INDONESIA #coronavirus:Askofu wa Ketapang ashauri vijana wawe mstari wa mbele kusaidia masikini zaidi!
Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican
Katika Barua kwa ajili ya Tume ya vijana ya Baraza la maaskofu nchini Indonesia iliyoangazwa tarehe 31 Machi 2020 inasema: “kuweni makini na kusaidia watu masikini na walio katika mazingira magumu, ninyi wenyewe na familia zenu, kwa kutumia zana na fursa za njia za mawasiliano kwa ajili ya kuwasadia wengine ili wakidhi mahitaji yao. Katika barua hiyo kwa mujibu wa Shirika la habari UCA News, askofu anawaalika vijana wakatoliki wawasaidie masikini zaidi na wawe wabunifu katika mapambano dhidi ya Covid-19..
Vijana fuateni hatua zote zilizochukuliwa
Askofu wa Ketapang, katika Wilaya ya Kalimantan magharibu anawakumbusha vijana kufuata hatua zilizowekwa ili kuzuia maambukizi yaani wakae nyumbani kuzuia usambaaji zaidi na kufanya mikutano yao kupitia mitandao na kuwa makini katika jamii, ili kuweza kuruhusu wahudumu wafanye shughuli yao katika huduma kwa wale tu wenye kuhitaji matibabu muhimu ya dharura. Na zaidi anawashauri wasiache kamwe hata mmoja peke yake na wasiache hata mmoja ahisi kudharauliwa katika kipindi hiki kigumu.
Ni wakati sasa wa kufanya kila liwezekanalo
Ni kipindi chenu sasa cha kufanya lolote liwezekanalo ulimwenguni na vizuizi vya kimwili haviwezi kuwa vizingiti . Kwa njia ya ubunifu vijana wanaweza kuwa viongozi wa mstari wa mbele katika hali hii na wanaweza kushinda kwa pamoja kipindi hiki kigumu, anaandika asikofu. “Ni wakati sasa kwenu kugeuka kuwa mstari wa mbele kwa kuwa mifano halisi ambayo wagonjwa, walemavu na maskini wanaweza kupata chakula cha bure”.
Vijana ni wabunifu, wanaweza kama ambavyo tayari katika mazingira
Aidha Askofu anaamini kwamba kile ambacho vijana wanaweza kutafakari ni kama kile ambacho wao tayari wanafanyana kwa ajili ya mazingira, kwa ajili ya Kanisa, jumuiya ya kimataifa, na wanaweza kusaidia maskini waliokumbwa na virusi na wanaweza kufanya kwa namna ya ubunifu na kutumia uwezekano wa njia zote za kisasa. Nchini Indonesia takwimu ya maambukizi ya covid-19 tarehe 31 Machi 2020 ilikuwa ni 1,528 na vifo 136.