Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Kenya wametoa tangazo kuhusu Televisheni ya Ukweli Katoliki kwa ajili ya kuonesha matumaini katika kipindi cha virusi vya corona.Televisheni hiyo imezinduliwa siku ya kwanza ya mwezi Aprili. Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Kenya wametoa tangazo kuhusu Televisheni ya Ukweli Katoliki kwa ajili ya kuonesha matumaini katika kipindi cha virusi vya corona.Televisheni hiyo imezinduliwa siku ya kwanza ya mwezi Aprili. 

Kenya#coronavirus:Baraza la Maaskofu watangaza Televisheni ya Ukweli katoliki!

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Kenya wametoa tangazo kuhusu Televisheni ya Ukweli Katoliki kwa ajili ya kuonesha matumaini katika kipindi cha virusi vya corona.Televisheni hiyo imezinduliwa siku ya kwanza ya mwezi Aprili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Inaitwa “ Ukweli Catholic Television” yaani Televisheni ya ukweli katoliki, ambacho kwa sasa ni chombo kipya cha televisheni cha Baraza la Maaskofu nchini Kenya (Kccb) na uwezekano wa kupitia jukwaa nyingine za YouTube na Facebook. Hilo ndilo jina ambalo linachukua maana yake kwa sababu ya ukweli katika lugha ya kiswahili. Kwa mujibu wa habari kutoka tovuti ya Shirikisho la Mabaza ya Maaskofu wa Afrika mashariki (AMECEA), wamesema kuwa uzinduzi wa chomo hicho umefanyika siku ya kwanza ya mwezi Aprili 2020  katika makao makuu ya “Radio Waumini” huko Kasarani, Nairobi.  Aliyeongoza tukio hili ni mhusika wa Tume ya mawasiliano ya kijamii ya Baraza la Maaskofu Kenya Kccb) Askofu Joseph Obanyi, ambaye katika fursa hiyo ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu iliyoonyeshwa moja kwa moja.

Katika mahubiri yake, Askofu amesisitiza namna gani ya kukabiliana na janga ambalo limetokana na maambukizi ya virusi vya corona hivyo chombo kipya cha televisheni kinataka kujibu kwa njia ya kutoa ujumbe wa matumaini kwa mujibu wa mafundisho ya Injili.”Nia yetu ni ile ya kutangaza Habari Nje hadi miisho ya dunia”, amesema askofu  Obanyi.

Televisheni ya Ukweli hata hivyo nyuma yake ina historia ndefu kuanzia na Ukweli Video Productions (Uvp), iliyoanzishwa tarehe 18 Mei 1981 Mmisionari wa Mapadre wa Shirika la Maryknoll, Padre Richard J. Quinn. Hiki ni kutuo kimoja wapo cha kwanza cha uzalishaji wa video kitaalam, chenye tabia ya kikristo barani Afrika na kikiwa na nia ya kuinjilisha katika bara kwa njia ya picha. Kadili ya miaka ilivyokwenda UVP imeweza kuzunguka na kutengeneza picha zaidi ya 290 , kazi za kisanaa na maonyesho, ambayo karibi 60 ni yenye tabia ya kichungaji.

Picha hizo zimeandaliwa kutoka nchini Kenya, Sudan, Tanzania, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi na Zimbabwe. Baadhi ya vipindi vilionyehwa hata na Luninga ya Taifa ya Kenya KBC,  na televisheni nyingine za kimataifa. Kunako mwaka 2008 Padre Quinn alistaafu na kwa sasa ni marehemu. Baraza la Maaskofu kwa maana hiyo waliomba Mkurugenzi mpya, Suor Lucy Lando, kubadilisha kituo hicho cha uzalishaji kuwa kituo cha televisheni hivyo hatua hiyo imetimizwa na shukrano kutoka kwa wasaidizi na wahudumu wa vyombo katoliki vya habari nchini Kenya na idadi kubwa ya walei.

04 April 2020, 14:11