Tafuta

2020-04-24 umeanza mwezi mtukufu wa radhamani kwa waislamu lakini katika kipindi cha virusi vya corona ambapo hawataweza kushiriki sala kikamilifu katika misikiti yao. 2020-04-24 umeanza mwezi mtukufu wa radhamani kwa waislamu lakini katika kipindi cha virusi vya corona ambapo hawataweza kushiriki sala kikamilifu katika misikiti yao. 

Mauritius #coronavirus Ujumbe wa Baraza la kidini kwa waislamu!

Baraza la kidini nchini Mauritius wametuma ujumbe wao kwa waislamu ambao kwa kipindi hiki cha janga la corona hawataweza kusali katika misikiti yao katika fursa ya mwezi wao mtukufu wa Ramadhani.Kwa waislamu,Ramadhani ni kipindi muhimu cha mwaka kwani ni muda wa kusali na kuangazia zaidi familia zao.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Waislamu katika pembe zote za dunia waliokuwa wakisubiri kuanza mwezi mtukufu  wa Ramadhani sasa umewadia japokuwa  katika kipindi ambacho kuna  maagizo tofauti katika juhudi za kupambana na virusi vya corona au covid 19  ikiwemo marufuku  ya kutoka nje na mikusanyiko ya umma. Kutokana na marufuku ya mikusanyiko, idadi ya  jamaa  katika misikiti pia ni marufuku katika mataifa tofauti kwa lengo la kuepuka maambukizi zaidi ya Covid-19. Kuanzia Nchini Saudia,kuingia na kutoka katika jiji la Makka na Madina imepigwa marufuku. Hija ndogo ndogo zimesitishwa pia kutokana na janga a virusi vya corona. Kwa ujumla ni Mataifa tofauti ikiwemo ya Mashariki ya Kati hata chini Uturuki mikusanyiko ya umma kwa ajili ya ibada na iftar vimepigwa marufuku!

Kufutia na janga hili basi  hata Baraza la Kidini katika Kisiwa cha Mauritius kinaelezea mshikamano wake kwa Waislamu wote ambao wameanza mwezi Mtukufu wa Ramadhani licha ya vizuizi vilivyopo ili waweze kuishi vema mwezi huu mtukufu wa kiislamu. Haya yanasomeka kutoka katika ujumbe wa Rais wa Baraza la Dini,Philippe Goupille,amnaye anawaalika, kama ilivyopendekezwa na maimamu wao, kuimarisha uhusiano wa kifamilia na kuishi Ramadhani hasa katika mwelekeo wa kifamilia.

Katika ujumbe wake ameandika kuwa usomaji wa Korani na sala za kila siku ambazo haziwezi kufanyika katika misikiti na pia  itakuwa muhimu kutoa sadaka kwa upendo wa wote, ndivyo viwe kpaumbele. Kiukweli ni nafasi nzuri ya kuweza kupyaisha uhusiano wa kifamilia na kujikita kwa kina katika mazungumzo na vijana na watoto, ameandika, huku akikumbuka kwamba hata Wakatoliki mwishoni mwa kipindi cha toba cha Kwaresima hawakuweza kusherehekea kama kawaida ya tukio hili kubwa na zaidi hawakuweza kukusanyika kwa pamoja katika makanisa kwa ajili ya  sikukuu kubwa ya Pasaka.

Kadhalika Philippe Goupille katika ujumbe huo ameandika kwamba wanaungana na dini nyingine kubwa kwa njia mpya ya kufanya kwaresma. Pia ni fursa ya kujisikia karibu na dini nyingine, ili kuishi hatima hiyo kama jamuiya na kushiriki uzoefu huu mpya ambao umewekwa kwa ajili ya wema wa raia katika kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona. Katika umoja pamoja nao watasali kwa namna ya pekee ili Mungu aokoa kisiwa cha Mauritius na kuwasindikiza katika kuzindua kwa upya maisha yao ya kijamii na kiuchumi, anaihitimisha ujumbe huo.

24 April 2020, 12:03