Tafuta

Vatican News
Chini ya miguu ya msalaba wa Yesu alikuwapo Maria mama yake Chini ya miguu ya msalaba wa Yesu alikuwapo Maria mama yake 

Italia:Ujumbe wa kiekuemene kwa ajili Pasaka:Msiogope!

Katika ujumbe wa Pasaka kutoka kwa viongozi wa shirikisho la makanisa ya kiinjili Italia,Tume ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI) kwa ajili ya Uekumene na Majadiliano ya kidini na Askofu Mkuu Gennadios, wa Kiorthodox nchini d’Italia na Malta wanahisi kuwa kama wanawake wa kwanza kutangaza ufufuko wa Bwana na pia kuhimiza waamini wasiwe na hofu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tukiwa tunakaribia Pasaka ya Ufufuko wa Bwana,katika Makanisa yetu yataadhimisha tarehe tofauti  ya kwanza 12 Aprili katika utamaduni wa nchi ya Magharibi na ile ya tarehe 19 Apili makanisa ya Mashariki, na katika misingi ya udugu ambao unakiri Bwana mmoja, tumahisi uhitaji wa kurudia kutoa neno la pamoja mbele ya  janga hili lililoikumbaTaifa na ulimwengu mzima. Ndivyo unaanza ujumbe wa Pasaka ambao Mchungaji Luca Maria Negro, Rais wa Shirikisho la Makanisa ya kiinjili nchini Italia (FCEI), Askofu  Ambrogio Spreafico, wa Jimbo Katoliki  Frosinone na Rais wa Tume ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI) kwa ajili ya Uekumene na Majadiliano ya kidini na Askofu Mkuu Gennadios, wa Kiorthodox nchini d’Italia na Malta (Patriaki wa Kiekumene wa Costantinopoli) wamependelea kuwaandikia waamini wakristo nchini Italia.

Katika ujumbe wao,amebainisha kuwa, mara moja kwa mwaka kama viongozi wa dini  ya kikristo  wamekuwa wakiwaaandikia jumuiya zao ili kuwakilisha kwa pamoja ujumbe wao wa Wiki ya maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo, wiki ambayo  kila mwaka huanza tarehe 18 na kumalizika tarehe 25 Januari sambamba na Siku Kuu ya uongofu wa Mtakatifu  Paulo Mtume wa watu.  Mbele ya dharura ya virusi vya corona na kwa mtazamo wa Pasaka hii ambayo siyo ya kawaida,hasa katika uzoefu wa kuishi katika kutengwa na upweke, wamehisi kwa kina dharura ya kutamka kwa mara nyingine tena neno la pamoja kuanzia na ujumbe wa kuwatia moyo na matumaini ya ufufuko wa Yesu.

Ujumbe wa kiekumene unasukumwa na Injili ya (28,4-8) mahali ambapo Luka anafafanua jinid ya ufufuko ulivyotokea akionesha tetemeko na Malaika wa Bwana aliyezungusha jiwe kubwa kutoka kaburini na kusababisha wote walikuwapo walinzi pia wanawake kuwa na hofu kubwa. Maelezo hayo yanaelezea kuwa kuna hofu ya kugandisha kama ilivyoonesha kwa walinzi, pia kuonesha  ambayo mchakato wa safari, ya wale wanawake kati yao ambao walikuwa wa kwanza kutangaza ufufuko. Na kwa maana hiyo ujumbe wao ni kuwataka waamini na wenye mapenzi mema kutokuwa na hofu.

Kama viongozi wa kidini wanahisi kuitwa kuwa kama wanawake watangazaji wa ufufuko, kwa maana  kifo hakina neno la mwisho na janga la corona linawapa mwamko wa nguvu  zaidi katika wito  wa kutaka  kuwa  pamoja katika dunia iliyo gawanyika na wakati huohuo inayounganishwa na mateso ya kibinadamu na ukarimu hawa kwa makini katika mahitaji ya wote kwa namna ya pekee  walio wa mwisho, maskini na walio baguliwa. Kwa hisia za shukrani hasa kwa Mungu wanawashukuru wale wote ambao wanajikita katika kutoa huduma ya wanaoteseka bila kuchoka. Aidha kwa kuukaribisha wito na mwaliko wa Papa Francisko kwa  Patriaki wa Kiekumene Bartolomeo, kwa Baraza Makanisa ya  Kiekumene, Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya, wanawaalika watu wote kuungana katika sala ambayo Yesu alitufundisha: “Baba Yetu uliye mbinguni…utuokoe na maovu yote”. Wanahitimisha ujumbe wao.

10 April 2020, 12:58