenye giza.

 Na Sr. Angela Rwezaula – Vatiacan

Ufufuko ni uhakika wetu, Mungu yupo pia katikati ya kifo na katika mateso  kwa namna hiyo kifo cha Kristo kinatatupatia ushindi. Ndiyo  maneno ya ujumbe wa Pasaka kutoka kwa mapatriaki na viongozi wakuu wa Makanisa huko nchi Takatifu  Yerusalemu ambao  katika ujumbe wao wanawakumbuka wale wote ambao katika mataifa ulimwenguni wako wanapambana katika nyakati hizi za dharura ya virusi vya corona.

Viongozi hawa  kumi na tatu wamesisitiza kuwa ufufuko unahimiza kipindi cha upyaisho na kuelekeza njia ya wakati ujao, mbali na kuwa na vipingamizi, ubaguzi, njaa na ukosefu wa haki. Kama waamini wa imani, wanasisitiza viongozi hawa kwamba uwajibikaji wao sasa na zaidi ni kufariji wanaoteseka, kuhakikisha ulinzi wagonjwa na kutoakwa  msaada wale ambao wanahitaji.

“Utume wetu kama wakaristo na kama binadamu”, wanasisitiza “ni kusaidiana na kuendelea kusali kwa ajili ya watu watu wote wakati wa kipindi hiki cha janga. Udhaifu wetu wa kibinadamu umeongezwa nguvu ya msalaba wa Kristo katika nguvu ya Mungu.

Kwa mjibu wa mapatriaki na wakuu wa makanisa ya Yerusalem wanasema, nguvu na neema ya ufufuko  italeta matumaini, uponyeshwaji na ushindi dhidi ya janga na kila hali halisi yenye giza.“ hakuna kitakacho zuia Habari Njema ya ufufuko isisikike Yerusalem na kila sehemu yoyote duniani, hata ikiwa mwaka huu hakuna radi Aleluya (...) Kristo amefufuka! Kweli amefufuka! Aleluya” . Wanahitimisha ujumbe wao Mapatriki na wakuu wa makanisa Nchi Takatifu Yerusalem.

11 April 2020, 15:13