Vatican News
Maaskofu nchini Ireland Kaskazini wanapinga sheria ya utoaji mimba..Katika barua yao ya wazi kwa umma wanadhibitisha kuwa maisha ni matakatifu kuanzia kutungwa kwake hadi kifo cha kawaida. Maaskofu nchini Ireland Kaskazini wanapinga sheria ya utoaji mimba..Katika barua yao ya wazi kwa umma wanadhibitisha kuwa maisha ni matakatifu kuanzia kutungwa kwake hadi kifo cha kawaida.  (©unlimit3d - stock.adobe.com)

Ireland Kaskazini:Maaskofu wanapinga sheria ya utoaji mimba!

katika jamuiya ambayo tamaduni ya maisha inakuzwa na kushamiri,haki za binadamu tangu kutungwa kwake hadi kufa,za mama na watoto wao ambao hawajazaliwa zinapaswa kulindwa kila wakati.Ndiyo ujumbe wa Maaskofu wa Ireland ya Kaskazini wanaandika huku wakisasisha ahadi yao ya kufanya kazi na sekta zote za jamii ili utamaduni wa kulinda maisha uwe kwa wote kweli.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kulingana na sheria mpya yenye ukosefu wa haki kwa watoto wasio zaliwa  iliyotolewa Kaskazini mwa nchi ya Ireland 2019, maaskofu nchini humo  wameandika barua ya wazi kwa jamii nzima. Katika barua hiyo inaanza “Tangu leo nakuendelea watoto wasiyo zaliwa watabaki bila mlinzi. Hakuana ambaye anaweza kufanya lolote mara moja uamauzi  wa utoaji mimba utakapokuwa umetolewa na kutumika. Haya ni matarajio yenye kuleta wasiwasi katika jamii yetu mahali ambapo sehemu kubwa ya watu bado wanatafuta kuhamasisha thamani ya huruma  na heshima ya kila maisha ya mwandamu”. 

Sheria iliyokuwa tayari Uingereza

Kifungu cha sheria kilipitishwa mwaka jana na bunge la Uingereza ili kupanua kanuni kadhaa katika eneo la Ireland ya Kaskazini ambazo zilikuwa tayari  zimekwisha kuwapo nchini Uingereza. Mojawapo ya hayo, kiukweli ni sheria inayotaka kuhalalisha utoaji  wa mimba ambapo kisheria ni halali nchini Uingereza tangu 1967, mwaka ambao walipitisha  Sheria ya Utoaji wa Mimba  ikihusisha Uingereza, Scotland na Wales, ukiacha Ireland ya Kaskazini ambayo kwa wakati ule ilikuwa na Bunge lake wenyewe la kutunga sheria juu ya mambo kadhaa, ambapo uwezo wake  ulipitishwa katika Bunge la Uingereza kunako 1972.

Harakati za kuokoa maisha ya binadamu

Katika barua yao aidha Maaskofu hao wanaandika “Leo hii Nchi yote, sisi sote na hasa  madaktari, tuko tunatafuta kufanya kile kiwezekanacho ili kuokoa maisha ya binadamu. Wakati idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona inaongezeka, magazeti yanatukumbusha kuwa mara nyingi nyuma ya takwimu kuna watu halisi. Maisha yao yanahesabika kutegemea na umri au uwezo, jinsia au mazingira. Ili kuzuia kupoteza maisha ya binadamu, serikali ya Uingereza iko inawekeza sana kutoa rasilimali za lazima ili kutibu wagonjwa na kulinda maisha ya watu wote wanaotoa huduma yao wakiwa mstari wa mbele”. “Katika muktadha huu, tunasikitishwa na kusikitishwa na uamuzi wa serikali wa kuanzisha sheria kali za utoaji wa huduma za utoaji wa mimba  Kaskazini mwa Ireland, ambazo zinakwenda zaidi ya kile kinachotakiwa na sheria na kupuuza kabisa maoni ya raia wengi,” wameandika maaskofu.  Kwa mujibu wa  maaskofu, utumiaji wa sheria hii utawezesha  kuwa moja ya uhalifu mkuu wa utoaji mimba ulimwenguni.

Maisha ya kila mama na mtoto hasiye zaliwa ni muhimu

Katika kusisitiza maaskofu wanabainisha kuwa “Maisha ya kila mama na mtoto wake ambaye hajazaliwa ni muhimu. Hizi sheria mpya ni kwa kuzingatia dhana ya kisheria kuwa mtoto ambaye hajazaliwa hana haki, japokuwa mtoto anahitajika, hata hivyo, kila mtoto asiyezaliwa ni muhimu bila kujali umri au uwezo, jinsia au mazingira; ana haki ya kulindwa na jamii ambayo yeye ni ya kwake na ambayo anastahili kuheshimiwa. Hata mwanamke yeyote ambaye anakabiliwa na ujauzito ambao haukupangwa ni muhimu, anayo haki ya kutunzwa na kulindwa dhidi ya kila aina ya shinikizo kuhusu utoaji mimba.

Watu wote wenye mapenzi mema hawapaswi kukubali sheria ya utoaji mimba

Mkutano wa Bunge la Kaskazini siyo tu bila ushawishi: wanasiasa na watu wote wenye nia njema wanaotambua asili iliyo kamili ya sheria hawapaswi kukubali kwa upole tangazo lao, kwa maana hiyo  maaskofu wana watia  moyo kwamba “katika siku zijazo tunakusudia kuwasilisha kwa maandishi juu ya maoni yetu kuhusu sheria. Katika jamuiya ambayo tamaduni ya maisha inakuzwa na kushamiri, haki hizi za mama na watoto wao ambao hawajazaliwa zinapaswa kulindwa kila wakati. Sisi, maaskofu Katoliki wa Ireland ya Kaskazini tunasasisha ahadi yetu ya kufanya kazi na sekta zote za jamii, ili utamaduni huu wa maisha uwe ukweli kwa wote.

02 April 2020, 08:53