Katika siku kuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi,Mei Mosi, Baraza la Maaskofu Italia wataikabidhi nchi yao chini ya Ulinzi wa moyo safi wa  Bikira Maria. Katika siku kuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi,Mei Mosi, Baraza la Maaskofu Italia wataikabidhi nchi yao chini ya Ulinzi wa moyo safi wa Bikira Maria.  

Italia#coronavirus.Mei Mosi,Baraza la Maaskofu kuikabidhi Italia chini ya ulinzi wa Maria,Mama wa Mungu!

Katika siku ya Mei Mosi,Baraza la Maaskofu Italia,wameamua kukabidhi nchi chini ya Ulinzi wa moyo safi wa Bikira Maria,Mama wa Mungu.Mei Mosi ni Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi sambamba na mwanzo wa Mwezi wa Maria.Kwa njia hiyo inaleta maana kukabidhi kwa mama Maria mahangaiko ya kipindi cha janga la covid19.Aidha Baraza hili limetoa mchango wa milioni 2,400,000 kusaidia miundo ya aina 5 katika nchi inayokabaliana na vovid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tukiwa tunaelekea kuadhimisha Mei Mosi ambayo ni Siku Kuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi sambamba na siku ya Wafanyakazi Duniani, Rais wa Baraza la Maaskofu Nchini Italia amesema kuwa siku hiyo wataikabidhi nchi ya Italia chini ya ulinzi wa Moyo safi wa Bikira Maria, Mama wa Mungu. Kwa njia ya Video, Kardinali  Gaultiero Bassetti amethibitisha kuwa amepokea barua zaidi ya 300 zilizojazwa na upendo na ibada ya Bikira Maria ambazo zinatoa maombi yao na mapaenekezo kwa kwa nini nchi yao isiwekwe chini ya moyo safi wa Bikira Maria katika janga hili la corona, kwa wale wote wanatoa huduma katika mahospitali na ambao watatakiwa kuendelea kusaidia wakati ujao?

Kufuatia na muktadha wa kupokea mapendekezo hayo na kuhimizwa na waamini wengi, Baraza la Maaskofu nchini Italia, wametoa uamuzi wa kuikabidhi Nchi nzima ya Italia kwa Mama wa Mungu ili aweze kulinda na kuiokoa taifa hili katika janga la virusi vya corona.   Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza ni kwamba , tukio hili la kukabidhi Taifa la Italia litafanyika Ijumaa Mei Mosi saa tatu kamili za usiku, masaa ya Ulaya, ambapo kutakuwapo na wakati wa sala  kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Kisima cha Caravaggio, Jimbo la Cremona, katika wilaya ya  Bergamo nchini Italia.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo inasema: “Uchaguzi wa tarehe hii na mahali, ni ishara, kwani Mwezi Mei kwa hakika kiutamaduni ni mwezi ambao umetolewa kwa Mama Maria hivyo kuuanza Mwezi huu na Tendo la kukabidhi Nchi kwa Maria katika hali ya sasa, inapata   maana yake msingi kwa namna ya pekee nchini Italia hasa kwa wagonjwa, wahudumu wa afya  wote, madaktari, familia na marehemu wote”. Kwa mujibu wa uchaguzi wa mahali maombi hayo ni katika muktadha wa ndani ya mateso na uchungu mkubwa wa watu wa eneo hilo kwa wakati wa majaribu ya dharura ya kiafya. Kwani ni eneo lilolopata mkasa zaidi ya maeneo mengine nchini Italia. Vilevile wanaongeza  kuwa siyo tu hiyo, Mei Mosi hata hivyo ni Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi, Mchumba wa Maria, kwa namna ya pekee Baraza la Maaskofu wa Italia, wanawakabidhi wafanyakazi wote, kwa utambuzi wa mahangaiko na hofu inayotazama ya wakati wao ujao.

Vile vile Baraza la Maaskofu nchini Italia wametoa Euro milioni 2,400,000 kutoka mfuko wa fedha wa kusaidia uitwayo “Otto per mille” ili ziweze kusaidia miundo ya hospitali zinazoendelea kukabaliana na dharura ya kiafya iliyosababishwa na janga la virusi vya corona au covid-19. Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI), ni kwamba mchango wa sasa unakusudia kwenda Katika hali halisi 5 msingi: Mfuko wa Papa Paulo VI wa Pescara, Nyumba ya Mateso ya Mtakatifu Yohane Rotondo (San Giovanni Rorondo),  Kwa Watawa wa Fatebenefratelli,  katika Wilaya ya Lombardo-Veneta;  Taasisi ya Mabinti wa Mtakatifu Camillo, Roma, Treviso, Trento, Cremona na  Brescia, na Shirika la watawa wa Mama wa Msaada wa Mungu.

Majengo haya kwa dhati ni yale yanayojishugulisha na msaada wa wagonjwa ambao ni wengi sana kwa mfano: Mfuko wa Paulo VI huko Pescara Jimbo kuu limefungua nyumba tatu ya kutunza wazee, lenye uwezo wa kila mmoja nafasi ya watu 150  hadi sasa ambao wana virusi vya corona na kituo chenye wagonjwa walio karibu kufa(mahututi)  nafasi 50 na kituo cha kuishi nafasi 30 kwa watu wengine wenye matatizo; San Giovanni Rotondo katika eneo lililotengwa la  wenye covid ni nafasi ya vitanda 123  na vitanda 18 vya wagonjwa mahututi( intensive care); Wilaya ya Lombardo-Veneta kwa watawa wa  Fatebenefratelli majengo yao yote yameongeza nafasi kwa ajili ya wagonjwa wenye maambuziki ya  “Covid-19”; Taasisi ya Mabinti wa Mtakatifu Camillo  wameongeza nafasi katika eneo nafasi ya vitanda 321,watawa 86 na karibu wafanyakazi walei 2000: hatimaye katika Shirika la Watawa wa Mama wa Mungu msaada, wanajikita katika shughuli za watu walio wadhaifu katika makazi ya kiafya kwa wagonjwa na walemavu.

Maaskofu wa Italia wanasisitiza kuwa kupyaisha kwa namna hii ya wazi ya kutoa faraja, inafungu moyo na kutoa matumaini. Lazima kukumbuka kuwa mchango huo unaongezewa na ule wa awali euro milioni 6 ambazo zilitolewa katika wiki za mwanzo kwa ajili ya dharuru ya vituo vingine 7 vya kiafya na kijamii katoliki uliogawanywa katika maeneo ya kitaifa.

21 April 2020, 12:35