Tafuta

Vatican News
Mwongozo uliotolewa na maaskofu nchini Mexico kwa makuhani una elezea mada ya uwajibikaji,sala,mshikamano, huduma na busara katika kukabiliana na janga la covid-19. Mwongozo uliotolewa na maaskofu nchini Mexico kwa makuhani una elezea mada ya uwajibikaji,sala,mshikamano, huduma na busara katika kukabiliana na janga la covid-19. 

Mexico#coronavirus:Kanisa la nchini Mexico latoa mwito wa kusaidia maskini!

Kipeo cha kiafya na kiuchumi,kimeathiri kwanza watu walio wa mwisho maskini ambao wanaishi kwa siku.Kwa muktadha huo Kanisa Katoliki nchini Mexico linatoa wito kwa wote kuwa na matendo ya dhati ya upendo.Maaskofu nchini humo pia wametoa ushauri msingi kwa mapadre katika mwongozo uliopewa jina “kuhani mbele ya changamoto kubwa Covid-19".

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kanisa Katoliki nchini Mexico limetoa wito wa dharura kwa watu wa Mungu ili wajikite katika matendo na ishara ya upendo kuwasaidia walio katika mazingira magumu na maskini, kwa sababu ya  kipeo cha kiafya iliyotokana na virusi vya corona. Katika muktadha huo  kipeo cha uchumi kimekumba sana wale ambao wanaishi kwa siku,wanaoihi barabarani hivyo masikini zaidi. Padre  José Manuel Suazo Reyes, msemaji mkuu wa Jimbo la Xalapa, amesisitiza kwamba kutokana na kuwepo karantini  ambapo watu hawaruhusiwi kutoka nje ya nyumba, uchumi unawakumba wafanyakazi wa kujitigemea  ambao wanapata chochote kutegemea na kufanya kazi kwa siku.

“Katika nyakati hizi tutafute kujikita katika kuongeza matendo ya dhati ya upendo kwa maana wapo watu wengi ambao wanaishi kwa siku na ambao kwa hakika watu hawa ni wale ambao wateseka zaidi na matokeo ya hali hii” amesisitiza Padre. Hata hivyo kwa kuongeza amebainisha kwamba kipeo hiki hakitakuwa ni cha afya peke yake lakini pia hata cha uchumi hivyo ni lazima kushirikishana, kujikita katika matendo ya hisani kuu na walio masikini na wenye kuhitaji zaidi.

Kufuatana na hali hii Caritas nchini Mexico zitaweza kutoa chakula kwa watu wenye kuhitaji, chakula kwa watu wanaoishi barabarani na madawa. Aidha Caritas Jimbo  maparokia yataendelea kutoa huduma muhimu, kama vile kutoa msaada kwa watu walio masikini zaidi, kufungua maduka ya madawa kwa ajili ya huduma msingi ya madawa kwa wanajumuiya, kwa maana wapo watu wengi kwa hakika wenye shida sana

Nchini Mexico pia ni moja ya nchi Barani Amerika ya Kusini ambayo imefuata hatua za kudhibiti dharura ya Afya ikiwa imechelewa ukilinganisha na nchi nyingine na hivyo kwa sasa maambukizi yamesambaa katika baadhi ya sehemu katika taifa. Baraza la maaskofu nchini Mexico aidha wametoa mwongozo juu ya nafasi ya kikuhani mbele ya dharura ya Covid-19. Katika mwongozo huo, unasema kila kuhani anapaswa kuwa daraja  la muungano kati ya Mungu na wanae. Siyo wakati wa kustarehe katika maisha yao kiroho na wala hakuna ruhusa ya kupunguza mtazamo kuelekeza katika hatari hii kubwa ya maambukizi.

Makuhani wajaribu kuwa makini kuwatunza wengine kama wajitunzavyo na kuwa wachungaji wema wa jumuiya nzima ya kikristo ambayo Mungu aliwakabidhi. Ndiyo ushauri msingi kutoka kwa Maaskofu wa Mexico katika mwongozo “ kuhani mbele ya changamoto kubwa Covid-19". Uwajibikaji, sala, mshikamano, huduma na busara ndivyo vichwa vya kila kipengele cha mwongozo uliotolewa na ambao unaweka chachu ya matendo ya kichungaji katika hali hii ya dharura, huku wakionesha na kufafanua baadhi ya mambo msingi ya afya katika kuzuia maambukizi.

06 April 2020, 12:32