Vatican News
Akili bandia  ambayo kwa ujumla imeanza kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta nyingi sana duniani lakini licha  ya hayo yote inatakiwa iwe uwazi na kufafanuliwa kwa watengenezaji wake Akili bandia ambayo kwa ujumla imeanza kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta nyingi sana duniani lakini licha ya hayo yote inatakiwa iwe uwazi na kufafanuliwa kwa watengenezaji wake  

LA CIVILTA’ CATTOLICA:Njia za kimaadili na majadiliano zitumike katika mfumo wa Akili bandia!

Padre Casalone katika Gazeti la CIVILTA' CATTOLICA katika makala ya jina“utafiti wa kushirikisha katika nyakati za kidigitali”anaweka wazi juu ya muktadha wa Akili bandia (IA) katika maadili kulingana na sahihi ya Februari 28 kwa mujibu wa viongozi wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha;Rais wa Microsoft,Ibm,Marekani,FAO na Waziri wa Italia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kutoa maelezo zaidi ili kuweza kutumia njia kimaadili katika mantiki ya Akili bandia  (IA)  ndiyo Madhumuni ya wito wa Maadili uliyosainiwa tarehe 28 Februari iliyopita, wakati wa kuhitimisha mkutano wa Taaasisi ya Kipapa ya Maisha  (Pav)na Rais wake Askofu Vincenzo Paglia; Rais wa  Microsoft, Bradford Lee Smith; Makamu Rais mtendaji  wa Marekani Ibm, John Kelly III;  Mkurugenzi  mkuu wa Fao, Qu Dongyu pamoja na Waziri wa Italia kwa ajili ya ubunifu wa kiteknolojia na kidigitali  Bi. Paola Pisano.

Kwa kujikita kutazama wito huo Padre Casalone  katika mada yake ameweza kujitikita awali ya yote juu ya hotuba ya Papa Francisko aliyoitoa kwa washiriki wa Mkutano wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha (PAV) wakati wa fursa ya maadhimisho ya miaka 25 ya Taasisi hiyo. Kwa muktadha huo makala yake inatazama mada mbili kuhusu matumizi ya Robot na ile ya Akili Bandia (IA). Katika hotuba ya Papa Francisko wakati fursa hiyo alionesha wazi baadhi ya misingi mikuu kuhusiana na masuala ya maadili ya dunia ya kidigitali akikazia juu ya kuepukana na itikadi za kisasa.

Jumuiya ya kibidanamu inahitaji kukua na utambuzi wa uumbaji na upendo wa Mungu

Tafakari ya Papa Francisko  wakati wa fursa ya maadhimisho ya miaka ishirini na tano  alianza kutazama jumuiya ya kibinadamu, kuwa inahitaji kukua kwa utambuzi wa pamoja juu ya uumbaji na upendo wa Mungu. Katika nyakati zetu, Kanisa linaitwa kutoa nguvu mpya ya ubinadamu wa maisha ambayo yanataka kuvunja shauku hii ya Mungu kwa ajili ya kiumbe chake. Juhudi mpya ni za kufuata, kuhamasisha na kulinda maisha ya kila kiumbe inayochukua hatua hiyo ya upendo upeo wa Mungu. Ni uzuri na uvutio wa Injili ambayo haiwezi kupunguzwa kamwe upendo wa jirani na kuuweka katika mantiki za kiuchumi na kisiasa  hata katika baadhi ya mkazo wa mafundisho au maadili ambayo yanafuata aina fulani ya kiitikadi.

Papa Francisko alisema ni lazima tupinge aina hizi za kiitikadi zinazojitokeza na kupata hata msaada wa soko na teknolojia kwa ajili ya ubinadamu. Utofauti katika maisha ya mwanadamu ni mzuri kabisa na ambao anastahili kufuatwa kimaadili, kwa ajili ya thamani ya kuhudumia viumbe vyote. Kashfa iliyopo kiukweli ni kwamba, ubinadamu hunapingana wenyewe, badala ya kuwa na msukumo kutokana na tendo la upendo wa Mungu.

Akili Bandia lazima ieleweke na kuwa wazi kwa wote

Katika Gazeti la La Civiltà Cattolica toleo la  4074 l ambalo limetolewa tarehe 4 Aprili 2020 Padre Carlo Casalone amezungumzia kwa kirefu huku akikazia misingi mikuu ya mantiki ya mifumo ya kiteknolijia  ya Akili bandia  ambayo kwa ujumla imeanza kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta nyingi sana duniani. Lakini licha  ya hayo yote  Padre Casaloni anasema awali ya yote inatakiwa “uwazi”.  Hii ina maana kwamba kimsingi Padre ansema mifumo ya akili bandia lazima ieleweke na hivyo inapaswa iweze kufafanulia na hivyo natakiwa iwe inayounganisha. Mahitaji ya wanadamu wote lazima yazingatiwe kwa njia ambayo kila mtu anaweza kufaidika nayo na watu wote kupewa hali bora za kufafanuliwa na kuendelezwa.

Waundaji na watengenezaji lazima wasibague

Pamoja na kufafanuliwa vema lazima iwajibike. Na hii inahusu kwa wale ambao hutengeneza na kutekeleza teknolojia hizi lazima waziendelee na uwajibikaji na uwazi. Suala jingine muhimu linatazama kutokuwa na usawa. Katika kufafanua hili anasema Padre Casalone , Akili Bandia ni lazima iepukwe kuundwa au kutenda kulingana na ubaguzi na hivyo itengenezwe kwa kulinda usawa wa binadamu na heshima. Na tena, amegusia juu ya kuamini.  Mifumo ya  Akili bandia (AI) lazima iweze kufanya kazi kwa uaminifu. Usalama na kufauata ufaragha: Mifumo ya Akili Bandia  AI lazima ifanye kazi kwa njia ambayo watumiaji wanalindwa na kuheshimiwa katika faragha yao.

Tafakari ya maadili wakati mwingine inakasirishwa

Padre Casalone aidha amebainisha kuwa misingi hii iendane pamoja na hati zilizofanyikwa kazi na mashirikia mbalimbali ya Umoja wa Ulaya kwani haikuwa dhahiri kwamba  wanaweza kushirikishana pia na makampuni makubwa nchini Marekani ambayo walisifu uhalali wao katika muktadha tofauti. Kwa mujibu wa Padre Casalone  “tafakari ya maadili” inakasirishwa na wale wanaofanya kazi kwenye uwanja huo na wako katikati ya michakato ya mabadiliko ya nidhamu zao, kwani  wakati walikuwa ni  wa kimaumbilie na madaktari na sasa wako katika nyakati za (data)takwimu  na wanasayansi wa kompyuta.

Teknolojia na habari havitofautiani

Kutokana na muktadha huu ndipo Padre Casalone anasema kuna umuhimu wa kuwa na  maadili ya kiteknolojia na kidigitali, ambayo yanapendekezwa iwe ya maadili, kama ilivyo ya teknolojia na habari  ambavyo kwa dhati havitofautiani, lakini vimeunganishwa kwa karibu sana. Biolojia inaweza kuingia katika mazungumzo na umoja na maadili kwa algorithms na kama kutengeneza daraja jipya la wakati ujao.

04 April 2020, 10:22